Spika wa Bunge. Mhe. Samuel sitta akitoa shukrani zake kwa Balozi Cisco Mtiro (kulia) kwa mapokezi mazuri kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wakati wa chakula cha usiku jana, katika Hotel ya Conrad mjini Bangkok. Balozi Cisco licha ya kuwa Ubalozi wake upo Kuala Lumpar Malaysia, pia anashughulikia nchi ya Thailand ambapo kwa kipindi hiki cha mkutano wa 122 wa IPU naye yupo Bangkok kuratibu ugeni wa Tanzania katika nchi hii.
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta na Balozi Sisco Mtiri wakibadilishana vitabu vilivyo tiwa sahihi za wajumbe waliohudhuria Mkutano wa 122 wa IPU toka Tanzania na wageni waalikwa kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo.

. Mhe. Balozi Sisco akifurahia kitabu chake chenye saini za wajumbe wa IPU toka Tanzania.
Spika wa Bunge.
Mhe. Dr. Christene Ishengoma naye akitoa Salam za Pongezi kwa mapokezi mazuri kwa balozi Cisco (mwisho kulia) kwa kipindi chote ambacho wamekua nae hapa Bangkok, Thailand kuhudhuria mkutano wa 122 wa IPU. Katikati ni Mhe. Prof. Idris Mtulia (Mb)

Mhe. Balozi Sisco Mtiro akitoka nje ya Hotel ya Conrad, Mjini Bangkok Thailand, mara baada ya chakula cha usiku na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano wa 122 wa IPU katika hotel ya Conrad, kulia kwake ni Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumba akimsindikiza.

Juu na chini Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta, akifurahia zawadi ya Track suit zenye nembo na rangi ya CCM ambazo zimetengenezwa na Mtanzania anayefanya shughuli zake hapa Bangkok Thailand, Bwana Nicholaus Kipalanga (shoto) alipomtembelea katika Hotel ya Conrad usiku kuamkia leo. Bwana kapalanga ana kampuni yake inayojishughilisha na uuzaji madini iitwayo Asili Germs International Co. Ltd ambapo pamoja na madini anafanya biashara za kutengeneza nguo za sare kwa order Maalumu kama vile sare za makampuni, Tshirt na truck suit kwa ajili vyama na kampeni mbalimbali.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. nilishtushwa sana na kichwa cha habari hii, huyo balozi hapa malaysia huwa tunamsikia tu, yeye yupo kwaajili yakutafuta wawekezaji na sikuwaunganisha watz, hatujawahi kufanya kikao hata siku moja na sasa ni mwaka wa 3

    ReplyDelete
  2. Fedha za walala hoi hizooo..zinatumika kupongezeana badala ya kuwekwa mahospitalini kununua dawa.

    ReplyDelete
  3. nimeishi ughaibuni zaidi ya miaka 10 na nimekwenda ubalozini mara moja tu kurenew passport yangu. sijui kwanini watu wanaona ni lazima mabalozi wawatafute na kuwakutanisha watanzania wanaoishi ughaibuni. kama nina shida ya kuonana na watanzania wenzangu, basi tunatafutana wenyewe hukuhuku mitaani.

    kitu kingine sijawahi acha shughuli zangu hata siku moja kwenda kuhudhuria mkutano na raisi au kiongozi yeyote wa serikali huku ughaibuni. kwa kweli sioni kabisa umuhimu wa kuonana na watu hawa. hawana jipya.

    ReplyDelete
  4. kaka michuzi jamaa hapo juu anasema ukweli ni kwamba hapa malaysia ni kama hakuna ubalozi tu watz maana hawana msaada wowote kwa watanzania wanaooishi hapa malaysia esp wanafunzi, kuna wanafunzi kibao tu hapa wapo stranded mitaani, mi nikiwa mmoja wapo lakini nimeenda kuomba msaada wa kunisaidia kurudi nyumbani jamaa wananiambia hawana fungu hilo sasa sijui ni wap ambapo ninaweza kupa msaada huo kama ubalozi wangu umeshindwa kunisaidia wadau naombeni mchango wa mawazo coz ma situation is hard nut to crak,malaysia ni ngumu u keepon spending frm jan to dec which is a dissapointment to many of us we thought mayb theres ana opportunity 2work while studing ryt here bt the whole thing is just a mase ryt here!wadau help me out am real stranded and i wanna get out here asap.

    ReplyDelete
  5. sijaona comment ankal! umeibana

    ReplyDelete
  6. Jamani jamani!watu mnashindwa kuelewa wanatoa lawama za bure!wewe umeenda mwenyewe then unataka ubalozi ukurudishe?how?yaani serikali itenge fedha za kuwarudisha watu nyumbani?soma majukumu ya ubalozi;ni kweli hakuna fungu hilo kwa ubalozi kuwarudisha..ama unataka watoe pesa mfukoni mwao?sometimes u have to think jamani sio kutoa lawama tuu, nenda kaji declare kama mkimbizi ama illigal migrant wakurudishe wenyewe

    Kingine tena i have been in malaysia August,2008.na kujionea mwenyewe kwa macho yangu jinsi balozi anavyo entertain wanafunzi huko, kiasi cha kwamba walifanya kama sebule yao. offcoz baloz na maafisa wake wapo very kind and social! problem wanafunzi waendao huko ni wengi ni wale wa starehe tuu, they had no option tz.

    Kuna wakati kulikuwa na case mwanafunz kaiba wine wisky supermarket. sasa hapo pia unataka ubalozi ukamtetee?how?

    ReplyDelete
  7. Bangkok hakuna ubalozi wa Tanzania! Ofisi zenyewe wanashea na wachina, aibu!

    ReplyDelete
  8. HUYU JAMAA WA TRACK SUIT ZA CCM ANAJUA HUU NI MWAKA WA UCHAGUZI HIVYO CCM WATAZIHITAJI SANA TRACK SUITS. ANATANGAZA BIASHARA HAPO

    ReplyDelete
  9. wachangiaji wa Libeneke mdau 11:01 na mdau 08:24

    Hatujayaelewa haswa malalamiko yenu,tunavyofahmu sisi tunaoishi huku Scandinavien,watanzania wenyewe ndiyo wanajiunganisha kwa kupitia vyama mbali mbali vya umoja wa watanzania,vyama vyetu vinasaidia wanafunzi wa hapa kama kumetokea matatizo kama hayo ya kurudi nyumbani au maziko ya kila mtanzania kama tumepotelewa na mmoja kati yetu,vyama vinasaidia watoto wasiojiweza huko Tanzania kutoka katika mfuko wa wanachama siyo kuomba misaada ubalozini ambao hautoweza kuchukuwa majukumu ya kila mtanzania anayekwama na majaribio ya maisha ya kujileta mwenyewe.

    Ubalozi wetu ambao makao makuu yake yapo mji wa Stockholm-Sweden upo wazi kwa makaribisho ya kila mtanzania wakati wote bila ya kujali tofauti zilizokuwepo za tabia,dini,ukabila au madhehebu mbali mbali kati yetu.

    Vyama vyote vya watanzania ninajihusisha kwa makaribisho ya ubalozi katika shughuri mbali mbali za watanzania.

    Muhimu kwanza mjiunganishe na kujitegemea wenyewe kupitia vyama vyenu,kama hamjabahatika kuunda vyama vya watanzania,inahitajika kuvianzisha kwanza kama watanzania.

    Mickey Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  10. Ni kweli ubalozi na maofisa wake wako so kind watu wanapafanya nyumbani kwa balozi kama kwao sasa we unayelalamika unataka balozi aje akutafute huko mitaani?
    Watanzania mnapenda sana kubebwa nyie!! uliendaje huko unataka ubalozi ukurudishe.??
    Jitahidini kwenye ukweli pasemwe acheni manung'uniko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...