Soma inawakaribisha wapenzi wote wa fasihi kwenye mjumuiko wa tamasha la Nne la fasihi litakalofanyika wiki hii kuanzia tarehe 27/11/09 hadi 29/11/09 - Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Shughuli za fasihi na maonyesho mbalimbali yatafanyika ikiwa ni pamoja na maonyesho ya kazi mbalimbali za usomaji na uandishi wa fasihi, kazi za ubunifu, mijadala ya kirika na masuala ya kijamii, simulizi za hadithi, tambo za kishairi, maonyesho ya vipaji kwa watoto na vijana, filamu ya wachawi wa bongo itaoneshwa, na pia maonyesho lukuki kutoka kwa wasanii na wanafasihi wengineo watajumuika pamoja na kutumbuiza pamoja katika siku zote hizo tatu za tamasha.

Unakaribishwa kuja na tungo, mashairi na kazi zinginezo za kifasihi na kisanii ambazo ungependa kuzionyesha na/ama kuzijadili pamoja na wadau wa jamii ya usomaji, ubunifu na utamaduni.
Siku na Muda na Tukio:
*Ijumaa 28 Novemba 2009, Saa 11 jioni hadi 4:00 usiku (Usiku wa Ushairi)

*Jumamosi 28 Novemba 2009, Saa 3 asubuhi hadi saa 8:00 mchana
(Watoto na Fasihi) Saa 9.00 jioni hadi 2.00 usiku
(ulingo wa waandishi na wasomaji)
*Jumapili 29 Novemba 2009, Saa 8 jioni hadi saa 11jioni (Mdahalo)

“Karibu Soma ujenge maarifa, ufurahie utamaduni na uburudike katika mandhari murua”
Vinywaji na vitafunwa vitapatikana kwa bei nafuu ~ karibuni

Edna Msumba/Rachel Thomas
E & D Readership and Development Agency
53 Mlingotini Circle,
Regent Estate,
Kinondoni,
P.O Box 4460
Dar Es Salaam,
Tanzania
Tel: +255 22 27772759
Cell: +255 713450856/713089775



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. aliye design logo ya soma alifikiria kwa makini kwa yule ambaye hafahamu kiswahili ataielewaje hiyo logo.... SOMALI..!!

    Papa Stan
    Moshi. kilimanjaro

    ReplyDelete
  2. habari za logo zinakujaje wewe kama msomaji nenda kasome kama vipi kauka watz bwana kwanza hatunautamaduni wa kujisomea kwa hiyo twende tukamajumuike. Mama Demere na Mama Elishi Hongereni sana tutakua pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...