Waziri wa Mambo ya Ndani,Lawrence Masha akimtunukia Cheo Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo uafisa wa Polisi. PC Happines Temu wakati wahitimu hao walipotunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo hayo kwenye Chuo cha maafisa wa polisi (Dar es salaam Police Academy) yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

NA MAGRETH KINABO NA MARY KWEKA- MAELEZO

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Lawrence Masha amelitaka jeshi la polisi lisivunje moyo kwa kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi bali wachukulie kama changamoto na kujidhatiti kukaimrisha mikakati ya kukabiliana na matukio hayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Masha wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo, iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es Salaam.

“Mnao wajibu wa wa kuwa mstari wa mbele katika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto hizi,” alisema Waziri Masha.

Alizitaja sababau za kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kuwa ni maendeleo ya Sayansi na teknolojia, ukosefu wa ajira, utandawazi, umasikini, ukuaji wa miji, ongezeko la makazi holela, kuzagaa kwa silaha, imani za kushirikiano,ongezeko la pengo baina ya matajiri na masikini pamoja na utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevyia.

Waziri Masha alisema kuongezeka kwa taarifa za uhalifu katika vituo vya polisi ni miongoni mwa mafanikio ya jitihada zinazofanywa na jeshi hilo, kuwahamasisha wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.

Hata hivyo Waziri Masha aliongeza kuwa makosa yanayowakera wananchi kama unyanga’nyi na uvunjaji wa majumba na wizi yamepungua.

Alisema takwimu zinonyesha kuwa mwaka 2008 makosa uvunjaji yalikuwa 27,491 na mwaka 2009 yalipungua hadi 26,561 hivyo kupungua kwa asilimia 3.4, wakati makosa ya wizi mwaka 2008 yalikuwa 31,130 na mwaka 2009 yalipungua hadi kufikia 28,427, hivyo yamepungua kwa asilimia 8.7.

Waziri Masha alilipongeza jeshi hilo, kwa kuendelea na mpango wa kuratibu na kusimamia mafunzo ya walinzi wa amani kimataifa ikiwa ni pamoja na kushiriki kwa vitendo shughuli za kulinda amani sehemu mbalimbali duniani.

“Serikali inaendelea kuvijengea mazingira mazuri vyombo vya ulinzi na usalamana kutatua matatizo ya makazi na maslahi ya watumishi wake.

Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) katika mwaka huu wa fedha inaendelea na wamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za askari kwa kujenga maghorofa 30 kambi ya polisi barabara ya Kiliwa, sita kambi ya Mabatini Mwanza, sita Musoma , Mara, Tatu Byekera ,Bukoba, 12 Ludewa Iringa, nane Kiwanja cha ndege Arusha, mbili Unguja Kuu Unguja na mbili Finya Kaskazini, Pemba.

Naye Mkuu wa chuo hicho, Elice Mapunda alisema kitaanza kutoa diploma ya sayansi ya polisi kuanzia mwaka 2010/2011 ikiwa ni jitihada za kukipandisha hadhi.

Alisema jumla ya wanafuzi walioripoti katika mafunzo hayo walikuwa 356 na wote wamefaulu, lakini wawili kati yao walishindwa kushiriki kikamilifu baada ya kuumia wakati chuoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sare hiyo kidogo inafanana na ile ya Polisi wa Uingereza!

    ReplyDelete
  2. uhalifu umeongezeka sana Tegeta yote hasa Tegeta Beach/Ununio... tafadhari Police jitahidini kukomesha uhalifu...wiki moja watu wamevamiwa sana na majambazi yenye silaha tena majambazi hayana aibu yana vamia maduka mapema sana saa mbili usiku tu.. huku wakirusha risasi hewani na kujerui raia wema..please please tunahitaji msaada wenu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...