KARIBUNI KATIKA BLOG YA WANAFUNZI WOTE
POPOTE TANZANIA (MATUKIO NA WANAVYUO)
Kwanza tunapenda kuwasalimu sana Ndugu walimu na wanafunzi na wadau wote mliopo popote nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla.
Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuwatambukisha kwenu Blog mpya kabisa inayo kwenda kwa jina la MATUKIO NA WANAVYUO ambapo lengo kubwa ni kuwakutanisha wanavyuo wote Nchi nzima na kubadilishana mawazo pia kujua nini kinaendelea kila wakati kupitia mtandao huu.
Hatuna mengi sana ya kuandika hapa kwa maana mtandao wenu unajieleza vizuri kabisa. Pia mtandao huu ni wanavyuo wote waliopo vyuoni sasa na wale walio maliza pia ni wa watanzania wote kwa ujumla kwa maana kuna mambo yanayo wahusu na muhimu.
Tunawaomba mpitie kila kona ya mtandao huu na kutoa maoni kama yapo nini kiongezwe ama kuboreshwa zaidi, Tunawakumbusha tena mtandao huu ni wako. sisi tunaongoza tuu kwa mawasiliano zaidi tutumie Barua pepe kupitia
tunatanguliza shukrani zetu pia atakae pata taarifa hii ampe na mwenzakeAsanteni sana.Matukio na wanavyuo Crew KUTEMBELEA MTANDAO HUU BOFYA HAPA http://www.tzwanavyuo. blogspot.com/
Lengo lingine liwe pia kuweka kumbukumbu ya michango mbalimbali ya kimawazo au mali ambayo hutolewa na wanavyuo (waalimu, wanafunzi na waliowahi kupita katika vyuo)kwa maendeleo ya taifa hili.
ReplyDeleteLakini mbona sijaona promotion vyuo vingine kama vile Sokoine University, Ardhi University na MUHAS (Muhimbili)?
ReplyDeletewadau tunawaomba kama mna Taswira ya hivyo vyuo mtutumie pia tutaweka moja kwa moja pia tunapokea matukio kutoka vyuo vyote na taarifa mbali mbali.. Huu ni mtandao wenu tumeni kupitia twanavyuo@live.com hatuna upendeleo wowote. wala ubaguzi wa chuo fulani
ReplyDeleteMh! wathomi wetu, hawachelewi kujiita kembriji ya tanzania hawa.
ReplyDeleteTunaomba wanavyuo mtuambie maana ya neno "libeneke" ni nini? Sijui kama ni neno la kiswahili sanifu au ni la mtaani. Kumbukeni hii blog ni ya wasomi kwa hiyo hatutarajii muungane na watu wengine kuharibu kiswahili. Tunatarajia blog hii iwe tofauti na blog zingine hasa ukizingatia kwamba ninyi ni wasomi na humu mtatoa ilmu.
ReplyDelete