1. Hakuna habari ama picha inayowekwa kapuni baada ya kuonekana ukurasa wa kwanza. inahamia ukurasa wa pili ama wa tatu kutokana na wingi wa habari na picha kwa siku.

2. Kuingia ukurasa unaofuata nenda chini kabisa kulia bofya penye 'Habari Zilizopita' utakuwa umepatia

3. Kutafuta habari kwa jina la mtu, sehemu, ama tukio angalia juu kulia na juu ya picha ya Ankal utakuta maneno 'Tafuta chochote hapa' ndani ya kisanduku. Weka mshale wako hapo hayo maneno yatapotea kishwa weka jina la mtu ama kitu ama tukio utavipata bila kelele wala mikwaruzo.


5. Chini ya picha ya Ankal juu kulia pana neno 'Kumbukumbu' ambapo ukibofya utapata kumbukumbu ya Libeneke ya Globu ya Jamii toka lilipoanza rasmi mnamo Septemba 8, 2005 kule Helsinki, Finland. Si vibaya ukatembelea habari na taswira za huko nyuma.

4. Anza namba moja. Hapa hakuna masharti wala vigezo vya kuzingatia. Wewe ni kubofya kwa kwenda mbele kuendelea kufaidi mambo ya Globu ya Jamii.

Libeneke Oye!





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal salam sana kutoka huku ugaibuni,asante sana kwa kutupatia habari mabali mbali za huko nyumbani Tanzania,blog yako ndiyo inayoongoza kwa kupendwa na watanzania tuishio ugaibuni,Ombi langu kuu ni kukuomba ujitahidi kui "activate" blog hii ya jamii ili iwe na speed ya kutosha,maana nadhani kutokana na u bussy uliopo humu blog hii imekuwa slow kila unapo"click"kutoka hatua moja hadi nyingine,kwa hiyo jitahidi kuboresha swala hili,maoni haya ni kwa nia njema na mapenzi ya blog yetu hii ya jamii,daima libeneke litadumu,asante.
    mdau Washington Dc,Usa.

    ReplyDelete
  2. mkuu wa libeneke, libeneke oyeee, hivi mkuuu huwezi kuligeuza libeneke liwe kama forums, nadhani litafunika sana, habari ni nyingi yaaani inakua kazi kubonyeza habari zilizopita, kama ni forum basi habari zinaweza kuwa katika majukwaa mbalimbali mfano siasa , uchumi, burudani nk, nadhani lingevutia sana, au unaonaje mkuu wa libeneke? asante kwa habari za nyumbani

    ReplyDelete
  3. Ikiwa forum itakuwa mbaya.. hivi hivi ndio poa.. hamna haja ya kuchagua.. we unasoma kila kilichomo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...