Mkurugenzi wa Masoko Bw. David Minja akizindua rasmi udhamini wa TBL kwa Kili Taifa Cup 2010 huku Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe akishuhudia
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Tanzania Breweriers Limited (TBL) David Minja akiongea mbele ya wanahabari (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo ilipotangaza udhamini wa jumla ya milioni 850 kwa ajili ya mashindano ya Kili Taifa Cup yanayotarajiwa kuanza mei 8 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela (wapili kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja huku Meneja wa Bia ya Kilimnanjaro George Kavishe (kushoto) na Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijage (kulia) wakishuhuda baada ya kuzinduliwa kwa ligi ya taifa itakayoanza kufanyika Mei 8 Mwaka huu kwa kushirikisha timu za mpira wa miguu mikoa yote ya Tanzania.

KILI TAIFA CUP 2010 LAZINDULIWA RASMI


Mashindano ya Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup 2010) yamezinduliwa rasmi katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wafanyakazi wa TBL na waandishi wa habari wakishuhudia.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kilimanjaro Premium Lager, moja ya aina za bia za TBL kudhamini mashindano hayo yanayosaidia kung’amua na kukuza vipaji mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi timu ya taifa na kwenye klabu kubwa za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo ni mara ya nne kwa kampuni ya TBL kudhamini mashindano haya.“Tunajivunia kufadhili mashindano makubwa kama haya ambayo si tu yataleta shamrashamra miongoni mwa washabiki wa soka kote nchini, lakini pia yatasaidia kung’amua vipaji vipya na labda kuwaingiza baadhi ya wachezaji hao kwenye timu za taifa au kwenye klabu zinazoongoza,” anasema David Minja, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL.

Alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yanafanyika chini ya dhima: ‘Kufikisha Soka ya Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,’ yatajumuisha timu 24 zitakazocheza katika vituo sita, ambapo inatarajiwa kwamba mashindano hayo yataanza Mei 8, 2010 hadi Mei 15, 2010 katika vituo vyote hivyo, ambapo kila timu itacheza na mwenzake kwenye ngazi za mzunguko kisha zitakazopata pointi nyingi zaidi zitaingia kwenye hatua ya robo fainali.

Kwa mujibu wa Minja, robo fainali hizo zitachezwa Mei 22, 2010 na fainali zitakuwa Mei 30, 2010, na kwamba vituo hivyo sita ni pamoja na Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga.

“Ufadhili kwa mashindano yote ni Tsh milioni 850 na kila timu itapokea fedha za maandalizi, usafiri na malazi pamoja na seti za sare za michezo kwa ajili ya mashindano hayo,” alisema Mkurugenzi huyo wa TBL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema; “Tuna furaha kwa kuwa mashindano ya mwaka huu pia yatahusisha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 lakini watakaocheza ni wale waliozidi miaka 18.

Timu zote zimejiandaa kwa ajili ya mashindano haya, hivyo tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kuunga mkono timu zao.” Kwa muda mrefu TBL imekuwa ikijifungamanisha na Kabumbu na kwa hakika inafurahia hali ya uhuishwaji wa ufadhili katika Soka.

Tanzania Breweries Limited (TBL) huzalisha, kuuza na kusambaza bia safi, vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL ina maslahi ndani ya Tanzania Distilleries Limited, na kampuni zinazohusiana nayo, Mountainside Farms Limited.

Bia za TBL zenye umaarufu zaidi ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt na Castle Lager. Vinywaji vya aina nyingine vinavyohusiana na kundi la TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds na Premium Cold.

Kundi la TBL limeorodheshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na imeajiri karibu watu 1,300 na inawakilishwa kote nchini na viwanda vitatu vya bia, distillery, a maltings facility na depo nane za usambazaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. TFF kweli kunalipa..Mwakalebela alipoingia TFF alikua hazidi kilo 70, sasa mmmhh hata mkanda haukai.

    ReplyDelete
  2. A free healthy and safety piece of advice. One of the guys from the left and one from the right ought to have swapped positions for the stage to be kept in balance...

    ReplyDelete
  3. JAMANI HEBU ANGALIA AFYA ZA HAO JAMAA WA TFF UKILINGANISHA NA ZA WADHAMINI WAO UNADHANI KUTAKUA HATA NA SHILINGI KWENYE ACCOUNT YA TFF? MASHINDANO YAKIFIKA KAPU!!!!!!

    ReplyDelete
  4. UNENE SIYO SIFA; NDIO MAANA WAZEE NI HADIMU SANA KUONEKANA BARABARANI; KWA HALI HII MWAKALEBELA?????
    MMMHMMM???

    ReplyDelete
  5. Hivi ni yeye kweli? Akipata ubunge itabidi awe kwenye wheel chair full time.

    ReplyDelete
  6. HUYU MWAKALEBELA NADHANI AMEAMUA KUFANANA NA YULE MWAKILISHI WA FIFA AFRIKA. TULISHAWAHI KUCHAMBUA HAPA KWENYE BLOG WAKATI FULANI ALIPOENDA ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  7. TFF WANA GM PALE KARUME, KWANI NINI JAMAA ASITUMIE KUWEKA MWILI SAWA. GM YA BURE KABISA KWAKE.

    ReplyDelete
  8. we michuzi huna adabu umebana meseji yangu kwani una undugu na huyu mwakalebela? si lazima aambiwe ukweli unataka afe kwa bp ndio tuanze ningejua bla blaa... hakuna kuremba hapa we mwakalebela tumbo karibia lifike mbagala fanya mazoezi!

    ReplyDelete
  9. hawa TFF KAZI YAO kuchapisha vitabu feki,Yanga kwa muda mrefu wamelalamikia kitu hiki.


    Mali walizonazo vingozi wa TFF ni kufuru huyu mwakalebela alikuwa mshika mkoba wa jamal bayser wa Timu ya Mtibwa. na anamwaga pesa za kugombea ubunge Iringa sijui ndio katika wizi huu wa TFF.?

    ReplyDelete
  10. michuzi nakuheshim sana kaka yangu. achia comment yangu.
    huyu jamaaa hilo si tumbo la kiongozi wa soka ktk nchi ambayo haina muelekeo wa michezo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...