Kwamba Globu ya Jamii toka izinduliwe kule Helsinki, Finland, mnamo Septemba 8, 2005 sio tu imekuwa blog maarufu ya Kimatumbi duniani bali pia imechangia kwa namna yake maneno kadhaa katika lugha ya Kiswahili kiasi hata si ajabu yakakubalika kuwa maneno rasmi katika kamusi?

Yafuatayo ni baadhi ya maneno ama misemo ambayo Globu ya Jamii imeweza kuyaibua na kuyafanya yakubalike na kufahamika  katika jamii, pamoja na tafsiri zake:

*MDAU: (Hakuna neno kama hili ila ni ‘Mshika Dau’ ama ‘Washika Dau’ (Stakeholder/holders kwa kimombo) ila baada ya promo nzito limekubalika kama lilivyo na kujulikana
*KUCHAFUA HALI YA HEWA: Neno la kistaarabu ambalo Globu ya Jamii imelipromoti kumaanisha matusi ama tusi ama mtu ama watu kufanya isivyo ndivyo.
*MAI WAIFU/HAZBENDI: Ni neon lililokuwepo siku nyingi, ila limekubalika kama kitajio cha mke/mume wa mtu
*HEPI BESDEI YA KUZALIWA: Siku ya kuzaliwa (Happy Birthday)
*WAOSHA VINYWA: Wakosoaji
*BARABARA YA MOROGORO ROAD: Barabara ya Morogoro
* CHUO KIKUU CHA UNIVERSITY CHA UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM: UDSM
*LIBENEKE: Chanzo ni mtindo wa Bendi ya muziki ya Mara Jazz enzi hizo. Hivi sasa ni aina yoyote ya hali ya maisha ama matukio katika jamii
*KUBEBA BOXI: Kufanya kazi  ughaibuni
*MBEBA BOXI: Mfanyakazazi anayeishi ughaibuni
*MLA VUMBI: Mtanzania anayeishi Tanzania
*NONDOZZZ: Shahada/Stashahada/Cheti cha kufuzu masomo
*MAMBO MSWANO: Mambo mazuri
*MSAADA TUTANI: Ombi la kusaidiwa kitu/Jambo
*BONGO TAMBARARE: Tanzania njema/nzuri
*MASHIMO YA MFALME SULEIMAN: Sehemu za siri za  mwanamke
*KIKOMBE CHA BABU: Sehemu za siri za mwanaume
*PAFYUMU: Harufu mbaya
*KIP LEFTI: Mashimo ya barabarani
*KIKWANGUA/VIKWANGUA ANGA: Ghorofa/Maghorofa
*BWAWA LA MAINI: Liverpool FC
*WAZEE WA DARAJANI: CHELSEA
*WASHIKA BUNDUKI: Arsenal FC
*MAN YU: Manchester United
*BOFYA: Bonyeza kitufe katika kompyuta yako
*MNUSO: Sherehe
*KUMEREMETA: Harusi

Aidha Globu ya Jamii inatoa shukrani kwa wadau wote kwa kuwa nasi muda wote huu na kutuelewa tunasema nini pindi tukitaja moja ya maneno hayo. 

Ikumbukwe kuwa Kiswahili kimeazima takriban maneno zaidi ya 60 toka lugha za Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiingrereza na  nyinginezo kwa minaajiri ya kuiboresha lugha yetu ya Taifa ambayo bado ni change mno mbele ya lugha zilizotukuka. 

Hivyo si vibaya kuiweka hii kama kumbukumbu na hadidu rejea huko mbele ya safari.  Kama kuna tulichosahau kukiweka hapa tunaomba msaada tutani.

-Michuzi
-----------------------
Wadau kadhaa wametukumbusha tuliyosahau kuweka kama ifuatavyo:

AKINA RAS MAKUNJA: Askari wa kutuliza ghasia
MAGITAA YA KINA RAS MAKUNJA: Bunduki wanazobeba FFU
FFU UGHAIBUNI: Ras Makunja na Bendi yake ya Ngoma Afrika
ANKAL: Ankal mwenyewe
ZE FULANAZZZ: T-shirt ya Ankal
KULA KONOZZZ: Kubamba/kukumbatia wakati wa kupiga picha
NANIHII: Kisichotajika ila ni dhahiri kila mtu anajua
WATANI WAJADI: Jirani zetu wa nanihii...
CHAKULA YA USIKU: Mchezo wa baba na mama...
MJI WA KUSOMA: Reading, Uingereza









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2011

    Basi ninaona kama ni hivyo tuifunge kuipumzisha blog yetu kwa muda kwani ninatumia muda mwingi kwenye blog hii ninahitaji likizo, hebu ifunge kwa angalau mwezi mmoja hivi tupumzike! LOL

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2011

    Kaka MISUPU hii ni habari njema na hongera sana kwa hatua kubwa uliyopiga.Mnyaazi MUNGU na aendeleee kukufanyia WEPESI katika shughuli zako za kila siku.Mimi ni mdau mkubwa sana wa blog yako na huwa nafarijika sana nikiwa nazipia habari katika hii blog kila siku na inanipa faraja kubwa sana kuona mambo yanayoendelea nyumbani na ulimwenguni kwa ujumla kwa sababu niko mbali kidogo na NYUMBANI.LIBENEKE OYEEEEEEEEE.BARIKIWA SANA!!!
    Mtanzania Halisi-Kwa BIBI!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2011

    Umesahau haya maneno muhimu sana:
    1. Ankal = Mjomba
    2. Ze fulanaz
    3. Kula konoz
    4. Watani wa jadi,
    ...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2011

    baadhi ya maneno hayastahili kuwekwa kwenye kamusi.yabaki tu kama utani na tuendelee kuwafahamisha watoto wetu kuwa hayana maana vinginevyo tutawaharibu.Mfano globu,hili neno sio sahihi hata kidogo,mai waifu wake,halina maana hata kidogo hata ukilitohoa kwa kiingereza,barabara ya morogoro road,halina maana hata kidogo.mm ninachokiona huwa unafanya utani,labda kuwakeleji wale wasio jua kiingereza kwa sababu kuna watu wanayatumia haya maneno bila kujua kama wanakosea.
    Ninashauri kama mtu uliyekaa sana chumba cha habari,una wajibu wa kuiambia jamii hasa watoto kuwa sio maneno yanayofaa kwa lugha yoyote iwe kiswahili au kiingereza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2011

    umesahau MIKONOZZ

    ReplyDelete
  6. Ankali umeshau moja nadhani,kuna hii kitu yaitwa CHAKULA YA USIKU,hahah!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2011

    Umesahau kina makunja askari wa kutuliza fujo au ffu

    ReplyDelete
  8. Baraka DungaJune 14, 2011

    Kaka Michuzi umesahau kula konoz vile unavopiga picha na wadau mbalimbali.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2011

    Na mengine kama

    GLOBU= Blog

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2011

    Kwa kuongezea...

    FFU WA UGHAIBUNI na bunduki zao-> Bendi ya akina Rasi Makunja na magitaa yao.

    Akina RASI MAKUNJA na magitaa yao-> Askari wa kutuliza ghasia Tz(FFU) na bunduki zao.

    Mdau wa Mashariki ya mbali.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2011

    Mimi nachangia kuhusu mtindo wa Libeneke,mtindo huu ulikuwa ni mtindo uliokuwa ukitumiwa na bendi ya Butiama Jazz na siyo Mara Jazz,Butiama Jazz makao yake yalikuwa Dar,Ukitaka habari zaidi za Butiama Jazz nenda kamuone mzee Alphonce Makello, kama sikosei kwa sasa yupo Shikamoo Jazz.Na kabla ya kuja Dar kujiunga na Butiama Jazz alikuwa kiongozi wa Kilombero Jazz kule Kilombero,Kidatu,Morogoro.
    Yeye ndiye muasisi wa mtindo huu wa Libeneke na ndiye aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Butiama Jazz,pia alikuwa mpiga gitaa mwenye sifa,nakumbuka hata Cosmas Thobias Chidumule alipitia bendi hii enzi hizo.
    Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2011

    ELEKTRONIKI - AFANDE KOVA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2011

    Kwa upande wangu ningeomba baadhi ya maneno yasingewekwa tafsiri yake kama CHAKULA YA USIKU,MASHIMO YA MFALME SULEIMAN,KIKOMBE CHA BABU sababu nawahurumia baadhi ya watoto wa WADAU wanaojifundisha kiswahili humu bloguni.Lol

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 14, 2011

    Umesahau hizi pia:

    MKUU WA WILAYA: Ankal Michuzi mwenyewe
    MITHUPU: Ankal Michuzi mwenyewe
    NEWALA: New York City
    UKEREWE: UK (United Kingdom)
    BUKOBA: Boston, Massachussets

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2011

    Ni kweli Kabisa sisi NGOMA AFRICA BAND tunakubali kabisa kuwa
    Globu hii ya Jamii,imekuwa sauti ya UMMA,na imechangia sana sana katika kukuza lugha,lakini kwa upande wetu sisi wasanii imtusaidia sana kujulikana kitaifa na kimataifa..na kujipatia matamasha mbali mbali..Blog hii imekuwa ikitanuka kuanzia uwekaji wa picha hadi maandishi..na sasa pia video za matukio mbali mbali.
    MUNGU IBARIKI BLOG YA JAMII !
    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    Pia FULANAZ!!!!!!!!!!!! ya ANKAL hisichanike..
    Wadau

    NGOMA AFRICA BAND AKA FFU

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2011

    Maneno hayo yote hayako kitaaluma kabisa sidhani kama tutaitendea haki lugha ya kiswahili kuyatia kwenye kamusi. Yanafaa kutumika kwenye mitaa na blog hizi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2011

    ANKAL UNAJUWA NIMECHEKA MPAKA BASI KUHUSU MACHIMBO YA MFALME SULEIMAN NDIO LEO NIMEIJUWA HIZO ZENGINE NAZIJUWA ANKAL BORA ZINDUA KITABU CHA MAMBO KAMA HAYA ULIYOYAANDIKA JUU HAPO ALAFU ZINDUA SEHEMU NAUHAKIKA JAPO WATANZANIA SI WASOMAJI KITABU ILA KITABU CHA NAMNA HIYO WATASOMA NA KUNUNUWA WENGI.

    MIE NA MALIZIA ANKAL UMESAHAU NA ZILE LALAMIKA INGILISHI NOTI RICHABO FROM MZ.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 15, 2011

    ANKAAAAAAAAAAAAAAL UMENIKUMBUSHA MBALI UNAKUMBUKA SUNDAY,NOVEMBER 25,2007 WATU WALIMTOWA "NISHAI" DADA MMOJA BAADA KUUWA KUHUSU KUSEMA MAI HASIBAND NA MAIWAIFU LOL.... ALIKUTUMIA BARUWA HEBU IWEKE TENA Lol. BWAWA OYEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 15, 2011

    Umesahu east afrika mashariki na kati!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 15, 2011

    FFU mnashangaza,sasa mbona jina lenu la WATOTO WA MBWA mnaliepa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...