Kikosi kamili cha timu ya Kijitonyama Stars a.k.a “wazee wa dozi” kipo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi ya TFF ngazi ya wilaya ya Kionondoni. Timu hii mbali ya kucheza soka la kitabuni pia linasifika kwa kutoa vipaji. Wazee wa dozi ambao hivi sasa wamejichimbia katika kambi yao Kigamboni, wanategemea kurusha karata yao ya kwanza siku ya Jumatano tarehe 24 February kwa kupambana na Friends Rangers katika uwanja uliopo shule ya Msingi Mwalimu Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hivi huyo mwenye jezi nyeusi ni refa au g'kipa?

    ReplyDelete
  2. Nasikia KIFA walitaka kuwadhulumu nafasi yao wakawapa Sifa Utd, bila vijana kupambana hadi DRFA kudai haki yao sijui ingekuwaje. Bongo soka hovyo kweli, kumbe KIFA wana timu zao wanazozibeba. Kazi kwelikweli!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Huyo ni kocha wewe, mwangalie vizuri, ha ha ha teh teh teh tih tih uuumwiiii.

    ReplyDelete
  4. Huyo ni refa, yote hiyo ni mizengwe ya KIFA kadi za timu walizipoteza ikabidi kabla ya mechi timu ipige picha na mwamuzi ili wakalinganishe na fomu za usajili, MKIAMBIWA BONGO SOKA MIYEYUSHO MNAKATAA, HII YOTE ILIKUWA FITINA TU ILA CHAMA LILIKOMAA HIVYO HIVYO!

    ReplyDelete
  5. Huyo wa tatu kushoto ni Godfrey Bonny?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...