Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dr. Willbrod Slaa akiwa na Bi. Josephine Mushumbusi (kushoto) mwanamke anaedaiwa kuwa ni mke wa Bw. Aminiel Mahimbo wakati akimtangaza kama mchumba wake katima moja ya mikutano yake ya kampeni.
Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa amedai kuwa hakufaham kuwa,mwanamke aliemtambulisha kuwa ni mchumba wake, Josephine Mushumbusi kuwa ni mke wa mtu na hata mwanamke huyo hakuwahi hakumwambia.
Aidha Dk. Slaa amedai kuwa taarifa hizo za kutuhumiwa kwake kuwa amemchukua mke wa Bw. Amaniel Mahimbo, amezisikia kwenye vyombo vya habari kwa mara ya kwanza kwani hakuwahi kuambiwa swala hilo hata siku moja.
Dr. Slaa ametoa madai hayo leo katika maelezo ya utetezi wake kwa tuhuma zinazomkabili za kupora mke wa mtu ambaye amemtambulisha mara kadhaa katika majukwaa ya siasa kuwa ni mchumba wake.
Aidha Dk. Slaa amekataa kumlipa fidia ya sh. bilioni moja Bw. Mahimbo aliyoiomba mahakama imtake Dk. Slaa amlipe kwa hasara aliyoipata kwa kuporwa mke na kudhalilika.
Utetezi huo umewasilishwa na wakili anayemtetea Dr. Slaa, Bw. Mabere Marando kuwa hakuwa akifaham kuwa Josephine ameolewa au aliwahi kuolewa na kwamba hata Josephine hakuwahi kumueleza kuwa yeye ni mke wa mtu.
Dk. Slaa ameitaka mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo kwani haina msingi wowote, kwasababu ni mdai mwenyewe aliejidhalilisha kwa kukubali kutumiwa na chama flani cha siasa (hakukitaja) ili kutoa habari hizo kwenye vyombo vya habari.
Pia amedai kuwa,kwa kuweza kutoa habari hizo kwenye vyombo vya habari mdai ameonyesha wazi kuwa hana maadili na mahakama hivyo imuamuru kulipa gharama za kesi hiyo.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa teka Oktoba 5, mwaka huu katika mahakama kuu.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa mwezi Septemba mahakamani hapo na Bw. Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.
Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.
Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo kumtangaza mkewe wa ndoa (Josephine) kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.
Mlalamikaji huyo, amedai kuwa Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara Baruti, Dar es Salaam.
Aidha amedai kuwa katika ndoa yake na Bi. Josephine wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.
Mahimbo alidai kuwa , ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake wa halali.
Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic, Mahimbo alidai hivi karibuni kuwa mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi.
Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha na mkewe huku akiambatanisha cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.

Hongera Mr Slaa, your the men you need that. Hiyo ni mother nature nani ambae hafanyi hivyo. Tunahitaji wasema kweli kama wewe, usimfiche wewe mweke mbele huyo Mama na sisi wakina mama tujitokeze zaidi mbele kupiga kura. Michuzi usibanie.
ReplyDeleteWe Mahimbo! Usilazimishe penzi kwa mwanamke asiyekupenda. Kama umeachwa umeachwa tu. Tafuta usawa mwingine badala ya kuganga njaa upewe fedha za bure. Wanawake wapo wengi. Unatudhalilisha wanaume wenzio huku, alaaaa....
ReplyDeleteNa kama upo kisiasa zaidi ukome kabisa...mambo ya familia/uhusiano na siasa hayachangamani mzee...
Kwani alikuja kumchukua nyumbani kwako???????? Ulevi wako na tabia zako chafu ndo zilimfanya Josephine hakukimbie. Sasa unaomba ulipwe hela yote hii kwa hasara gani uliyoipata? Mlevi mkubwa lala mbele likakuchweee huko huko. Hupatii hata centi moja ng'oooooooooooooo. Hicho chama kilichokutuma ulalamike mahakamani waambie wao wakupe hela lakini huzipati kupitia kwa mgongo wa Dr. Slaa Mzee wa Ikulu mtarajiwa. Dr.Slaa kaza mwendo. Alipomtambulisha ndo uliona kuwa umeporwa mke?????????? Ahaaaaaaaaaa lala mbele huko likakuchweee la machweo.
ReplyDeleteCHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE 2010. CCM ZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ
taarifa kama hizi ni lazima uzipambe
ReplyDeleteDk Slaa, acha usanii!
ReplyDeleteHuo ni uwongo kupitia mawakili; mawakili wengi ni waongo sana! Kazi yao ni kutaka kushinda kesi, hata kama wanatetea uwongo!
Yaani, mke aje kwako siku hizo zote na watoto. Uwakubali bila hata ya kumwuliza huyo mke hao watoto ni wa nani?
Come on Dr Slaa. Wewe si unajidai ni mwanasheria? Hujui ignorance of the law is no excuse. Umechemsha mzee. Eti hukujua? Ndiyo mnavyofanyaga hivyo? Kwa hiyo huyo mwanamke hukupewa na wazazi wake umejichukulia tu. Lo shame on you fisadi mkubwa we!!
ReplyDeleteCome on Dr Slaa. Wewe si unajidai ni mwanasheria? Hujui ignorance of the law is no excuse. Umechemsha mzee. Eti hukujua? Ndiyo mnavyofanyaga hivyo? Kwa hiyo huyo mwanamke hukupewa na wazazi wake umejichukulia tu. Lo shame on you fisadi mkubwa we!!
ReplyDeleteTANZANIA SIO KAMA USA AU EUROPE KWAMBA UKIOA AU KUOLEWA KUMBUKUMBU ZOTE ZINAPATIKANA KWENYE SYSTEM NDIO MAANA TUNATAKA KUIBADILI TZ KWA DR SLAA KUWA RAISI
ReplyDeleteBABU SEYA JE???????????????
ReplyDeletehiyo kesi mbona tunashinda chadema kwani kamanda wetu MABERE MARANDO ni kichwa namwania vibaya
ReplyDeletemimi nashangaa huyo bwana mahimbo sijui anabaki analilia mke namshauri aje kwenye dini yetu atapata wanawake wengine tena hata akitaka wanne(4) Tena warembo na atafurahia maisha ya hapa duniani ila kama katumwa na ccm basi hakuna jinsi ukweli ni kuwa ndoa siyo suala gumu kiasi hicho ila wagumu ni wanadamu wanahubiriwa kila siku ila hawataki
ReplyDeleteMTU AKISHAFIKISHA UMRI WA MIAKA 21 YUKO HURU KUFANYA MAAMUZI YAKE MWENYEWE BILA KUTEGEMEA WAZAZI. ITOKEAPO KUHUSISHWA WAZAZI NI SHAURI YA MILA NA DESTURI ZA KUWAENZI WAZEE WETU. HUYO MAMA YUKO HURU KUAMUA APENDAVYO NA WALA SLAA HANA LAWAMA YA KUTWISHWA VINGINEVYO NI KIINIMACHO CHA KISIASA KIPINDI CHA UCHAGUZI. HAKUNA FIDIA ATAKAYOPATA VINGINEVYO MHUSIKA ANGETOA TAARIFA POLISI YA KUPOTELEWA NA MKE WAKE, NA KAMA POLISI WANGEMKUTA YUPO NA SLAA TOKANA NA SHINIKIZO LA HUYO KUTAFUTA MKE WAKE HAPO NDO SHERIA INGEKUWA NA NGUVU.
ReplyDeleteJAMANI TUWE WAKOMAVU WA KUELEWA SHERIA SI USHABIKI WA KISIASA TU.
Na slaa ukikosa tu urais,huyo kakutoroka,maana huyo mwanamke ana tamaa anaju atakua first lady,jiandae na we kulia soonmaana urais hupati na yeye ataingia mitini n weyenazo.
ReplyDeleteMzee Slaa, that seems like a very lame defence. Wewe bingwa wa kulipua mabomu kama EPA utapeliwe na mwanamke aingie kwako hujui kam kaolewa- kakutapeli au kukua makini? Yaani ni fisadi au tapeli huyo mama unataka kutuambia? Kama hukua makni katika hili lililo karibu na wewe utakuwa makini kwenye yale yasiyo karibu na wewe au utatapeliwa kwenye mswala ya uongozi wa nchi? Tafuta utetezi wa maana mzee this is not respectful to the Tanzanian public.
ReplyDeleteAlafu CHADEMA inashindwa nini kuondoa UKASKAZINI kwenye hicho chama.Uko makini wewe lakini UKABILA na UKANDA ni dhambi kubwa ambayo ni sababu tosha ya kutokupigia kura.
MAHIMBO HUNA MKATABA WOWOTE WA KISHERIA NA DR. SLAA. SASA UNAMDAI NINI! MDAI MKEO ALIYEKUMWAGA WAKATI UNA MKATABA NAE WA NDOA.
ReplyDeleteDR. SLAA NA JOSEPHINE WANATAKIWA WAKUDAI WEWE GHARAMA ZA KULEA UNAODAI WATOTO WAKO.
HALAFU HII NI AIBU KWA MWANAUME RIJALI KUDAI ETI UMENYANG'ANYWA MKE!! HIVI WEWE NI MWANAUME KWELI!! NINA WASIWASI NA WEWE!! ETI MKE WAKO WA NDOA ANAFANYA BIASHARA SIKU ZOTE HIZO HUMWONI WE KIMNYAA. DUME ZIMA UMEKAA NDANI TUU HATA WWATOTO HUWAONI. WE KIMNYAA!! NAKWAMBIA HATA HAO WATOTO UNAODAI WAKO SIO WAKO.
KAMA KUNA CHAMA KINAKUSHAURI BASI IMEKULA KWAKO. WANAKUABISHA AFU BAADAE HUWAONI.
JOSEPHINE KUNA KITU KITAMU ANAPEWA NA DR SLAA WE ULISHINDWA KUMPA.
"DUME LA PAKA HALISHINDWI KUPANDA DARINI"
Umepolwa Mke na nani?majambazi?
ReplyDeletetazama hata maana ya kupolwa haujui?
Sasa muda wote huo ulikua wapi kumtafuta na kujitangaza kwenye vyombo vya habari?Mkeo atawezaje kusafiri kikazi usijue anakwenda wapi?
Umejizalilisha mwenyewe na Jamuuri unatakiwa ikushtaki kwa uzembe na uongo.
Kama unataka mradi ungeomba msaada upewe ,kwanamna hiyo basi hata mimi nitapiga dili na mkewangu akatembee na Ankoba afu baadae nitamdai Anko milioni 2.
We mdau wa hapo juu mbona unachanganya mambo? Hapo siyo issue ya ignorance of the law, hapo ni kuwa Dr. Slaa hakupewa complete information by the time wanaingia "contract" ya uchumba na Josephine, na ni Jsephine aliyepaswa kutoa complete disclosure ya status yake, sasa Dr. Slaa ni malaika mpaka aote? Kama ni kumdai amdai Josephine kwa kuvunja ndoa yao.
ReplyDeleteBinadamu wengine wanachekesha yaani mchumba unapewa na wazazi wa mwanamke hii ni kali jama. Au nipate bahati kama hiyo ya kupata mke na mtoto nianze kuuliza maswala ya baba yao. Kweli sasa nimeamini mambo bado kina mama kweli mna shida
ReplyDeleteHivi Watanzania tumekosa mwelekeo?? Personal issues mbona ndizo tunazishabikia?? Na kwa bahati mbaya tunajianika dunia nzima ituelewe upofu wetu ulivyo!!
ReplyDeleteTumesahau kuweka kipaumbele kwenye mambo ya msingi sehemu tunakotaka taifa letu liwe miaka 50 au 100 ijayo tunaangalia petty issues!! Kweli Mwalimu alisema, umaskini mkubwa zaidi ni umaskini wa mawazo au akili!!
Na kwa bahati mbaya hatuwezi kumpata Malaika kushuka kuja kuiongoza nchi hii!!
Pamoja na uvivu wetu wa kusoma na kuangalia habari za maana duniani na kubaki kulalamika tu, tunajua wenzetu walivyo kwenye kasi ya kuelekea kwenye level nyingine ya nchi zao. Kenya - middle Income Country, Rwanda hao usiseme. Tunalalamika EAC, lakini hatusemi tunataka nini kwenye EAC!!
Kwa bahati mbaya tumekataa midahalo, hivyo tumekosa nafasi ya kuhoji utekelezaji wa ahadi zinazotolewa na wagombea!! Sasa wahandishi (au waandisi) wa habari na wenyewe wamepotelea kwenye "semantics" badala ya kuzipembua sera za vyama!!
Cheap politiki!!
Swala hapa si CUF, CCM, wala Chadema: swala ni mustakabali wa taifa la Tanzania!! Personal Interest za watu wenye upeo mfupi na finyu, hakika utatupeleka pabaya. You can fool some people some time, but not all the people all the time, alijisemea mtu mmoja hapo kale (simfahamu huyo mtu – nilisikia kwa Bob Marley akiimba).
Kwa nini uchukue airtime kubishana kwamba Dar - MZA treni ni masaa matatu, au kumi, au 24?? Kama mnataka kuuliza kitu kama hicho, midahalo ndio ingekuwa fursa pekee ya kuchomekea kitu kama hicho, na kumuumbua anayehusika, kama yawezekana!!
Mwisho naomba nikumbushe, hapa simlaumu mtu yeyote ila nasisitiza kuwa kila M-Tized ajitume kwa taaluma yake: Mhadishi wa habari, mchumi, mhasibu, afisa wa serikali, mwanamichezo, mwanasiasa, hata viongozi wetu katika ngazi mbalimbali!! Bado tuna nafasi kubwa ya kwenda mbele kwa speed ya Konkodi!!
Let's grow up, not get aged!!
Vidumu vyama vyote!!
Hoyaa wewe mahimbo inawezekana jogoo halipandi mtungi ndiyo maana ukakimbiwa na mke, hata hao watoto sijui kama ni wako inawezekana jamaa walikuwa wanakusaidia kuzalisha ukiwa na mke wako.. DNA inatakiwa kufanya kazi yake kwa hao watoto tujui baba yao ni nani...
ReplyDeleteDr. Slaa anatudanganya. Haiwezekani kuwa alikuwa anam date huyo mwanamke na hajui kuwa ni mke wa mtu. Kama huyo mwanamke hakumuambia basi aachane nae kwani huyo mwanamke she is not honest with him.
ReplyDeleteMaan i really don't like CCM but i think CHADEMA ni worse more than CCM. Dr Slaa nimefuatulia kampeni zake and he is not offering any solutions to our long time problems. All he is preaching is EPA and kulipua mabomu style ambayo mwenzake Lyatonga alitumia na kushindwa kuwa convince wa-Tz back in 1995.
Eniwei, may be tusubiri 2015 tumpate Musa ataekuja kutukomboa na kutepeleka kwenye Promise Land.
Imani
We Mahimbo, yaani amekuwa mtamu baada ya Mwananchi mwingine kumchukua? Yawezekana mlikuwa hata TUNDI hamli, sasa una ganga njaa hapa. acha ushamba, kuna wanawake kibao wanataka kuolewa, kaowe sio kudandia gari lililokuacha. Duh watu wengine bwana. Umechacha!
ReplyDeleteMaendeleo yanaanza nyumbani...wewe unaweza kuleta maendeleo na nyumbani kwako ni harufu mbaya?? Kawaongoze wa mbulu sio watz..
ReplyDeleteMimi nakubaliana na wewe mia kwa mia tafanye hukujua ukajichukulia mke na kujiozesha mwenyewe sio? je ulipata uhakika na watoto ni wanani? wewe kama RAHISI mtarajiwa ulikubali kulea watoto ambao sio wako bila kuwasiliana na BABA yao? kutokana na UMRI uliokua nao ulikuwa bize kwa kujiaandaa kuiongoza NJI(nchi)mpaka ukapitiwa na kusahau KUOA,swali je ukishaingia IKULU utaweza vipi kutatua maswala ya MKE na MUME wakati huna uzoefu nayo?au utamwacha achukuliwe na wengine kamaulivyo jichukulia wewe? mzee mwezangu ulikuwa unachapa nje tuu bila kuoa nyie ndio mnaotuharibia watoto wetu mitaani na vijigari vyenu MITAANI.kiongozi wa UMMA ujisafishe kwanza kabla hujapanda JUKWAANI sio upanda jukwaani na MIZAMBI kibao hadi unaanguka chooni.UMRI huo unachumbia je utaoalini?
ReplyDeleteHUYO MAHIMBO MWENYEWE NASIKIA NI "KULA KULALA" alikuwa anamtegemea mkewe, mamaaa akachoka AKASEPAAAAAAAA
ReplyDeletePigeni kelele wee lakini ukweli unabaki pale pale kuwa DR SLAA KAFUMANIWA NA MKE WA MTU.
ReplyDeleteNa huyo Marando anayemtegema mhu! mie sisemi utetezi hauna uzito wowote, alitakiwa apeleke vielelezo mahakamani kuwa huyo mwanamke si mke wa mtu hajaolewa au aliolewa akaachika. Lakini alivyofanya ni kukubali kuwa yeye ametembea na mke wa mtu kwa kutokujua. Hivi mtu mzima na akili zake mwanamke sio mwari wala kigori utaache kumuuliza kama yuko single au kwenye relationship maana mwanamke mwenyewe umri umeenda hasa!
Haya wajameni tumesikia na lengo lako limetimia utapata kura za kuongeza ruzuku lakini hukua na nia ya kuwa rais, maana usingelichukua mke wa mtu kuogopa kashfa, ungelioa kabla ya kampeni, lakini kwa kuwa lengo lako sio kuwa rais ndio maana umeyafanya hayo!
JAMANI MGEKUWA NYINYI NDIO WACHUKULIWA MGEFURAHI...ACHENI UJINGA WA KUSHABIKIA VYAMA,HUYU JAMAA HAKUMUACHA MKEWE MKUMBUKE...
ReplyDeleteDr hapo umefanya uzembe mkubwa.
ReplyDeleteunakamata mchumba bila kumuuliza historia
Unauliza historia na unadanganywa kirahisi, utatufaa kweli? Nimerudi nyuma kukuunga mkono
Bwana SHARORO hapo juu, inaonekana hujafuatilia historia ya Dr. Slaa vizuri. Usiandike kama huna uhakika na kitu. Kwa taarifa yako Dr. Slaa alioa na wameashaachana na mkewe. Halafu wewe sijui unaishi kwenye dunia gani? Hivi kuoa kuna umri wake maalum? Na maana ya ndoa inaonekana bado hujui.
ReplyDeleteIn Europe to have an affair with someone's asset is not wrong,Ni sawa tu Angalia ASHLEY COLE,JOHN TERRY,Je kuna alolipa FIDIA?!! Sikuyajua haya hadi nilipoporwa mke na mfanyakazi mwenzake wa mke wangu!Niliporipoti nikaambiwa hakuna kosa kuanza mahusiano hata ukiwa ndani ya ndoa kwa NCHIYETU*(UK,)if you are more concerned find a solicitor, HAWA MADADA ZETU WA KIBONGO wanadanganyika kidogo tu! mtu akiwa na cheo au hela,Pole mzee tafuta chombo chengine kama nilivotafuta mimi!Nimeshaporwa nimeanza tu kwa kuwa nina rangi nyeusi na alienipora ana rangi nyeupe na kazi.TEH TEHE TEHEE!!!
ReplyDelete