Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo akiwavalisha medali wachezaji wa timu ya gofu Wanawake Tanzania.
 Meneja wa kilaji cha Jamii cha Ndovu Special  Malt cha Tanzania Breweries Limited  ambao walidhamini michuano hii, Bi. Pamela Kikuli  (fulana ya kijani) akiwa  na baadhi ya wachezaji wa timu ya Gofu ya Wanawake Tanzania wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi iliyofanyika jana jioni katika viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar. Kulia ni Hawa Wanyeche,na watatu kulia ni Nahodha wa timu hiyo Madina Iddi  na kushoto ni mmoja ya wachezaji nyota Angel Eaton. 

Tanzania Ladies Golf Union ilianzishwa mwaka 1992 and ikasajiliwa na Baraza la Michezo la Taifa. Chama hiki kilianzishwa ili kuwapa nafasi wanawake wa rika zote kwenye mchezo huu wa Golf.


Tanzania ndio waandaaji wakuu wa michuano hii ya chalenji ya gofu ya Afrika mashariki ya mwaka 2011. Timu zilizoshiriki zilikuwa ni Zambia, Kenya, Uganda na Tanzania, na timu ya Tanzaia (Tanzanite) iliibuka na ushindi.

Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli, alisema  Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Ndovu Special Malt, kinatambua umuhimu wa kuinua vipaji mbalimablai, ikiwemo mchezo huu wa Gofu. Ndovu Special Malt imekuwa na inaahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuinua vipaji kama hivi.
 Wachezaji wa Tanzania wakishangilia ubingwa wao
Bi. Monica Ntege akiwavalisha medali wachezaji wa timu ya gofu Wanawake ya Zambia  kwa kuibuka washindi wa pili katika michuano hiyo iliyofikia tamati jana  katika viwanja vya Lugalo,jijini Dar.
 Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Mbonile Burton akizungumza machache mbele ya mgeni rasmi pamoja na wageni mbalimbali waliofika kwenye tamati ya michuano hiyo,kwenye viwanja vya Gofu,Lugalo jijini Dar.
 Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Zambia,Moono Mwila pichani kushoto akimkabidhi zawadi ya bendera ya chama chakeRais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Uganda Dr Rose Azuba kuonyesha ushirikiano mzuri kwenye michezo.
Wageni waalikwa mbalimbali walifika kushuhudia tukio hilo .
 Timu ya Gofu Wanawake Tanzania wakishangilia jambo.Timu hiyo imeibuka kinara kwenye michuano ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania iliyofunguliwa mnamo Agosti 16 kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar na kufikia tamati jana. Ndovu walidhamini michuano hiyo
 Mfunguzi wa Michuano hiyo ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyokuwa ikishirikisha Mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania,Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Tanzania, Jenerali George Waitara
akimkabidhi trofi Nahodha wa Timu ya Gofu Wanawake Tanzania,Madina Iddi
 Timu ya gofu Wanawake Uganda nao wakikabidhiwa zawadi zao pamoja na Medali,ambao waliibuka washindi wa nne katika michuano hiyo.
Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Mbonile Burton akiwakabidhi zawadi wachezaji wa timu ya Gofu Wanawake ya Kenya,ambao waliibuka washindi watatu katika michuano hiyo.
.
 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo akikabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha Madina Iddi,mara baada ya kuibusha washindi katika mashindano
ya Gofu ya wanawake kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati,ambapo Tanzania waliibuka Washindi.Michuano hiyo ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania, ilifunguliwa mnamo Agosti 16 kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar na kufikia tamati jana,Agosti 18
 Timu ya Gofu Wanawake Tanzania wakiwa na baadhi ya Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kombe lao,kwa ushindi wao mnono walioiubuka nao kwenye michuano ya Chalenji ya gofu kwa wanawake iliyoshirikisha mataifa manne Kenya, Uganda, Zambia na wenyeji Tanzania 
 Baada ya kukabidhiwa kombe kwa timu ya Tanzania,ilikuwa ni furaha na vifijo kwa wadau wa mchezo huo
Timu ya Tanzania na makombe yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Congratulations Ndovu for sponsoring this event. We Golf enthusiasts are very grateful that you have shown the way to others that such so called unpopular sports discipline should also be promoted this way. Kudos to organisers and Kudos to Ndovu!!

    ReplyDelete
  2. Dah! Mbona mmetunyima uhondo jamani, kumbe kulikuwa na michuano makubwa namna hii, nasi hamkutup taarifa za kutosha! Jamani tusiwe wachoyo hivyo jamani. Hata hivyo pongezi kwa waandaaji na wadhamini. Gofu ni mchezo ambao kama utapatiwa kipaumbele kama michezo mingine, Tanzania itafika mbali kimataifa.

    ReplyDelete
  3. Nimefurahi kukuona Mbonile Burton ukifanya vitu vyako kwa Gofu ya wanawake. Unastahili sifa kwa uongozi thabiti. Ila usisahau kueneza mchezo huu adhimu mashuleni, maana huko kuna vipaji lukuki!

    ReplyDelete
  4. Go Mbonile go! show them how its done!

    ReplyDelete
  5. Nilikuwa nasikia tu kuhusu Gofu ya wanawake, nikajua n i blah blah tu. Kumbe kweli Tanzania tuko juu. Hongera sana kinamama kwa kutwa ubingwa!

    ReplyDelete
  6. I am so proud of you girls. Work hard keep it up.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...