Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akimweleza jambo Naibu Waziri wa Utamaduni China Mhe. Madam Zhao Shaohua ( kulia) mara baada ya kuwasiri Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Shaohua amewasiri leo kwa ajiri ya ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo kesho anatarajia kuelekea Dodoma kwa ajiri ya kumtembelea Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.). Pembeni ya Mhe Nyalandu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw.Sethi Kamuhanda.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akimkaribisha Naibu Waziri wa Utamaduni China Mhe. Madam Zhao Shaohua mara baada ya kuwasiri Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Shaohua amewasiri leo kwa ajiri ya ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo kesho anatarajia kuelekea Dodoma kwa ajiri ya kumtembelea Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (Mb.).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2011

    Jamaa kiboko hawa,ni naibu waziri ,anaziara ya siku tatu tu,anaonana na watu muhimu kwa tanzania kama waziri mkuu nk,mission complete.
    Sisi tunatoa macho tu,bado tunashangaa wenzetu washajua nini wanatafuta kwetu kwa faida ya watu wao(wachina kila mahali na kila biashara).
    Sisi viongozi wetu wana msururu wa watu kibao kwenda nje na huwa hawana la maana wanaloendea ,maana hakuna mabadiliko yoyote baada ya ziara zao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2011

    Narudia haya maoni ,wachina wanaleta naibu waziri kwa siku tatu tu,na kashapangiwa kukutana na viongozi muhimu kama vile waziri mkuu nk hivyo mission accomplish kwa raia wao,kununua viwanja na kujitafutia masoko hata ya kandambili(yeboyebo),kuuza maua,kuuza majani.
    Sisi viongozi wetu wanakwenda nje na misafara wa watu teletele na hakuna manufaa yoyote kwa nchi wala kwa walipa kodi,tunabaki tunashangaa kila leo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2011

    Something fishy here!naibu waziri wa VIWANDA anakwenda mpokea naibu waziri wa UTAMADUNI?
    Wshachakachua tayari na washagawana,mama anakuja kufunga mjadala wa miaka 9999 kwa bei ya ubwete.
    Ustaaadh usizuie hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...