Arusha Airport

BARUA YA WAZI KWA MH. WAZIRI WA UJENZI

YAH: MATENGENEZO YA SEHEMU YA ABIRIA WANAOSAFIRI NA WANAOWASILI (ARRIVAL / DEPATURE LOUNGE)

Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Kuna habari zisizo rasmi kuwa mfanyabiasahra mwenye asili ya ki-asia anayeendesha bisahara ya mgahawa /restaurant katika kiwanja cha Arusha ndiye aliyepewa kazi ya kufanya matengenezo kuanzia mwezi march 2011 (jina tumelihifadhi).

Tumekuwa tukiona mkandarasi akiingia na kupima maduka ya wafanyakabisahara bila taarifa yeyote ya kimaandishi na hatujawahi kuona tangazo lolote linalohusu kufanyika matenegezo hayo, hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba taratibu za kumpata mzabuni hazikufuatwa.

Kwa maana hiyo kuna uwezekanao mkubwa wa mianya ya rushwa. Mfanyabishara huyo mwenye asili ya ki-asia anamiliki duka la Duty free kiwanja cha Julius nyerere pia kiwanja cha Kilimanjaro.

Sisi Wafanyabiashara tuna wasiwasi kwamba endapo ujenzi huo ambao hakufuata taratibu za gharama za juu sana za matengenezo hayo na kusababisha kodi za pango kuwa juu zaidi ya kawaida kwa wafanyabiahara na hivyo kuwafanya wafanyakabiashara washindwe kumudu gharama za pango maana ana tabia hiyo.

Tunapenda Kutoa Angalizo taratibu za zabuni zifuatwe na zabuni hiyo itangazwe kwenye vyombo vya habari(magazeti,mbao za matangazo n.k)

Tunaomba mamlaka husika zifuataitlie kwa umakini juu ya suala hili

WAFANYABIASHARA KIWANJA CHA NDEGE -ARUSHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hapo hakuna hoja, Labda hiyo ya kupima bila taarifa.
    Vingine ni upuuzi tu -- ana mgahawa, --ana duty free shop, --- ni Muasia!!

    ReplyDelete
  2. Basi ndio hizo zenu. Muasia ni nani, wacheni ubaguzi utawatafuna wenyewe. Mtanzania ana haki, haki haina rangi, kabila wala dini. Hivi mkizungumzia haki za binadamu zinakua binadamu wa rangi gani. Ndio yale yale aliyosema nyerere ikifikia stage ya mwisho ya ubaguzi hata ndani ya makabila yenu mtabaguana kuna kwa mifano hai, wenzetu wachaga wa rombo na wachaga wa wapi sijui hawaelewani na wala hawoani,na kule mara vita vya koo tafauti ni mifano tosha. Kila siku huwa tunawasikia mkipondana. Alipotoa rushwa ulimwona unao ushahidi. Hii blog ina baadhi ya watumiaji sio kwamba hawana elimu, bali hata maarifa ya kawaida hawana. Hata watoto wanaolelewa katika mazingira magumu wana afadhali sana.

    ReplyDelete
  3. Suala hapo ni taratibu za zabuni kufuatwa, kama zilifutwa hakuna mjadala. Wapewe taarifa hao kazi iendelee, tusipende kuonewaonewa huruma watanzania!!!!

    ReplyDelete
  4. hiyo nikweli kabisaa,mimi huyo mze namjuwaa karibia viwanja vyote amewekezaa yeye,na hiyo pia ya kujenga kimya kimya ndio zake kwa kuwa anampa dili muhindi fulani ana kikampuni chake cha architect jina kapouni kipo shopaz.ili afanye kiundugu,mimi mwenyewe nimesha design pale dar airpo.huu ni mwanya wa rushwaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...