Habari za leo Mdau,
NAOMBA NIWEKEE KWA WADAU
Nimatarajio yangu wote ni wazima na mnaendelea vizuri na kazi. Kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa nimejaribu kufuatilia adha kubwa tunayoipata sisi Wakazi wa Temboni, Kwa Msuguri, Mbezi, Kibamba na kuendelea along Morogoro Road.
Kero hii kubwa hasa nyakati za asubuhi (saa 11 alfajiri na saa 2 asubuhi) na jioni (kuanzia saa 10 hadi saa 3 usiku) huwa inasababishwa na TUTA (BUMP) lililowekwa na TANRORADS eneo la Kimara Stop-Over.
Yes, I agree with Kinondoni Municipal Council na wadau wengine idea ya kuwa na hili tuta ni kupunguza mwendo kasi wa Mabasi, Malori, Daladala,Taxi Drivers n.k. Lakini ukifuatilia kwa karibu zaidi utaona hakuna tija yoyote inayopatikana na uwepo wa hili tuta pasi na kusabibisha unnecessary traffic congestion.
Wadau hii kero inaongezeka day by day na ni hakika siku moja it will reach its climax na kusababisha usumbufu mkubwa kwa Wananchi. Nafikiri ni vyema sasa Wadau tukajipanga na kwenda kumwona Manager wa TANROADS - DSM na kukaa naye meza moja ilikuweza kutatua kero hii kubwa.
I know kila mtu anayetumia barabara hii anaguswa na kero hii na huwa tunazungumza zungumza tu mitaani bila ya kufuatilia kwenye ngazi husika. Nafikiri ni sasa ni muda muafaka tukahamasishana na kwenda TANROADS ili kuweza kupata ufumbuzi. Ndugu mdau, the above is my opinion naomba opinion yako ili tuweze kujua way forward.
Regards, Mdau Albert

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Na mimi nakuunga mkono kwa 100% maana pamekuwa ni shida kubwa sana. haiwezekani mtu unatoka Ubungo kwa dk 20 hadi Kimara Mwisho alafu pale mpaka Stop Over unatumia dakika 30 wakati ni kama 2km tu. Pana tatizo kubwa na serikali inaona lakini hailifanyii kazi. Hawaoni ni kiasi gani cha hasara tunapata kuanzia gharama za mafuta kwa magari yanayopitia ile njia kwa nyakati za asubuhi wakati wa kwenda kazini na jioni pia. Pia hawaoni ni muda gani ambao unapotea kwa kukaa kwenye foleni, ni masaa mangapi ya kufanya kazi tunayapoteza.
    Mimi nipo tayari kushiriakana na wadau ili tuweze kwenda kumuona Manager wa mkoa wa Tanroads ili kama ikiwezekana waangalie jinsi ya kuling'oa na kutafuta njia ingine.

    ReplyDelete
  2. Kabla hujatoa malalamiko haya jiulize kwanza je, ajali pale kimara stop over zimepungua kutokana na tuta hilo au zimeongezeka? Kama jibu ni "zimepungua" basi tuta hilo ni heri liwepo na ninyi mjitahidi kuamka mapema na kuwahi kazini.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Mon Feb 22, 03:17:00 PM tatizo ni kwamba TANROADS hawajawekw tuta pale bali wameweka kibaraza, yaani haitofautiani na kitanda na hapo walipunguza kidogo. Mbona kuanzia Ubungo hadi Kimara Stop Over kuna matuta manne na mbavu 12(matuta madogomadogo yanayokaa matatu matatu)
    na watu hawajayapigia kelele. Lile sio tuta ni kitanda kile

    ReplyDelete
  4. sio kuweka bump pale wangejenga kivuko cha juu kwa wavukaji!!!!

    ReplyDelete
  5. Mdau Albert uliyetuma hii msg nafikiri haijakukuta na haujawahi poteza mpendwa wako pale stop over. Mimi nimeishi stop over muda wa miaka kama mitano, ndugu zangu wa karibu na rafiki wakaribu kama 9 wameuwawa hapo sto over . Nafurahi saana kama kwa sasa wameweka tuta maanamadreva walikuwa wapumbavu saana hata hawatoi muda wa wapita miguu kuvuka.Yaani nimeshuhudia siku moja watu watatu kwa muda tofauti wamegongwa na kufa hapo hapo. Na hamu sana kurudi Bongo nikaota hilo tuta na ninapongeza saana watu wa Tanroads.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Mon Feb 22, 03:17:00 PM umeoji kama ajali zimepungua au zipo na umetoa jibu la kama zimepungua. na je kama zipo bado unashauri nini?
    pia ajali sio kati ya gari na waenda kwa miguu ata gari inapogonga lingine kwa nyuma inaposimama ghafla ni ajali.

    ReplyDelete
  7. Wenzetu walioendelea hawakupunguza ajali kwa kuweka matuta!!! Katika karne hii ambapo watu wanajitahidi kwenda kasi na kukimbia, sisi ndio tunawazuwia na kuwarudisha nyuma kwa kuweka 'vibaraza' barabarani.
    Tazama barabara hiyo kutoka Ubungo hadi Kimara, vibanda vya wanaosubiria mabasi kwa kujikinga na jua na mvua vimebaki vingapi,jiulize vinakwenda wapi? Angalia hii ya Jangwani kutoka Faya hadi Ubungo nako viko vingapi, vimekwenda wapi,jiulize pia taa za barabarani ziko ngani na zingine zimekwenda wapi? Je suluhu ni kuweka matuta!!!
    Leo nimesikia Dr.Shukuru Kawambwa anakubali kwa Serikali imechemsha mkataba wa TRL!!!! Huyo ni Dr.lakini sijui anatumiaje elimu yake kuondokana na 'kadhia' ya TRL.
    INATIA UCHUNGU SANA.
    Mtanzania,
    tmajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
  8. Nafkiri kwa kuongeza matuta barabarani ni kuongeza umaskini wetu, hebu jamani fikirieni, unapoteza masaa matatu katika umbali wa kilomita 18 tu je tutafika kweli, yaani masaa sita kama ni kwenda na kurudi. wenzetu wanaoendesha magari makubwa kwao ndio kero kabisa. mimi naona Yale matuta yote yaondolewe na kuwekwe vivuko vingine hata kama ni cha kama pale manzese ingawa nacho hakitumiki. itasaidia kupunguza kero yetu na hivyo vifo vya ndugu zetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...