Wafanyakazi wa Benki ya Azania wakijumuika katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya waliyoifanya katika meli maalumu na baadaye kujumuika katika michezo mbalimbali kisiwani Bongoyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Ni wakati wa vilaji, vitafunwa, Bolingo na ngai
na Bongo Fleva kama kawa...

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (mwenye fulana ya njano) akionyesha umahiri wake katika kusakata mpira wa miguu alipojumuika na wafanyakazi wengine wa benki hiyo katika Kisiwa cha Bongoyo wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.
Bosi kumbe wamo...
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakishuka katika mashua kuelekea katika Kisiwa cha Bongoyo walipojumuika katika michezo mbalimbali katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya walioifanya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Yohana Balele (mwenye suti nyeusi) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw. Charles Singili (kulia) wakizindua rasmi tawi la benki hiyo la Kahama mkoani Shinyanga. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Bw. Andulile Mwakalyelye.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Azania imelenga kupanua huduma zake katika mwaka huu kwa kufungua matawi katika maeneo ya Mbezi Mwisho, Kariakoo, Sam Nujoma, Dar es salaam, Katoro/Biharamulo, Arusha, Lamadi/Simiyu, Kogongwa/Kahama, Geita na Tunduma.

Hatua hii ni mkakati wa kimaendeleo wa benki hiyo katika kujiimarisha kihuduma kwa kuwafikia wateja wengi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba wamefikia hapo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya
menejimenti,wamiliki,wafanyakazi na wateja wa benki hiyo kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw. Charles Singili aliyasema hayo katika hafla yakuukaribisha mwaka mpya iliyofanywa na benki hiyo katika Kisiwa cha Bongoyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Singili alisema benki hiyo inaendelea na mikakati kuhakikisha kuwa huduma zao zinaendelea kuimarika kadri miaka inavyosonga mbele na kwamba uongozi unawashukuru wadau wote wa kibenki waliowawezeshsa kufika hapo walipo..

Kwa upande mwingine alitoa shukrani za pekee kwa wamiliki wa benki hiyo (NSSF, PPF, PSPF, LAPF, EADB) ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa benki hiyo inakua na kuwa imara wakati wote ambapo alitoa rai kwao pamoja na wadau wengine kuongeza bidii ili benki hiyo iweze kupiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo mwaka huu.

“Mafanikio tuliyofikia ni matokeo ya kazi nzuri ya menejimenti ya benki pamoja na wadau mbalimbali wa kibenki wakiwemo wateja wanaounga mkono huduma zetu hivyo tunatoa shukrani kwa jamii nzima ya kitanzania wakiwemo wamiliki wetu kwa kuifanya Azania isonge mbele,” alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na maeneo hayo pia benki hiyo ina mpango wa kufungua matawi mengine katika mikoa ya Dodoma,Morogoro na Mbeya na kwamba upanuzi huu wa huduma utakwenda kwa awamu kulingana na uwezo wa kifedha wa benki.

“Kiukweli tumedhamiria kuendelea kujiimarisha na mpango wetu umelenga zaidi kupanua huduma ili kuwafikia watanzania wengi zaidi, tumepanga kufika kila kona ya nchi na kwamba hilo litaangalia uwezo wetu wa kifedha lakini ni matumaini yetu kuwa malengo yetu yatatimia,” alisema Singili.

Wamiliki Wazalendo wa Benki ya Azania wanayoisimamia kwa miaka kumi ya kujiendesha na kiasi cha hisa wanazomiliki ni NSSF 35%, PPF 30%, PSPF 12%,LAPF 14%, EADB 6% wakati wadau wengine wa kawaida wa kitanzania na wafanyakazi wa benki hiyo wanamiliki 3% ya hisa za jumla za benki hiyo.

Kwa sasa benki hiyo ina mtaji wa sh. bilioni 19/- na wakmba tayari imefungua
matawi saba katika maeneo mbalimbali nchini katika miaka kumi ya kujiendesha tangu ilipoanzishwa rasmi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nyinyi ndio mnajua kula bata hadi raha, heri ya mwa mpya wote kwa ujumla.

    ReplyDelete
  2. Naomba mamlaka husika iangalie upya matumizi ya merikebu hii hasa kubeba abiri ambao wanakuwa wametumia vileo. Ni vema abiria wa chombo hicho wakawa alert endapo hatari itatokea.

    Pili, uongozi wa Azania bancorp uwe makini sana, haiwezekani kuingiza namba ya kubwa ya wafanyakazi wake kweny chombo kama hicho bila ya kufanya risk analysis. What if chombo kinazama au kupata ajali yeyote?

    ReplyDelete
  3. Ila miguu mingine haipendezi kwenye pensi ila utafanyaje sasa kama upo beach

    ReplyDelete
  4. Maendeleo ya benki ok, lakini je hapo, mtaalamu wa mambo ya security/health and safety kweli aliangalia hii ishu ya kuwa kwenye meli, mpata usiku iliangaliwa au bata alikuwa ni lazma aliwe. You people mnaonekana kuwa mmesoma, lakini hapa naona wengi mlifumba macho. Ndio ikitokea ishu inakuwa ni balaa bin mtume, wengine sijui hata kama kuogelea wanajua....
    Vizuri imeisha vyema..

    ReplyDelete
  5. Good to see such football-ing exercise,because, I think this group of office workers need this kind of PE every week. They, in majority, have obnoxiously obesities, the result of beers, nyama choma, (Barbecue) bar soups and a long hour office sitting with limited walking exercises. Guys...PE could serve your life from having heart attacks, diabetes, muscle clump and other diseases and, hence, a happier and longer life. To ensure healthily productivity in many companies, managers are ought to ensure that there is a weekly exercise; get together, as a number one priority for employers and employees. As soon as they do that I think employers will gradually see remarkable reductions in sickness leave, late to work, morning hang overs, and more importantly, employees’ sharpness through their every day duties.

    ReplyDelete
  6. Je wanajuwa kuogelea kama kutakuwa na tatizo? Kuiga kuna mengi!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  7. Kweli tunatanuwa lakini wengine tumetoka vijijini hata maji ya kunywa hakuna sijui kwa nini tunaweka kutanuwambele badala ya kusema ngoja tuone kama mwaka huu tunaweza kukusanya vijisenti tukaweke hata mambomba vijijini kwetu, angalau watu wapate maji inagwa ni bomba moja kaya kumi. Labda tutaendela kutanuwa mambo ya maendela ni mengne ya nchi na vijijini ni tungoje mfadhili.

    ReplyDelete
  8. health and safety issues siyo tu ktk merikebu, pia ktk majengo, mabasi ya abiri, kwenye disco,maji ya kunywa listi ni ndefu.

    Ila ni vizuri kujiuliza kila mara kuwa kuna tahadhari na usalama wa kutosha ktk kila tunachofanya.

    Mdau
    Ktk Space Station
    Outer Space.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...