Udzungwa Mountains National park sio hifadhi maarufu kwa wengi kama zilivyo Serengeti, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na nyinginezo. Kikubwa kinachofanya wengi tusiifahamu yawezekana kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa wanyama wengi ambao ndio huwa kivutio kikubwa kwa wazalendo wengi. Ukweli unabaki kuwa Udzungwa Mountain National park ni hifadhi ya kipekee ambayo ni mahususi kwa wale wanopenda kwenda kuona miti, Viumbe hai wadogo na wa kati ambao hustawi ktk misitu ya ki-tropiki. Hii hifadhi ipo mkoani Morogoro. Kufika huku unapita bwawa la Kidatu.
Mambo haya na mengine mengi kuhusu utalii na hifadhi zetu nenda:
http://tembeatz.blogspot.com/
http://tembeatz.blogspot.com/
Naomba kusahihisha: Udzungwa Mountains National Park ipo mkoa wa Iringa na si Morogoro lakini access yake nzuri na inayojulikana sana ipo Morogoro kama mdau alivyoelekeza hapo.
ReplyDeleteMilima ya Udzungwa ina viumbehai aina nyingi ambavyo havipatikani katika maeneo mengine duniani.
ReplyDeleteMfano kuna aina ya ndege (Partridge), aina ya kima (Kipunji) na vyura wanaozaa wa Kihansi.
Watanzania tuuthamini na kutambua urithi wetu. Tusisubiri mpaka wazungu waje kutembelea watwambie vitu hivyo. Tujitahidi tutembelee maeneo hayo.