Asalaam alaykum

Tarehe 10, septemba 2011 ni siku ya majonzi makubwa kwa Zanzibar. Tarehe hiyo imetutia majonzi na simanzi nyoyoni mwetu. Mamia ya Wazanzibari wamepoteza roho katika ajali ya meli ya MV Spice Islander. Kati ya waliopoteza roho zao ni watoto wachanga, watoto wa skuli, maharusi na watu wazima.

Ni kwa masikitiko makubwa tunatanabahi kwamba mayatima wengi, wajane na wakongwe wengi wamepoteza watu waliokuwa wakiwa tegemea. Sasa maisha yao yamekabiliwa na upungufu wa matumaini.

Kwa hivyo ni wajibu wetu kuwathibishia mayatima, wajane na wazee waliopoteza wapenzi wao kwamba tuko pamoja nao na kwamba nasi tulio Denmark na Skandinavia kwa jumla tunaungana na wenzetu Ulimwenguni kote hususan Zanzibar kuhakikisha kwamba majonzi ni yetu sote na sisi vile vile tutajaribu kuweka plasta kwenye jaraha lao zito.

Kwa hvyo tunatangaza kwamba Jumapili ya tarehe 18 septemba, 2011 kutafanywa mkutano wa kukusanya misaada ya kuwapunguzia shida mayatima, wajane, wazee na waathirika wote kwa jumla.

Mkutano utafanyika Tjørnegade 9, 2200 Nørrebro (nyuma ya makaburi ya Nørrebro), kuanzia saa 14:00 hadi 19:00.

Wote mnakaribishwa.
Wasalaam
Dt. Yussuf

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...