AHSANTE SANA NDUGU MDAU KWA MADA YAKO YA SOFA PAKA. KWA UFUPI MIMI NI MMOJA YA WADAU MCHEZA SOKA NA PIA NI MPENZI SANA WA MAENDELEO YA SOKA YA HAPO NYUMBANI TANZANIA, AFRIKA MASHARIKI NA AFRIKA KWA UJUMLA.
KWA UFUPI NAPENDA KUIPONGEZA TIMU YA DAR YOUNG AFRICANS KWA KUTUWAKILISHA VIZURI NA HATIMAE KUTWAA UBINGWA. PILI NAPENDA KUIPONGEZA TIMU YA SOFAPAKA KWA KUONYESHA SOKA NZURI NA YENYE USHINDANI NA HATIMAE KUNYAKUA NAFASI YA PILI.BILA KUSAHAU SIMBA SC. HII NI HATUA KUBWA SANA KWA KLABU ILIYOANZISHWA SI CHINI YA MIKA KUMI ILIYOPITA.
PIA HONGERENI SANA SOFAPAKA KWA KUJITANGAZA VIZURI NA HASA KWA KUTUMIA NJIA YA MTANDAO YANI WEBSITE YENU ILIYOTENGENEZWA KWA UTAALAMU KABISA. HAKIKA UNGENIULIZA MIMI KAMA NILIKUWA NAJUA SOFAPAKA NI NINI BASI JIBU LANGU LINGEKUWA KICHEKESHO KIDOGO. LABDA NINGEJARIBU KULITENGANISHA NENO HILO KATIKA MANENO MAWILI YA SOFA NA PAKA. HAHAHA NINA UHAKIKA HILI NDIO LILIKUWA WAZO LA WENZANGU WENGI TU HASA HUKU UGHAIBUNI. LAKINI SI PUNDE TU NIMESHAJUA KUWA NINI MAANA YA SOFAPAKA NA HATA BAADA YA KUTIZAMA WEBSITE YAO NIKAJIFUNZA KITU KINGINE KIPYA YANI BLUE TRIANGLE CEMENT AMBAO NI WADHAMINI WAKUU WA TIMU HII.
TUKICHUKULIA MFANO HUU MDOGO TUU TUTAJIFUNZA KUWA NJIA HII YA MTANDAO INASAIDIA KUSAMBAZA HABARI KIURAHISI KABISA NA KWA HARAKA SANA NA HATA KWA DUNIA NZIMA.

SASA KAMA MDAU MWENZANGU ALIVYOSEMA
(1)JE TIMU ZETU KONGWE ZA YANGA NA SIMBA ZINAJUFUNZA NINI KATIKA HILI?? HASA KATIKA WAKATI HUU WA ULIMWENGU WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA??
(2) JE CHAMA CHA SOKA (TTF) NAO WANAJIFUNZA NINI KUHUSU MADA HII YA SOFAPAKA??
LABDA KWA KUWASAIDIA KUJIBU TU MAANA WAO WAKO BUSY SANA KATIKA KUHESABU HELA ZA MAPATO YA MILANGONI NA BILA KUJUA WAZITUMIAJE. JE WADHAMINI WA SOKA HAPO NYUMBANI KUANZIA VODACOM, KILIMANJARO, TUSKER WANALIONAJE SWALA HILI LA WEBSITE HASA UKIZINGATIA WAO KAMA WADHAMINI WANAFANYA HIVYO HILI KUPATA PUBLICITY AU KUJITANGAZA??
TUKIANZIA NA VILABU VYETU VIKUBWA VYA YANGA NA SIMBA, TUNAVIPENDA SANA!! NA SISI KAMA WATANZANIA HATUNA LINGINE LA KUJIVUNIA KATIKA HISTORIA YA SOKA LETU ZAIDI YA UMAARUFU NA UKONGWE WA VILABU HIVI. IKUMBUKWE SIJASEMA MAFANIKIO NIMESEMA UKONGWE NA UMAARUFU.
TUKIJA KATIKA MAFANIKIO AAH HAPO MTATUWIA RADHI KWANI HATUJAONA KITU BADO TUTAISHIA NA USHABIKI WETU WA NYUMBANI TUU "MNYAMA KAMFUNGA YANGA AU ULEE WA KANDAMBILI KAMFUNGA SIMBA"" HAHAHA BILA KUSAHAU NA ZILE NYIMBO ZETU SIMBA KAINAMA YANGA .....!! MTAMALIZIA WENYEWE!!
IKIJA ENYIMBA AU AL-HILALY BASI SISI TUMBO JOTO BABAKE!! TURUDI KWENYE MADA MIMI NAONA UTUMIAJI WA MTANDAO NDIO NJIA RAHISI YA KUJITANGAZA ZAIDI KULIKO NJIA YEYOTE ILE. MIMI LEO NAIJUA TIMU YA SOFAPAKA NA SIMENTI YA BLUE TRIANGLE KITU AMBACHO NILIKUWA SIKIJUI JUST FEW HOURS AGO.
SASA TUKICHUKULIA MFANO HALISI WA VILABU VYETU HIVI AMBAVYO HIVI SASA VINADHAMINIWA NA KILIMANJARO BEER. JE HUWEZI KUONA KUWA KUNA MTU KAMA MIMI SOMEWHERE IN THIS WORLD HAIJUI YANGA AU SIMBA NA KILIMNJARO BEER NA KAMA MNGEKUWA NA MITANDAO INGEKUWA RAHISI KWA MTU HUYU KUWATAMBUA NA KUITAMBUA BEER HII??
FAIDA NYINGINE YA KUJITANGAZA NI KUWEZA KUWATANGAZA WACHEZAJI WENU NA KUONYESHA TAKWIMU ZAO AMBAZO ZITAWASAIDIA KUPATA SOKO LA KULIPWA. PIA NJIA HII YA MTANDAO ITASAIDIA KUVUTIA WAPENZI WENGI ZAIDI AMBAO WATAKUWA WANAVUTIWA NA HABARI ZA KLABU NA WACHEZAJI KWA UJUMLA NA KUFANYA WAO KUFURIKA VIWANJANI KUJA KUWAONA LIVE. WATU WAKIFURIKA UWANJANI NADHANI KWA AKILI YANGU FUPI INANIAMBIA KUWA NDIO MAPATO YA VILABU YANAONGEZEKA.

TUKIJA KWA WADHAMNI YANI KILIMANJARO, TUSKER, VODACOM, NMB NA VITU KAMA HIVYO LABDA NIWAULIZE NINI MTAZAMO WAO WA KIBIASHARA BAADA YA MIAKA 50? JE NI KUUZA VINYWAJI NA SIMU ZAO HADI NEWALA NA BIHARAMURO AU CAIRO HADI BEIJING?? KAMA JIBU NI JUST KUUZA BIDHAA KWA HAPO HAPO TANZANIA BASI HILO MMESHALIKAMILISHA NA SASA MSUBIRI KUHUJUMU MAKAMPUNI NA MYAFIRISI NA KUSAHAU KUWA KUNA WAJUKUU ZENU WANATAKIWA KURITHI KUTOKA KWENU.
NA KAMA NIA NI KUUZA BIDHAA HADI NJE YA MIPAKA, JE TUTAFIKA? NA KAMA HADII HII LEO VILABU VYA LIGI KUU, WADHAMNI NA VYAMA VYA SOKA HAVINA HATA WEBSITE?? AU TUNAJIDANGAYA NA HAO WASHABIKI 5000 WANAOJAZA UWANJA WA JAMHURI, KAUNDA, SOKOINE?
OOH NAJUA KUWA FASIHI INATEMBEA LAKINI KUMBUKA BY THE TIME INAWAFIKIA WALENGWA ITAKUWA TAYARI INA MAPUNGUFU NIKIMAANISHA KUWA KILIMANJARO BEER ITAKUWA NJARO BEER, TUSKER WATAIITA TAKA NA HATA VODACOM WATATAMKA KAMA ODACOME??
JE IKIWA SASA MITANDAO INAWAFIKIA HATA WANAKIJIJI KULE IFUNDA KWANI SASA WANA INTERNET HATA KWENYE SIMU ZAO INGEKUWA RAHISI KUWAFIKISHIA WALENGWA UJUMBE MOJA KWA MOJA?? HII LEO KONYAGI NI KINYWAJI MAARUFU HAPA USA? JE MNADHANI HILO HALIWEZEKANI KWA TUSKER NA KILIMNJARO BEER??
NA LA MWISHO NA PENDA KUTOA MASIKITIKO YANGU KWA LIGI KUU YA KENYA NA CHAMA SHIRIKISHI. KWAKWELI BAADA YA KUTAZAMA PICHA ZA SOFAPAKA NILISIKITIKA SANA. HIVI KWELI HII NI LIGI AMBAYO ILIKUWA IMEBEBA VILABU VIBABE KAMA GOR MAHIA, AFC LEOPRADS, BREWERIES YA KENYA??
MIMI WAKATI HUO NIKIWA MDOGO NILIKUWA NAOGOPA NIKISIKIA YANGA AU SIMBA ANACHEZA NA VILABU HIVI. AU WADAU MNASEMAJE?? LAKINI LEO HII NI HAIBU UKIANGALIA MAENDELEO YA LIGI HII. VIWANJA HAVIJAI KABISA!! YANI HATA WATU MIA MBILI HAWAFIKI?? MECHI ZINGINGE ZINACHEZEWA KATIKA VIWANJA KAMA MWANANYAMALA SHULENI?? HIVI KWELI NI HII LIGI AMBAYO ILIKUWA INATOA WAKINA PETER DAWO, THOBIAS OCHOLA "JOGOO"? MAHMOOD ABBAS? PETER OTIENO? KADENGE NA KADHALIKA??
LAKINI JIBU MNALO WENYEWE KUWA UBADHILIFU NDIO UMEPELEKEA HAYO NA LEO MNAYAONA. IKUMBUKWE KUWA CHAMA CHA SOKA CHA KENYA KILISHAFUNGIWA NA FIFA KWA AJILI YA UBADHILIFU WA FEDHA. JE NI MDAHAMNI GANI ATAKUWA TAYARI KUDHAMINI LIGI WAKATI WATU WANASHIBISHA MATUMBO YAO??
JE NI SHABIKI GANI ATAKUWA TAYARI KUACHA MECHI YA MANCHESTER, LIVERPOOL NA ARSENAL KIDEONI ILI AKATAZAME GOR MAHIA NA SOFAPAKA?? JIBU MNALO WENYEWE NA PIA NI FUNDISHO KWA CHAMA CHA SOKA CHA TANZANIA YANI TTF. WASWAZI WANASEMA UKIONA MWENZIO KANYOLEWA BASI WEWE TIA MAJI. KULIKUWA NA WAKATI UWANJA WA TAIFA UNAJAA HATA AKICHEZA NYOTA NYEKUNDU NA LIPULI YA IRINGA!! LEO HII UWANJA HAUJAI MPAKA ACHEZE YANGA NA SIMBA?? KWA TAARIFA YENU NASI TUNAELEKEA HUKO HUKO KWA WATANI WA JADI KENYA.

LA MWISHO KABISA NI USHAURI WA BURE KWENU:
(1) TIMU ZIWE NA WEBSITES NA VIJARIDA (HEKO YANGA), WACHEZAJI WATANGAZWE NA VILABU PAMOJA NA WADHAMINI KWA KUWATUMIA WAO KATIKA MATANGAZO YOTE KUANZIA BILLBOARDS NA HATA VIDEONI. HAINA MAANA KUMTUMIA MTU ASIYEJULIKANA WAKATI MCHEZAJI ANA INFLUENCE KUBWA KULIKO MTU WA KAWAIDA. HII PIA ITAWAONGEZEA VIPATO WACHEZAJI NA KUWAFANYA WAONGEZE JUHUDI KWANI WAKIWA MAARUFU WATAPATA MIKATABA YA MATANGAZO. HILI LITAONGEZA USHINDANI WA LIGI. IKUMBUKWE WAO NI AIDLES! HII PIA ITAWAFANYA HATA WATOTO WETU WAVUTIWE NA MPIRA HIVYO KIBIDIISHA ZAIDI KATIKA MAZOEZI.
(2) PIA MAKAMPUNI YATAWEZA KUJITANGAZA ZAIDI KAMA TIMU ZIKIFANYA VIZURI ZAIDI NA KUUZA BIDHAA NJE YA MIPAKA YETU. PIA NINGEPENDA KIONGEZWE KIPENGELE KATIKA MIKATABA HIYO KUWA TIMU LAZIMA ZIWE NA WEBSITES ZA KUDUMU.
(3)KWA CHAMA CHA SOKA HILI LITASADIA KATIKA KUKUSANYA NA KUTAWANYA HABARI NJE NA NDANI YA MIPAKA YETU NA KUIFANYA LIGI IJUILIKANE ZAIDI NA KUPATA WADHAMNI ZAIDI. PIA KUKIFANYA CHAMA CHA SOKA NA VILABU KUENDESHA SHUGHULI ZAO KIUFANISI NA UWAZI ZAIDI(TRANSPARENT).
PENDEKEZO NINGEPENDA KUPENDEKEZA WEBSITE YA SUPERSPORT UNITED, STARS UNITED (www.starsunitedfc.webs.com) ZIWE MFANO WA KUIGWA NA VILABU VYETU HAPO NYUMBANI(PITIA). HONGERA AZAM FC, MTIBWA SUGAR NA AFRICAN LYONS (INGAWA NA WENYEWE NI WAVIVU KU UPDATE HABARI ZAO).
MWISHO KABISA MAANA SASA NIMESHAKUWA KAMA MWALIMU WANGU MMOJA WA AZANIA AKISEMA MWISHO BASI MWISHO UNAKUWA MREFU ZAIDI KULIKO HABARI YENYEWE!
NINGEOMBA VYUO VIKUU NYUMBANI VIANZISHE KOZI MAALUMU YA URATIBU WA MICHEZO AU KIDHUNGU WANAITA SPORTS MANAGEMENT ILI WATANZANIA WANUFAIKE NA HILO NA PIA NA SISI TULIO UGHAIBUNI NI MOJA YA DEGREE ZINAZOONGOZA KWA MALIPO BASI TUKIPATA WASAA BASI TUFANYE HIMA ILI TUKALISAIDIE TAIFA HILI MAANA LIKO GIZANI!!
AHSANTENI NA NAOMBA TUJADILI MADA HII!
MDAU USA- RIVAAAAA!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu nakupongeza kwa article nzuri na kutoa changamoto, ila jifunze kuandika vitu muhimu tu maana watu hawana muda wa kusoma all these "craps".... jamani hata kuandika kiswahili pia tabu...

    ReplyDelete
  2. Ni vyema mdau umeileta hii mada hapa. Lakini je wahusika wataiona kweli? Ushauri wangu pamoja na kuwa umeileta hapa, kama itawezekana ungeituma kwa email (najua baada ya kuzitafuta na kuzipata itachukua muda ila usife moyo, ndo mwanzo wa mazuri) kwenye anuani za wadhamini wote uliowataja, timu husika za ligi Tz(najua wengine hawana email), TFF(hawa wanaweza wakawa kiungo kizuri cha time zote kufika ujumbe) na n.k. Labda inaweza ikaharakisha ujumbe kufikia walengwa. Ila hili ni wazo langu tu katika kutaka huu ujumbe mwanana uwafikie walengwa, huku sisi tukiendelea ku-discuss hapa.Huenda ikawa pia wanajua ila kuendelea kuwakumbusha ni jukumu letu wananchi/wapenzi wa soka pia.

    Nawakilisha.
    Mdauzzy

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa TFF na hao wawili ndio wanaoua soka letu...soka limekuwa kichaka cha wezi, kwasababu hakuna usimamizi mzuri na kila anaejaribu kurekebusha mambo wanampiga vita.

    Ili soka ikuwe hapa Tanzania tunahitaji viongozi wa kweli ktk soka.. tunao watanzania wanaoupenda sana mpira lakini wataishia kupenda Arsenal, Manchester, Liverpool, Real Madrid n.k.
    wachezaji nao wakuwa wakitumiwa tu kama mwiko wa kupikia unaungua lakini hauli chakula.

    Waamuzi ni vibaraka wakupanga matokeo, hilo linasababisha kiwango kushuka kwani wachezaji hapati ushindani wa kweli, ukiwapeleka kwenye mpira wa kweli wanachemsha. hivyo wazunguka red na green mpaka wanazeeka. halafu mnataka wachezaji wa kulipwa. mtawapata wapi?

    Fukuzeni hilo genge la wezi ndio mpira utakua.

    ReplyDelete
  4. We anon. wa kwanza MESSAGE SENT! Wewe si editor wa hii globu.

    ReplyDelete
  5. suala hapa sio hoja wa babaake haja... hapa ni kuongelea ukweli na ukweli ni kwamba vijana wa jangwani walipopata taarifa kwamba porini kuna mnyama simba walienda wakamkamata wakachinja wakala boxing day wakaambiwa paka ana roho saba hata ukipiga vipi hafi wakamkamata wakapondaponda mpaka akafa... watu wanasema ukienda nyumba ya mtu ukamuua baba mwenye nyumba na kumrithi mke wake basi ukweli watoto wake watakuita baba... hivyo basi tumeua bingwa wa kenya na sasa tunatangaza rasmi bingwa wa kenya kwa sasa ni "DAR YOUNG AFRICA SPORT CLUB" kama unabisha katiza mitaa ya jangwani saa moja moja usiku ukutane na vijana wa ngetwa wakutoe ujinga au panda kwenye mnazi kisha jiachie

    ReplyDelete
  6. very true mdau ila mi navyowajua watanzania hilo litaongelwa leo kesho limeisha yani kama tumelogwa

    ReplyDelete
  7. Ukweli ni kuwa tumekosa viongozi wenye "Vision" sio tu kwenye clubs kama Simba na Yanga bali hata TFF. Kwa sababu TFF inaundwa na viongozi wa Clubs hatuwezi kuwa na mabadiliko ya kweli mana ni walewale, watu wabinafsi na wasiopenda kuona mbele, watu wanaojali pale walipo tu. Inashangaza kwa nini TFF haiwezi kujiendesha kibiashara....Ona ligi kubwa kama za Ulaya, ni vyama vya soka ndio vinaweka changamoto kuendeleza clubs mana mfumo wote ni wa kibiashara.
    Kuna mapungufu mengi sana kwenye mfumo wetu wa soka, na tunahitaji wataalamu wa kuweka mipango dhabiti. Nimejaribu kutafuta contact za mwenyekiti wa TFF au club kubwa kama Simba na Yanga ili niwape ushauri wa kitaalamu tena kwa bure lakini hakuna mahali pa kupata hizo contacts. Kama kuna mtu anazo naomba apost...mi nipo nje ya nchi lakini natamani sana kutoa mchango wangu wa jinsi gani clubs na TFF wanaweza kuwa matajiri na kufanya soka kuwa burudani kubwa kwa Watanzania na sehemu nyingine za ulimwengu. Mimi ni nina utaalamu wa Strategic management I can offer a free consultation kama hawa viongozi wakiwa tayari kushirikiana, na ndani ya miaka miwili wataona matokeo yake......
    Basi tusipende kulaumu sana bali tuwasaidie hawa tunaowaona hawafanyi kitu kizuri wapige hatua....

    ReplyDelete
  8. Yaani munakuwa kama hamuijui nchi yenu!! Hivi niambieni ni sekta au fani ipi ambayo inafanya kazi vizuri?? Mpira ni symptom ya matatizo makubwa yaliyopo nchini. Angalia mashindano mbalimbali ya mpira ya kimataifa yanafanyika lakini nchi ya Tanzania haipo. Tunakuwa kama wahindi ambao mpira si fani yao (angalau wanangaa kwenye fani nyingine).

    Kuwa na website ni jambo jema. Ila ukiwa na kitu kizuri ambacho unakiamini ni kizuri huoni aibu kukionyesha kwa watu. Tunaona aibu kuweka mambo yetu kwenye web kwa sababu hatuamini kama ni mazuri. Sisi wenyewe hatuendi kuutazama mpira wetu, tutamwonyesha nani nje na aupende mpira wetu.

    Kila mtu atafakari mwenyewe tatizo nini kabla ya kulalama. It all starts in the mind!! tuache kuridhika kwa vitu vidogo na kujifanya rahisi (cheap).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...