Mh.Balozi wa Tanzania Bi Mwanaidi Majar pia alihudhuria

Baadhi ya Watanzania wanaoishi DMV walitikia wito wa kumshindikiza ndugiyao mpendwa Marehemu Kidee Bendera jana jumamosi.

Watanzania wakiwa katika mstari wa kumuaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho

  
Mdhamini wa pendo la Peter Walden kushoto akifatiwa na Peter Walden mwenyewe kwenye mstari wa kwensa kuaga mwei wa Marehemu.

Mh. Mama Munanka akitoa salam zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Kidee Bendera. ndani ya kanisa  la  Calvary Lutheran liliopo mitaa ya Georgia Ave. Silver Spring Maryland

Watanzania wanaoishi hapa Maryland waliochangia kwa hali na mali pia walionekana kufurika katika Misa ya ndugu yao Marehemu Kidee Jana Aug 20,2011 kwenye kanisa la Calvary Lutheran Silver Spring Maryland.
  
Kaka Peter Ligate (kulia) akiwa na Mume wa Marehemu Kidee Bendera Cliford Tazanu.
Mh. Balozi wa Tanzania Bi Mwanaidi Majar akipata picha ya pamoja njee ya kanisa la Calvary Lutheran lililopo mitaa ya  Goergia Ave. Silver Spring Maryland Nchini Marekani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community Washington  Metropolitan (TAMCO) akiwa na Mh Abass Misana akiwa na Watanzania wezake kwenye Misa ya ndugiyao mpendwa Marehemu Kidee Bendera Iliofanyika katika kanisa la Calvary Lutheran Silver Spring Maryland Marekani.

Mh Oska akitoa mkono wa kuaaga!

Swahilivilla: Siku zote sitoacha kusema hili Watanzania Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo pamoja na  mitazamo ya wengine, mchango wako katika kazi yoyote ulenge kujenga jamii yenye kujitambua, kujithamini na kujiwajibisha, pale panapo mahitaji kuhusu jamii yetu kwajumla. 

Hii nikuonyesha Amani, maelewana, upendo, na ustahi wajamii yetu hii tuipendayo katika kipindi hiki kigumu kilichotukabili. M/mungu atualie Imani, upendo na mshikamano katika jambo kama hili ambalo kila mmoja wetu liponjiani kumtokea. (Kila kilichoumbwa hakikosi kuonja mauti) Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki Watanzania walio kila pembe ya dunia hii Amin.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa, Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Wamenifurahisha sana wanaume wetu wa kibongo, wamebeba watoto wao kwa mapenzi na mabusu, sio wazazi wetu jamani hapo ingeonekana kakaliwa na mwanamke wakati ni love tu wazee.

    ReplyDelete
  2. Mtoto mali ughaibuni ndio viza hiyo na mabenefit!!

    ReplyDelete
  3. Huyu mtu anayesema mabenefit anaishi marekani au??? Who told you? Unless untaka kujidhalilisha kuwa section-8! na umtafukuze mume ndiyo utaiona hiyo hela ya serikali which is going to end soon! Karibu uje uze mtoto huku utaona unavyogawana mshahara na mayaya. Ndiyo maana tunawabeba everywhere we go hata kazini wangeruhusu watoto ningebeba wakwangu maana its too stressful and expensive kutunza watoto huku. Hakuna cha jirani u gat to pay hourly or daily, akiwa mchanga anajinyea na kujikojolea its even worse utalipa mshahara wote rate za day-care ni zaidi ya dola 1000 kwa mwezi upo hapo|??????????

    ReplyDelete
  4. Anony wa pili ninaomba ufafanue zaidi maelezo yako. Pia ningeshukuru kama ungenijulisha/tujulisha wewe uko ughaibuni ya nchi gani. Ni vema kuwa mkweli kuliko kusema uongo,ali mladi uonekane kuwa una good time huko uliko. Watu wamejikamua kwa upendo kusafilisha miili ya ndugu zao nyumbani, wewe unasema benefit!!?? Mwajili gani atakaesafilisha mwili toka Babiloni hadi Bongo?

    Asante sana anony wa pili kwa kusema machache na yaliyo ya kweli tupu. Tukisema ukweli siku zote tunaelimishana katika jamii. Lakini tukisema uongo tunadanganyana na kutumbukizana shimomi. Fikiri sana kabla ya kuandika. Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...