Mchezaji wa timu ya Tanzania ya U-23, Jamal Mnyata akijaribu kumtoka beki wa timu ya Seychelles,Bibi Jonathan katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa kumbukumbu za sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Na Woinde Shizza,Globu ya Jamii - Arusha

Mshambuliaji chipukizi wa timu ya taifa ya vijana Thomas Ulimwengu amefunga hati triki kuongoza timu ya vijana U-23 mara baada ya kuizamisha timu ya taifa ya Sheli sheli (Sychelles) magoli matatu kwa moja.

Ulimwengu alianza kuesabu goli la kwanza katika dakika ya pili ya mchezo mara baada y kupokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji Salumu Machaku kabla ya kuongeza bao la pili katika dakika ya 49 kufuatia piga nikupige iliyotokea katika lango la timu ya Sychelles.

Nyota ya Thomasi Ulimwengu ilizidi kung'ara katika dakika ya 61 ya kipindi cha pili pale alipoipatia timu ya taifa ya vijana U-23 goli la tatu baada ya kugonga vyema pasi iliyopigwa na Juma Seif Kijik.

Kwa upande wa timu ya Seychelles walipata goli lao la pekee katika dakika ya 34 kupitia kwa mchezaji wao Laruu Allen baada ya mabeki wa timu ya taifa ya vijana U-23 kuzembea kuokoa mpira katika eneo la hatari.

Kocha wa timu ya vijana aliwatoa wachezaji watatu kwa mpigo Thomas Ulimwengu ,Salumu Machaku na Babu Ally ambapo nafasi zao zilichukuliwa na wachezaji Hussen Javu,Hamis Mcha pamoja na Salum Kanoni.

mara baada ya mechi kumalizika Ripota wa Globu ya Jamii alifanya mahojiano na kocha wa timu ya Tanzania U-23,Jamhuri Kihwelo naye alisema kuwa ushindi wake umepatikana kutokana na timu yake kuwa nzuri pamoja na vijana wake kujianimini,

"mimi naweza sema kuwa ushindi wetu umetokana na sisi wenyewe kuweza kujiamini vijana wangu wanajiamini sana na wanacheza kwa nguvu zote pale wanapokuwa wanacheza na timu kubwa, wanatumia nguvu zaidi pia kuwepo kwa kocha wa timu ya taifa imewaongezea vijana morali ya kucheza"alisema Jamhuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...