Rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua
anauguza matatizo ya moyo na figo
Makamu wa Rais Goodluck Jonathan (shoto)
anakuwa kaimu Rais wa Nigeria.

Bunge la Senate nchini Nigeria, kutokana na rais Umaru Yar'Adua kuugua kwa muda sasa, limepiga kura na kuamua kumkabidhi madaraka Makamu wa Rais, Goodluck Jonathan.

Katika mjadala mkali bungeni, maseneta hao walisema hatua hiyo ilibidi ili kuiepusha nchi hiyo kwa kukosa uongozi thabiti, na kuwepo pengo katika uongozi, jambo ambalo linazuia maendeleo.

Pengo hilo la uongozi limekuwepo nchini Nigeria tangu mwezi Novemba mwaka jana, wakati Umaru Yar'Adua alipougua na kwenda Saudi Arabia kupata matibabu.


Waandishi wa habari wanaelezea kwamba bado haijafahamika wazi ikiwa kura ya bunge ina uwezo kamili katika kumkabidhi uongozi makamu wa rais, Goodluck Jonathan.
Bunge dogo la Nigeria, leo pia linajadili tatizo hilo la uongozi.
Rais Umaru Yar'Adua anaendelea kupata matibabu nchini Saudi Arabia. Mabaraza yote mawili ya bunge yalipitisha mswada Jumanne hii unaosema Bw Jonathan "kuanzia sasa atasisimia shughuli zote za ofisi ya rais, amiri jeshi mkuu wa majeshi...kama kaimu rais."

Baraza la Seneti la bunge hilo la Nigeria lilipitisha mswaada wa pili unaosema Bw Jonathan ataacha kuwa kaimu rais mara tu Bw Yar'Adua atakapolijulisha bunge kuwa amerejea kutoka likizo ya matibabu.

Katiba ya Nigeria inasema makamu rais anaweza kuchukua madaraka pale tu rais atakapoandika barua kwa bunge akisema kuwa hawezi kufanya kazi zake kama rais. Bw Yar'Adua hajaandika barua kama hiyo.
Hata hivyo, Rais wa baraza la Seneti David Mark alisema Jumanne kuwa mahojiano aliyofanya Rais Yar'Adua na shirika la utangazaji la Uingereza - BBC - mwezi uliopita yalikuwa ushahidi kuwa yuko katika "likizo ya matibabu."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mambo yetu ya Afrika...Mchezaji wa Togo anaechezea Aston Villa alisema Nothin is serious in Africa...Salaam za Rambirambi kutoka CAF ni kuifungia Togo miaka minne.

    Sasa hapa angalia watu wazima wanaamua kabisa kusema mahojiano ya kwenye Redio ni ushahidi....Hii ni ajabu kabisa.
    Hivyo hapa bunge limefanya uamuzi ambao ni illegal na kinyume na katiba.

    Katiba ya Nigeria inaruhusu njia mbili moja ni hiyo ya barua na mbili ni Bunge kupiga kura ya kumuondoa raisi(Impeachment) hakuna sehemu inayosema eti bunge limkabidhi madaraka Makamu wa Rais....Kwa maneno mengine watu wazima wanaamua kushooiya.

    Tatizo hapa ni kuwa kwa utaratibu usio na maandishi Rais hutoka kasikazini(Waislam wengi) na Kusini(Wakristo Wengi) na Baada ya Obasanjo wa kusini hii ni zamu ya Kaskazini (Yadua) hivyo akimuachia Jonathan ambae ni wa kusini utaratibu utavurugwa ....Na tatizo Jeshi wengi ni Kaskazini.
    Na ndio maana wanaogopana ...Haya tusubiri matokeo.
    Mdau

    ReplyDelete
  2. nchi gani toka desember mwaka jana raisi ni mgonjwa na tena yuko nje ya nchi halafu bado anahesabika ni kiongozi ndio maana bara la afrika ni maskini kabisa duniani

    ReplyDelete
  3. Nimependa neno hili - "kukosa uongozi thabiti"

    ReplyDelete
  4. hakuna jipya asa afrika mambo ya siasa

    sishangai kbs hii kitu,maombi

    vyovyote tu

    ReplyDelete
  5. wewe unyesema nchi gani toka december mpka sas nchi haina Rais Tanzania mh Nkapa alipokuwa matibabu for 3months mbona hukusema vitu raisi ni mtu kama wewe ugonjwa hauchagui kiongozi wala mlalahoi hapo ndoo Mungu alicheza mambo yakijifanya mungu watu tuache kabisa

    ReplyDelete
  6. kujifanya MUNGU ni ni pale binadamu anapomuhukumu binadamu mwenzake adhabu ya KIFO ila raisi akiwa mgonjwa anatakiwa kukabidhi madaraka kwa makamu wake tena raisi wa nigeria ni mgonjwa sana

    ReplyDelete
  7. wewe mdau unayesema sasa ni zamu ya kaskazini kuongoza nchi na unasema unasubiri kuona wanajeshi wanaanzisha mapinduzi je unafikiri wanajeshi hawaogoi kifo?je jiulize DADIS KAMALA yupo mahututi je hakuwa mwanajeshi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...