Mwenyekiti wa Baraza la Michezi la Taifa (BMT), akizungumza jana mchana katika ufunguzi rasmi wa kambi ya  mchezo wa Tennis, katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana. Kanali kipingu alisema kuwa hakuna namna nyingine ya kupata wachezaji bora na timu bora zidi ya kuwekeza michezo kwa watoto. Hivyo alitoa ushauri kwa Serikali na wadau wapenda michezo kuelekeza nguvu zao katika kuibua na kukuza vipaji vya michezo vya watoto.
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Tanga Cementi,Erick Westerberg,akielezea kwa waandishi wa habari jana mchana katika viwanja vya Gymkhana, namna kampuni hiyo  ilijidhatiti kudhamini kambi ya watoto wadogo wachezaji wa mpira waTennis. Westerberg alisema kuwa Simba Cement, imeamua kudhamini ´kambi ya mchezo huo kwa lengo la kukuza vipaji vya watoto na kwa kuthamini umuhimu wa michezo nchini hususani kwa rika la vijana na watoto.
Kocha wa kimataifa waTennis,Fabrizio Coldarone, akizungumza´na waandishi wa habari jana kuhusu ujio wake na nini Watanzania watarajie kutoka kwake.Alisema kuwa atajitahidi kuwafundisha wachezaji hao chipukizi jinsi ya kucheza mchezo huo kwa kiwango cha Kimataifa.
Baadhi ya wachezaji chipukizi wa Tennis, wakiwa katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam Jana mchana. Picha na zote  na Victor Makinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...