Wapo madereva watiifu na wafuata alama za barabarani hawa wanastahiili sifa. Kawia ufike. Lakini watu hawa hawapo salama mara zote kwai wanaweza kusababishiwa ajali na madereva 'waruwaru' kutokana na uzembe wao. Aghalabu, si wote wasababishao ajali ni wazembe kwani kwa habati mbaya dereva aweza kusababisha ajali kutokana na tatizo la ghafla la kiafya au kughafilika kusikozuilika.

Kwa namna yoyote ile, madereva wa vyombo vyovyote vinavyotumia barabara pamoja na waenda kwa miguu yawapasa kuwa makini wawapo barabarani. Kwa walio waamini, tujikumbushe kujikabishi kwa Mungu na kuomba ulinzi wake ili atulinde na kutuepusha na ajali, lau ni mapenzi yake, basi na tuufikie mwisho uliomwema na azipokee roho zetu. Pole kwenu nyote mliowahi kukumbwa na ajali.

Subi www.wavuti .com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    Ni kweli kabisa. Tunaendesha magari kila siku na tuko kama tumejikabidhi kwa lolote. Tunalazimika sana kuomba Mungu atupatie ulinzi wa hali ya juu ili kila kukichwa turudi majumbani mwetu tukiwa wazima. Ni kwa neema tu tunapona na maajali au kutoka wazima.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2010

    Ndomana ikaitwa AJALI mengine bahati mbaya.... Ila wengine namna wanavyokatisha duh hatari Mungu atuepushe na kuzidi kutulinda... Seif.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    HII NDIO STYLE YA UENDESHAJI MAGARI SAUDI ARABIA. NI PURE 100% AMBAE AMEWAHI KUISHI SAUDI ARABIA ATAKUBALIANA NAMI. NI KAMA VILE HAWAJALI THAMANI YA MAISHA NA MALI. NITAKUTUMIA CLIP ZAO UONE

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2010

    yahee mi naitwa makame, nafanya kazi posta mpya, naishi kunduchi, kwa hiyo mizinga nshakuwa na aleji na magari, leo ntatembea kwa mguu toka kazini mpaka nyumbani kwa njia za vichochoroni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...