Baadhi ya mashuhuda wa kijiji cha Mlumbilo , Kata ya Mtibwa, Mvomero wakinyoosha mikono juu kuashiria walipewa sh; 10,000 na akusaini vocha bila kupata pembejeo za kilimo
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mlumbilo, Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero wakinyopsha mikono juu kuashiria walisaini vocha na kupewa sh 10,000 bila ya kuchukua pembejeo za kilimo
Baadhi ya watuhumiwa wa wizi wa vocha za ruzuku katika kijiji cha Mlumbilo, Kata ya Mtibwa, Mvomero, wakiwa wamefungwa pingu mikonini mwao wakisubiri kufikishwa kituo cha Polisi Mtibwa
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Fatma Mwassa, ( aliyevaa vitenge ) akiambataana na viongozi wengine kwenda Kijiji cha Mlumbilo
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Fatma Mwassa akifafanua jambo kuhusu mbuni zinazotumiwa na mawakala wa pembejeo na watendaji wa vijiji kuhujumu vocha hizo na kuibia seriikali mamilioni ya fedha. Picha na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Mawakala wa usambazaji wa Pembejeo za Vocha za Ruzuku ya Serikali kwa wakulima katika Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Thomas Mushi na mwenzake Eliford Mahenge ni miongoni mwa watu 10 wakiwemo viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mlumbilo , Kata ya Mtibwa , wanaoshikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuhusika na wizi wa vocha za Ruzuku ‘kuchakachua’ kwa nia ya kuibia Serikali mamilioni ya fedha.

Tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti huyo wa mawakala wa vocha za Pembejeo wa Wilaya ya Mvomero lilifanyika jana nyumbani kwake eneo la Madizini, Turiani, baada ya awali kukamatwa kwa wasaidizi wao waliowapatia jukumu la usambazaji wa vocha hizo kwa wakulima wa Vijiji kadhaa vya Kata ya Mtibwa, Turiani na Kibati.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na amri iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Fatma Mwassa, ambaye alifanya ziara ya kushitukiza katika Kijiji cha Mlumbilo kilichopo Kata ya Mtibwa, akiambatana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo na Maofisa mwengine ,mara baada ya kupewa taarifa na wananchi wema juu ya kuwepo kwa uchakachiaji wa vocha hizo.

Wananachi hao walikuwa wakisainishwa vitabu vya vocha ya mbegu, mbolea na kupandia na kukuzia na kupatiwa sh: 10,000 kutoka kwa mawakala hao na kuacha kuchukua pembejeo hizo , ambapo kutokana na mpango huo mawakala wananufaika kwa kupata sh: 44,500 kutoka sh: 54,500 zinazotolewa na Serikali kama Ruzuku ya kuwachangia wakulima.

Waliokamatwa mbali na Mwenyekiti wa Mawakala wa Wilaya ya Mvomero na mwenzake ,ambao wengine ni Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji hicho, Marko Mwakatundu na Mwenyekiti wake Enedeus Mdesa .

Wengine waliotiwa mbaroni ni Wasaidizi wawili wa Mawakala hao, ambao ni Hamis Bakari aliyekuwa mfanyakazi wa ugawaji wa vocha kupitia Wakala Mushi na mwezake Mohamed Juma , ambaye alikuwa akimfanyia shughuli za ugawaji wa vocha hizo wakala Mahenge.

Mbali na hao, wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vocha ya Kijiji, Amani Said pamoja na wajumbe wa Kamati ya Vocha , Benjamini Nzunza , Monica Sanane na Esther Peter .

Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Geoege Mhina, alisema mawakala hao kwa pamoja walipewa Vocha 1,200 zenye thamani y ash: 21,800,000 , zikiwemo za Mbegu , mbolea ya kupandia nay a kukuzia ambazo tayari Serikali imechangia kwa jumla wake sh: 54,500 na mkulima kupaswa kuchangia sh: 81,500 kwa pamoja.

Akizungumizia wizi huyo uliofanywa na Mawakala hao kwa kushirikiana na watendaji wa Serikali ya Kijiji hicho, Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo , ambapo kwa watendaji wa Serikali ya Kijiji pia watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuachishwa kazi mara moja.

Aliwapongeza wananchi wenye uzalendo na nchi yao kwa kuwafichua mawakala na watendaji wao wanaowahujumu na kuwasababishia washindwe kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kujitokesheleza kwa chakula na biashara.

Hata hivyo jinamizi hilo la uchakachuaji wa vocha za ruzuku limejitokeza tena katika Wilaya hiyo muda mfupi baada ya kuanza upya kwa zoezi la usambazaji wa vocha hizo kufuatia kuzitishwa na Mkuu wa Mkoa huo Issa Machibya , mapema Juanuari , mwaka huu kwa ajili ya kuhakikiwa upya kutokana na uchakachuaji uliojitokeza mwishoni mwa mwaka jana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. watu kama hawa nao pia utawakuta wanapiga kelele..."tatizo ni ufisadi"... wakati wao wenyewe ndiyo hivi.

    ReplyDelete
  2. Kutokea mitaani mpaka ngazi za juu wote ni ufisadi tu ila unatofautiana ki jinsi unavyofanye. Nchi imeoza kilamtu anajichukulia chake.Yaani tumepata fikira za kipebari kwenye uchumi wa kicommunist sasa ndio haya tunayaona. There is nothing to much to take ndio hivi kila mtu anajichukulia tu hata visivyochukulika.

    ReplyDelete
  3. Wacha kusingizia ubepari, ni ujinga wa watu wetu ndio umewafikisha hapo, na pia ni kosa la uongozi kutoweka wazi hao wakulima wanatakiwa wapate nini kwenye hizo vocha.

    Kwa mfano ingewekwa wazi tangu mwanzo kuwa hizo vocha thamani yake ni shs 54 elfu hivi watu wangechukua hizi elfu kumi kumi kweli? Hebu ziwekwe wazi kama pesa za MMEM tuone kama wizi wake hautapungua!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...