Hekaheka katikati ya uwanja wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uwanja wa Uhuru Jijini leo, ambapo vinara wa ligi hiyo wamejiongezea pointi 3 muhimu kwa kuifunga Manyema Fc bao 2-0.

Walikuwa ni washambuliaji hatari Ulimboka Mwakingwe na Mussa Hassan Mgosi waliofunga mabao hayo, ingawa katika Mchezo huo uliokuwa na upinzani katika kipindi cha kwanza uliichukua timu ya simba muda mrefu mpaka kufanikiwa kupenya ngome ya Manyema na kufanikiwa kupata goli la kwanza kwenye dakika ya 63 ya mchezo huo kwa goli safi lililofungwa na Ulimboka Mwakingwe.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa timu ya Manyema aka "Mkuki wa Sumu" baada ya kuwachezea vibaya Mussa Mgosi katika eneo la hatari hivyo kusababisha adhabu ya Penati katika lango lao na kumfanya mchezaji huyohuyo Mussa Mgosi kufunga goli katika dakika ya 71.

Kwa matokeo hayo ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manyema Rengars ina maana timu ya Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi 46 ikiwa ni tofauti ya poiti 10 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga wanaofuatia kwa pointi 36.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Duuh Ankal punguza uyanga jana tulipata habari mapema na mipicha mikubwa mikubwa leo hii habari unatuletea muda wadaku na kapicha kadooogo.
    wako
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  2. Hivi zimebakia point ngapi jamaa walirudishe kombe lao Msimbazi?

    ReplyDelete
  3. Wewe Kisiju pwani hata ivyo ushukuru kupata hako kapicha ka timu yako kwani hata Ankal mwenyewe mpirani hakuenda hizo habari ni kwa msaada tu wa Bwana Bukuku(full shangwe). bila ya hiyo sijui ingekuwaje.
    Mdau
    Holland

    ReplyDelete
  4. Mnyama anafurahisha sana, jamaa walikaza sana na kucheza kwa ubabe toka mwanzo baada ya kuahidiwa kitita kikubwa cha fedha na wapinzani, baada ya goli la pili wakaanza kulia lakini walisahau waswahili wanasema "nia haizidi uwezo"

    ReplyDelete
  5. Hongera Simba SC. Sio ajabu kufanya vema ktk mashindano ya kimataifa, upinzani wa ndani mnaopata ni mkubwa mno kiasi kila mbinu za kutafuta goli zinatumika. Msaada kama kuna mdau anafahamu website ya TFF ili tupate habari mbalimbali hasa kuhusu Timu ya Taifa, Makocha, wachezaji, nk.
    Mdau, Dar.

    ReplyDelete
  6. hongera mnyama naona heshima imerudi kwa kishindo.respect

    ReplyDelete
  7. wadau mimi nina swali. hivi hawa IPPMEDIA wana ugomvi gani na Simba?!! maana kama mtakua mmegundua huwa hawatoi matokeo ya mechi za Simba unless wawe wamefungwa!! sio ITV wala Radio One! na jana asubuhi kwenye habari za magazeti kwa aibu kabisa wanasoma vichwa vya habari vingine lkn habari kubwa kabisa ya ushindi wa Simba hawaisomi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...