Mlezi wa Mtandao wa wanataaluma (Tanzania Professionals Network - TPN) Dk. Maua Daftari (shoto) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania na Meya wa Jiji la Dar, Alhaj Adam Kimbisa, msaada wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya shilingi 1.4m/- vilivyotolewa na wadau baada ya kuhamasishwa na Jamii Forum, Globu ya Jamii, TPN na mwanakijiji.com kusaidia waathirika wa mafuriko huko Kilosa katika sherehe fupi iliyofanyika jana jioni ofisi za Msalaba Mwekundu jijini. Wengine wanaoshuhudia toka shoto ni Rais wa TPN Mzalendo Sanctus Mtsimbe, Mike Mushi na Max Melo (wakurugenzi wa Jamii Forum) na ankal wa Globu ya Jamii. Misaada hii ni awamu ya kwanza ya michango hiyo ambayo bado inaendelea kutolewa
Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Meya wa Jiji la Dar Alhaj Adam Kimbisa akimshukuru Dk. Maua Daftari baada ya kupokea mchango wa pesa taslimu wa shilingi milioni moja na elfu 68 na senti 80 zilizochangwa na wadau mbalimbali duniani kusaidia waathirika wa mafuriko huko Kilosa.
Picha zingine na maelezo ya namna ya kuchangia ndugu zetu
----------------------
Globu ya Jamii kwa kushirikiana na TPN, http://www.jamiiforums.com/ na www.mwanakijiji.com tunatoa shukrani za dhati kwa wale wote waliojitolea kuchangia ndugu zetu walioathirika na mafuriko huko Kilosa, mkoani Morogoro. Msaada ni msaada tu, hauna udogo wala ukubwa, muhimu ni tendo (gesture) ya kuguswa na matatizo ya wenzetu na kuamua kusaidia.
Michango inaendelea kupokelewa na si lazima iwe ni pesa taslimu bali hata misaada ya mablanketi, vyakula na maji, madawa, nguo, viatu na kadhalika. Bofya hapo juu kujua namna ya kufikisha msaada wako huku ukikumbuka kwamba kutoa si utajiri.

Inawezekana: Watanzania KWA Watanzania Harambee ya Mafuriko Kilosa
-Michuzi

------------------------------------

JINSI YA KUCHANGIA:
Tumebuni njia mbalimbali za kuweza kuchangia vitu kama vyandarua, maboksi ya maji safi, nguo, madawa (ambayo hayajapita muda au kufunguliwa), mahitaji ya watoto na kina mama n.k.

A: MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
P.O. Box 1133
Dar es Salaam
Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843

Email: logistics@raha.com

B: KUTUMIA MTANDAO WA WANATAALUMA WA TANZANIA (TPN).
Hivyo TPN itakusanya michango yetu kwa njia mbalimbali hapa chini na kuiwasilisha kwa TRCS na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kampeni hii.

2. Kuingiza Benki au kuhamishia fedha benki(bank deposit and transfers):
· Jina la Akaunti: Tanzania Professionals Network,
· Jina la Benki: CRDB Bank ; Tawi: Lumumba
· Jiji: Dar Es Salaam; Nchi: Tanzania
· Swift Code: CORUTZ TZ
· US $ (Fedha za kigeni) A/C No: 02J1 007 608 900;
· TZS A/C No: 01J1 007 608 901

C: KUTUMIA MITANDAO YA SIMU
3. M-Pesa (Vodacom): 0768 777 888
4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88
5. Zap (Zain) 0784 00 88 99

6. Michango ya kutumia makato ya kila siku ya Airtime za simu:
“Changia Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047.

7. Western Union — Tuma kwa jina la: Mr. Emmanuel Mmari; TPN Finance and Administrative Manager; Dar Es Salaam; Tanzania. Tuma nakala ya MTCN kwa president@tpn.co.tz, info@jamiiforums.com na
mwanakijiji@jamiiforums.com na issamichuzi@gmail.com ili kuweka rekodi sahihi.

8: Michango ya vitu mbalimbali: Ofisi za TPN — Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS; Ghorofa ya kwanza, karibu na TBC (RTD) Radio. Piga simu 0715 740 047 kwa kupata msaada wa kuja kuchukua vitu kama huna usafiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...