Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dr. Rajni Kanabar (wa pili kutoka kulia) akitoa utambulisho kwa waandishi wa habari juu ya ujio wa madaktari bingwa kutoka India ambao watashirikiana na madaktari wa hospitali hiyo kutoa huduma za magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya mifupa na viungo, moyo, figo na magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo leo jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Dr. Rajesh Pandit mtaalam wa magonjwa ya moyo, Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dr. Rajni Kanabar, Kaushal Mishra Daktari Bingwa wa tiba za Mifupa, Dr. Avinash Ignitius mtaalam wa magonjwa ya figo na Dr. Aman Gupta ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa haja ndogo.
Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dr. Rajni Kanabar (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya uimarishaji na utoaji wa huduma za magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya mifupa na viungo, moyo, figo na magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo kwa kushirikiana na mataktari bingwa kutoka nchini India leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni meneja wa mifumo ya komyuta ya hospitali hiyo Jingne Oza.

kwa habari kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hakuna wamatumbi? hiyo hospitali ni Delhi au Dar? anyway, madaktari wa kimatumbi longolongo sana, hawachelewi kuomba kitu kidogo....

    ReplyDelete
  2. sasa untaka matibabu au umatumbi? kama unataka hivyo nenda muhimbili ukafe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...