Baadhi ya wazee walioshinda michezo mbalimbali ikiwemo ya kuvuta kamba katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa ikiwani shamrashamra za siku ya wazee Duniani , Oktoba Mosi ya kila mwaka , wakizawadiwa zawadi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, ( wapili kutoka kulia) , leo baada ya kushinda kwao.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, Halima Dendego ( kulia) akitaniana bibi aliyeshinda mchezo wa kuvuta kamba kabla ya kupewa zawadi yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu) kutoka kulia, leo ikiwa ni maandalizi ya siku ya wazee Duniani Oktoba Mosi , mwaka huu , kitaifa inafanyika Mkoani hapa .
Bibi wa makamo akifanyiwa uchunguzi wa afya yake na Dk Baraka Nzobo kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ili kubaini kama anao ugonjwa wa kisukari ili awezekupewa ushauri na tiba katika Hospitali hiyo, upimaji huo ulianza kufanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, ikiwa ni maandalizi ya siku ya Wazee Duniani ya kila mwaka, Oktoba Mosi, kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro
Baadhi ya wazee wakike na wakiume wakifanyiwa uchunguzi wa macho kwenye uwanja wa Jamhuri wa mjini Morogoro ili kubaini matatizo yao kabla ya kupewa ushauri na tiba kutoka kwa wataalamu wa macho, kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ,leo ikiwa ni maandalizi ya siku ya Wazee Duniani , Oktoba Mosi, mwaka huu , ambapo kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro.Picha na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Leo ni siku ya watoto, mnaharibu kuchanganya mambo na kuadhimisha siku ya wazee!!

    ReplyDelete
  2. Mbona serikali imekuwa dhulumati kwa kutomaliza kuwalipa wazee wa Jumuiya?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...