Habari Kaka,

Hiki ni kipande cha video toka kwenye filamu ya Mwamba Ngoma, tusaidie shavu hapo bloguni kwetu.

MAELEZO:

Muziki ni biashara kubwa sana ambayo ikisimamiwa vyema inaweza kuwa na mchango mkubwa katika suala zima la mapato ya serikali. Lakini hata hivyo bado inaonekana kama vile muziki wa Tanzania bado haumfaidishi yeyote kasoro msikilizaji wa kazi hizo.

Tazama video hii umsikie John Kitime, mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, akizungumzia machache yanayokwamisha wadau wa muziki washindwe kuwa na mafanikio kama ya wale wa ughaibuni.

Halafu msikilize kaka Kusaga pia, mmiliki wa radio Clouds, radio ya watu, naye ana ya kwake ya kusema kama mdau wa muziki kwenye sekta ya matangazo.

Pia utapata wasaa wa kumsikiliza MwanaFA, mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye nayo anayo ya kwake ya msingi kabisa yatakayokufungua macho uone imekuwajekuwaje tumekwama hapa tulipo.

Pia ndani ya video hii utapata kuona na kumsikia mmoja wa wasambazaji wakubwa wa kazi za muziki na filamu hapa Tanzania, naye ana yake ya kusema.

Pata elimu-burudani.

Video hii ni kipande kimojawapo kinachotengeneza filamu ya Mwamba Ngoma.

Asante,
www.wahapahapa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Uongo.. eti 20% inatokana na muziki. Please!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...