Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Bw.Ghonche Materego akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi cheti kipya cha usajili viongozi wa lililokuwa Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) ambalo kwa sasa litajulikana kama Mtandao wa Wasanii Tanzania.
 Mwenyekiti wa iliyokuwa SHIWATA ambayo sasa itajulikana kama Mtandao wa Wasanii Tanzania,Bw.Twalib akipokea cheti cha usajili wa mtandao huo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego.
 Msanii na Mjumbe kutoka iliyokuwa SHIWATA mbayo sasa inakuwa mtandao wa wasanii,Ahmed Olotu a.k.a Mzee Chilo akitoa shukrani kwa Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego.
Sehemu ya wanachama wa SHIWATA waliohudhuria hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti.

Na Mwandishi Wetu

Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) limebadili jina lake rasmi na sasa litajulikana kama Mtandao wa Wasanii Tanzania.

Mabadiliko hayo yamefanywa ili kuendana na mfumo mpya wa utawala unaojengwa na Wasanii wenyewe kwa kuwezeshwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambao unatambua uwepo wa mashirikisho manne ya wasanii ambayo ni la Ufundi, Maonyesho, Filamu na Muziki.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi cheti kipya cha usajili iliyofanyika wiki hii kwenye Ukumbi wa BASATA, Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Ghonche Materego alisema kuwa, jina la SHIWATA limebadilishwa ili kuepuka mkanganyiko katika mfumo huo mpya wa utawala kwenye tasnia ya sanaa.

“Nawapongeza sana kwa uamuzi huu mliouchukua wa kubadili jina, maana ingeleta mkanganyiko kwenye mfumo wa utawala wa sanaa tunaoujenga sasa ambao pia ninyi mmeshiriki kikamilifu kuufanikisha” alisema Materego.

Aliongeza kuwa,utawala wa sanaa unaojengwa na BASATA unawaunganisha wasanii wote nchini kupitia mashirikisho hayo manne ya aina za sanaa zilizopo ambayo wanachama wake ni vyama na mitandao mbalimbali ya wasanii.

Huku akipongeza juhudi na matunda ya mtandao huo,alitoa wito wa kujipanga na kuingia katika moja ya shirikisho la wasanii kwa ajili ya uchaguzi wa mashirikisho unatarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya uongozi wa muda uliokuwepo madarakani kwa mwaka mmoja kumaliza kipindi chake.

Awali Mwenyekiti wa Mtandao huo mpya wa Wasanii,Taalib Kassim aliishukuru BASATA kwa kutambua uwepo wake,na kuahidi kwamba watakuwa bega kwa bega na Baraza katika kuhakikisha tasnia ya sanaa inapiga hatua.

Shirikisho la Wasanii limelazimika kubadili jina lake na kuwa Mtandao wa Wasanii ili kuingia kwenye moja ya mashirikisho ya sanaa yaliyopo kwani kwa mfumo uliopo wa utawala katika tasnia ya sanaa nchini lingebaki pembeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...