Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu akifungua mkutano wa maafisa toka nchi tano wanachama (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda) wanaokutana kujadili mchakato wa kuanzisha sarufi moja itakayo tumika kwa nchi hizo tano leo jijini Arusha. Picha zote na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
Wajumbe katika mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nchi za EUROPA zinazotumia sarafu ya EURO wanajuta kuwa na sarafu moja, si Tanzania 'tunataka' sarafu moja ya AFRIKA-MASHARIKI?

    Sije Tanzania ikawa kama Republic of Ireland, Greece n.k, nadhani huu mchakato wa sarafu moja Afrika mashariki unahitaji kujumuisha wadau wengi ambao siyo wanasiasa au watendaji serikali ili kuweza kupata maoni 'halisi' ya Mtanzania atafaidika vipi.

    ReplyDelete
  2. Acheni kupoteza hela za walipa kodi kwa kuanzisha project ambazo haziwezekani,economic and market imbalance ni kigezo tosha kuwa haiwezekani,angalieni mfano wa effect ya euro katika european union countries na pia tafuta jawabu la kwanini england bado inasuasua kutumia euro,then ndio muanze kuleta hizo topic
    mdau istanbul

    ReplyDelete
  3. Hata mimi naunga mkono maoni ya wadau hapo juu. Kwanza hiyo sarafu itatusaidia nini? ndo itaondoa umasikini? au kuleta machafuko kwanza mambo ya East Africa watu wengi hawataki mlifanya kulazimisha tena mlipounganisha Rwanda na Burundi ndo mlialibi kabisaa make hizo nchi mbili azifai kwa sababu ya ukabila wao. Mimi binafsi siitaji siona maana yake zaidi ya watu wachache tu kujineemesha na East Africa. Mfano bei ya kahawa Uganda iko juu lakini Tanzania tunaambiwa imeshuka na ndo maana wakulima hasa wamipakani kama Karagwe wanawauzia wafanyabiashara wa uganda sasa sarafu ndo itasaidia nini au ni mradi wa watu fulani kujineemesha.
    mdau

    ReplyDelete
  4. Haya mambo ya EA naona tunaburuzana tu, hivi ni vitu gani ambavyo tutaletewa wananchi tupige kura ya maoni? EA wanaamua wanasiasa, dual citizenship wanaamua wanasiasa sasa lini watanzania tutapewa nafasi ya kuamua mambo mazito yatakayobadilisha mipaka yetu, uraia wetu, mifumo yetu ya kifedha na kisiasa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...