Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya BAKWATA , Dar es Salaam, leo kuhusu suala la Kadhi Mkuu. Kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum.
Mufti amefafanua kauli ya serikali iliyotoa bungeni kwamba haina tatizo na suala la Kadhi Mku na kwamba swala hilo limerejeshwa kwa Waisilamu na litashughulikiwa kidini.
Sheikh Mkuu pia amewatoa wasiwasi waumini wa Kiislamu kwamba si kweli serikali imekataa swala hilo na kufafanua kwamba kuna kamati ya wataalamu imeundwa kuangalia namna ya kuwezesha kuwepo kwa Kadhi Mkuu bila kuathiri kisheria na kanuni za nchi pamoja na umma kwa jumla.
Mufti ameataka waislamu kufanya subira wakati majadiliano kati ya wanasheria wa Kiislamu na waserikali wakiendelea na majadiliano juu ya suala hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2010

    I hate these kind of issues that tend to be pushed into everybody's throat. I would wish to see contiguous issues such as poverty, education, and health are viewed as crucial and inescapable. Instead, the government, segments of religious institutions, and some ill-wishers are rolling the ball on insignificant issues such as this of Kadhi. How are Tanzanians going to wake-up one day and find themselves poverty free just by instituting a Kadhi court? I am indeed flabbergasted and puzzled by this. please help.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    Nzuri kwa Sana Kaka Michuzi kwa kutupasha habari hiyo but naomba turekebishe kidogo hilo jina la Sheikh wa Mkoa si Alhaj Bali ni Alhad Mussa Salum Naqashabandy
    Abuu-faiza

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    nakuunga mkono comentor wa kwanza,
    watanzania tuna haja ya kutambua matatizo yanayotukabili na kujua yapi yapewe kipaumbele na yapi yanaweza kufanya taratibu, we need to priorotise how to alocate our scarce resources, watanzania tunajualikana kama ni watu tuofuata dini zetu vizuri tu, sielewi kuwa na kadhi ndio kutafanya tumjue mungu zaidi ama.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    Ww Anony wa 30 June 12:47:00 hivi umesoma vizuri Michuzi alivyomtambulisha huyo Sheikh wa mkoa, ama umekurupuka 2 kumrekebisha pasipostahili?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    the country goverment is religous free.i hope haita leta conflict in our peaceful country.selikali isiruhusu kutawaliwa na dini yoyote katika maamuzi yake.i don't know how this kind of courts work but mmh!my eyes open and my ears ready to hear.
    We have to pray for peace in this country.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2010

    wewe anony wa kwanza unaakili sana.
    haya mambo ya kujadili kadhi badala ya kazi ni upumbavu mtupu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2010

    Wewe anon wa kwanza punguza chuki,kama jambo la kadhi ni muhimu kwa walio waislamu wewe kinakuwasha nini?
    Wengi wenu mkisikia kinachowahusu waislamu chuki zenu zinajitokeza halafu mnajifanya watanzania watu wa amani hamna amani yoyote zaidi ya chuki za dini ya kiislamu.
    Wewe binafsi umefanya nini katika jamii yako kupigana na umasikini au elimu?

    ReplyDelete
  8. NALEZOWAGAKABISAJune 30, 2010

    Ukisikiliza nyimbo yako, imejaa chuki binafsi na ni kweli ukiimba nyimbo ambayo unataka kuua basi lazima vyombo vya sheria vikuchukulie hatua, umeimba bila insha, hakuna message ya maana hapo.
    Inaonyesha jinsi bado ulivyo check bob, na jinsi unavyoitaji elimu tena sana.
    Huwezi kunidanganya eti wewe unaweza kuwaongoza watu na kuwaletea maendeleo jimboni kwao.
    Kwanza hata sijui kama una mji zaidi ya kumtegemea kaka ambaye amechacha kwa kutokua na kadi za kuchanja na za wizi, na kama angeendelea kufanya kazi apo royal mail na kuendelea kukwiba angekua jela sasa. Kila kukicha kaka yako anasaidiwa na mke wake kwa vi benefit anavyopata Uingereza, ukumbuke ni wewe Mr II uliotokea kwenye TV eti kuonyesha crib yako (ambayo ilikua ni ya kaka na vitu vyote), na wajanja wakaja wakakomba, halafu leo hii eti unataka kuwawakilisha wananchi bungeni! Utaongea nini? Zaidi ya kutaka kupata hivyo vihela vya ubunge na kufanya matanuzi na kutukana watu!
    Kama kweli wewe hupendi wizi na unyanyasaji basi ungeanza nyumbani, kwa kukataa kutumia mahela ya wizi ya kaka na kuukana ufuska wake, hapo kweli tungekuona wa maana.
    Huwezi kujilinganisha na wanasiasa maarufu ambao hawakusoma, zaidi ya kuwadhalilisha maana wao hawakufanya haya mambo yako, wao waliwakilisha wananchi, walituletea uhuru, walituongoza mpaka hivi sasa. Wewe utaweza?
    INAONYESHA JINSI CHADEMA WALIVYOWABABISHAJI KISIASA, NA NDIO MAANA CCM WATAENDELEA KUWA MADARAKANI TENA KWA SANA KWA MFUMO HUU WA KISANII WA VYAMA VYA UPINZANI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...