Soko la mwanjelwa linavyoteketea kwa moto eneo la sido jijini mbeya,chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijajulikana
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
Baadhi ya  mabanda sokoni hapo tayari yameteketea kabisa na moto
Kama kawaida kikosi cha maigizo cha zimamoto mbeya kimeendeleza libeneke la maigizo yake ya kwenda kwenye tukio na gari bovu ambalo hata maji ya kuzimia moto huo halina.na hapa wanaonekana askari wa kikosi hicho wakibishana huku moto ukiendelea 
Kufa kufaana....... kibaka tayari ameshaiba na huyooo anatimka zake.
Dada nae hayuko nyuma katika la kujisevia bidhaa sokoni hapo, keshachukua kapeti na kutokomea nalo.


kwa picha Zaidi Bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamani kwa nini huu mkoa wa Mbeya una tatizo hili la kuungua masoko ??Kila kukicha soko limeungua nadhani kuna sababu maalum na kunahitajika uchunguzi wa kina.Na tabia ya kushangaza nchini mwetu kwa nini haya mazimamoto huwa yanakuwa mabovu na pia kuenda ktk matukio bila maji ??Hii yote ni watu kutowajibika na pia uongozi mbaya,Tumefikia miaka 50 sasa tangu tupate uhuru wetu na bado tunakuwa na matatizo ya kijinga kama haya,afadhali hata enzi za wakoloni uzembe huu haukuwepo,kujitawala isiwe ndiyo sababu ya kuwa wazembe na kutowajibika katika kazi zetu.kweli bongo tambarare !!!!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana ndugu zangu wa Mbeya.

    Lakini mbona moto umezidi tena kila siku sokoni kunaungua kunani?

    ReplyDelete
  3. Sidhani kama kuna haja ya kuwalalamikia watu wa fire kwa kuwa na magari mabovu. Wakupewa lawama ni serikali kwa kushindwa kutoe vitendea kazi vya kuaminika kwa fire brigades zote za Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Nyie watu wa faya kuweni wabunifu katika kutafuta fedha za kuboresha huduma zenu, sio kila kitu serikali tu. Ninyi pia ni serikali kwa vile mu sehemu yake. Come on guys, change!

    ReplyDelete
  5. We need a special strategy for TZ when dealing with accidents. In this case, there is a fire truck but no water and the truck is not working. Small businesses can not afford fire extinguishers. Fire trucks and fire extinguishers are not manufactured locally. Are they insured? The strategies that are applied in Ughaibuni can not work in TZ. Is there enough funds to finance accident prevention program?

    ReplyDelete
  6. Poleni sana ndugu zangu wa MBEYA, ila kama gari ya zima moto ilifika haina maji kwenye tank lake ni makosa,lawama sijui apewe nani kwani umeme shida ukirudi unaleta maafa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...