Mh. Henry Shekifu
Mpiganaji Jamila Omar

MKUU WA MKOA WA MANYARA MH. HENRY DAFFA SHEKIFU MUDA MFUPI ULIOPITA AMETANGAZA RASMI NIA YAKE YA KUWANIA UBUNGE KATIKA JIMBO LA LUSHOTO MKOANI TANGA WAKATI ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKAM HOTELI YA KITALII YA NAURA SPRING ILIYOKO MJINI ARUSHA.

SHEKIFA ANAPAMBANA KUMWONDOA MBUNGE WA SASA BALOZI ABDI MSHANGAMA AMBAYE PIA WALIPAMBANA NAY KATIKA UCHAGUZI ULIOPITA WA MWAKA 2005. AIDHA MH. SHEKIFU PIA ALIKUWA MBUNGE WA LUSHOTO KWA MIAKA KUMI KUANZIA MWAKA 1995 HADI 2005 HADI PALE ALIPOSHINDWA NA BALOZI MSHANGAMA.

KATIKA TUKIO LINGINE PIA MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI WA KITUO CHA LUNINGA CHA CHANNEL TEN MKOANI ARUSHA JAMILA OMAR PIA AMETANGAZA NIA YA KUWANIA UBUNGE WA VITI MAALUMU KWA CCM KATIKA MKOA WA ARUSHA.

JAMILA OMAR MBALI YA KITAALUMA KUWA MWANDISHI WA HABARI LAKINI PIA NI MTAALAMU WA MIFUGO NA KABLA YA KUINGIA CHANNEL TEN ALIFANYAKAZI NA RADIO UHURU. PICHA NA HABARI NA NOVATUS MAKUNGA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2010

    Serikali haina budi kutunga sheria ya kupunguza kima cha mishahara kwa wabunge wetu!

    Wengi wanakimbilia maslahi binafsi ya kuwa mamilionea baada ya mika mitano.

    Sasa wewe ukiwa Mkuu wa Mkoa...wabunge sijui wangapi chini yako...unalilia ubunge wa nini?

    Serikali haina budi kuepusha madhara ya (hata) kupoteza maisha kwa wagombea ubunge ana magenge yao!

    Mtanzania Futurologist

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2010

    Kuna jambo mimi silielewi!! Kuna ulazima gani mtu ambaye una madaraka ya ukuu wa mkoa na bado una kiu ya ubunge? Kama lengo ni kuwatumikia wananchi (ambavyo sasa ndio imekuwa kauli mbiu) je ukiwa mkuu wa mkoa unatumikia akina nani? Na pia tuna tatizo moja la kugawa vyeo kama njugu ndio sababu ya kufanya wenye tamaa kuzunguka zunguka kama fisi; mfano sioni sababu yoyote ya mtu aliyetumika kwenye ubunge na awamu zilizofuata akaangushwa kupewa ukuu wa mkoa na tena mtu huyo mate kumtoka arudi kwenye ubunge. Mimi nafikiri tuna kila sababu ya kuiangalia katiba yetu na kwa mawazo yangu kuna vitu tuvibadilishe kama si kuviondosha kabisa kama twahitaji maendeleo!! Mfano mkuu wa mkoa kama huyu sasa unadhani atatekeleza majukumu yake kiufanisi wakati kichwani anawaza akagawe takrima jimboni ili achaguliwe? Ni mawazo yangu tu, thus yakikugusa usiyatoe!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    hongera dada jamilah nakutakia mafanikio mema,nakuamini katika hilo kwani unayaweza,je utaweza kukabiliana na rushwa katika kura za maoni hapo sasa haya ngoja tusubiri

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    huyo shekifu ni kipi alichokisahau? si alikuwa mbunge kwa miaka kumi! sasa anataka nini? nchi hii!! aliyeturoga alishajifia zamani sana!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    Tanzania haina wenyewe au ndo kama anony hapo juu alivyosema kuwa aliyetuloga keshakufa.. yani nchi yetu badala ya kukimbizana na nchi nyingine kimaendeleo,watu wanafikiria kujilimbikizia mali tu. sasa Mkuu wa mkoa anataka ubunge ili iweje? kwanza kama alishakuwa mbunge kwa miaka 10 na hakubadilisha chochote anafikiri atabadilisha nini akipewa sasa? na huo u-kuu wa mkoa ni tosha sana kuleta maendeleo katika mkoa husika wakati ubunge ni katika jimbo moja?? haiingii akili kutaka kugombea ubunge ilhali tayari ni mkuu wa mkoa??? Tanzania inatakiwa kubadilisha katiba haraka sana ili watu wasiwe na hizi njaa za kuwa na vyeo viwili au zaidi wakati ufanisi ni zero.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2010

    Hivi mtu unaweka kuwa mbunge on and on and ond???

    I like bloggers here so much....ati " wenye tamaa kuzunguka zunguka kama fisi"


    YOu made my day....Nimecheka sina mbavu...

    Tanzania nchi yetu kama mchezo wa radio wnaoact hawaoni nikichekesho lakin tunaosikiliza especilly sisi tulio mbali tunaona kama kichekesho vile...


    Kweli mkuu wa mkoa uache watu wako ukimbilie kuwa mbunge kwanza jimbo lingine mbali kabisa na unapoishi....Utumishi wa umma unao tayari.Kwanza kwa kuwa appointed bila kuchaguliwa na watu. Ungekaa chini usemue MUngu asante. Kama ulikua una hamu ya kuwa public servant umefata kwa free ride.......

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2010

    Hongera sana mbunge wetu Mtarajiwa Mheshimiwa Henry D.Shekifu.Tumekumiss sana kwa hii miaka mitano iliyopita.
    Nakuomba usife moyo na wala usikate tamaa kutokana na maneno ya watu.Sisi wazaliwa na wakazi wa Lushoto ndio tumekuomba kwa moyo mmoja uje ugombee tena katika jimbo letu.Maskini watu hawajui kwamba wazee wa Lushoto kwa busara zao ndio waliokufuata na kukuomba ugombee.

    Mungu yupo pamoja nawe na tunakusubiri kwa hamu wananchi wako wa Lushoto tunatambua na kuthamini mchango wako kwa maendeleo ya jimbo la Lushoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...