Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akibusu pete ya Balozi wa Vatican Nchini, Joseph Chennoth kabla ya mazungumzo yao ofisini kwake jijini Dar es salaam leo. Balozi huyo amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini na alikweda kuaga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Vatican nchini, Joseph Chennoth ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba leo. Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini alikwenda kuaga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Vietinam Nchini, Nguyen Duy Thein kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Vatican ndio inayowagawa watanzania kwa misingi ya kidini na mfumo kristo,jambo la kujiuliza tangia lini nchi moja(Italy) inakuwa na mabalozi wawili ktk nchi moja? Huu ni mkakati wa kuimarisha ukristo kupitia serikali ambayo inatokana na walipa kodi wote na wadini zote. Ikija kwa upande wa waislamu wanataka mahkama ya kadhi kelele zinaanza ooooh watatumia kodi za wananchi kwa dini moja. Mikataba pia aliyo sign lowasa kwa kanisa kupitia serikali ya walipa kodi wote ni dhulma kubwa na ufisadi kwa watanzania.

    ReplyDelete
  2. Ankal nadhani una maana MABALOZI NA SI MALOZI. LOL.

    ReplyDelete
  3. Mdau hapo juu na wengine wana ufahamu mdogo kuhusu MoU kati ya kanisa na serikali na wala sio mkataba. Ni kwamba Kanisa linamiliki hosipitali na shule nyingi na hizi zinatoa huduma kwa watu wote. Kwa yale maeneo ambayo Serikali imeshindwa kujenga mathalani hosipitali za kiwango fulani basi huteua hosipitali moja yenye hadhi ya wilaya, mkoa ama rufaa miongoni mwa zile binafsi na hizi huitwa hosipitali teule. Mfano ni Bugando, KCMC, Hydom, Chimala, Huruma nk. Lutheran wanagenga hosipitali nyingine yenye hadhi ya rufaa Arusha.

    Sasa kwa kuwa ni jukumu la Serikali kutoa huduma ya afya na haina uwezo basi huwa inapeleka madaktari na vifaa vingine vya afya katika hosipali hizi kuziongezea nguvu ili kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi na ndio msingi wa hiyo MoU. Wote ni mashaidi unapoenda KCMC ama Bugando unapata huduma sawa na pengine bora kuliko Muhimbili ama Mbeya na kamwe hutabauliwa kwa namna yeyote ile.

    Kwa hiyo aliyeomba MoU ni serikali na sio Kanisa, Kanisa ni tajiri na linajitegemea kwa mapato ya ndani na misaada toka nje. Mfano mpaka sasa kanisa lina Vyuo vikuu zaidi ya kumi na vingine vingi viko njiani kufunguliwa, watakuja wajukuu zetu wataambia ni MoU ndio iligenga hivyo vyuo.

    Pili Italy na Vatican ni nchi mbili tofauti kabisa ni sawa na Afrika Kusini na Lesotho. Vatikan ni nchi ya Kikatoloki kama ilivyo Iran (Shia), Pakistan (Suni) U.K. (Aglikana), Denmark(Lutheran) n.k. Kama tatizo ni Balozi wa Papa basi tufukuze mabolozi wote wanaowakishisha balozi za kidini.

    Kadhi ataleta fujo tu mf. wakristo wanaoleana na waislam atafanyaje kazi? Kwani wanaomtaka nani kawakataza? Kuna mahakama tayari inatosha, wasiotaka kwenda huko ndio wakayamalize nje ya mahakama huko serikali haihusiki.

    ReplyDelete
  4. anony wa tatu: bwana we achana nae huyo anony. wa kwanza.hao hawaishi kulalamika mambo ya kijingajinga. ni kama vichwa vyao vimejaa maji ya nazi, maana kila siku wanaeleweshwa lakini hawataki kuelewa. mbona mambo mengi wakristo wanatendewa lakini hawalalamiki. mathalani the most recent issue, ibada ya kuwaombea marehemu huko maisara, mbona imeendeshwa kiislamu pekee. kuna uhakika gani kuwa hakukuwa na Mkristo ndani ya meli? lakini kwa kutambua kuwa majority ya wazanzibari ni waislamu tumeamua kuichunia. lakini mngekuwa ni nyie yangeongelewa hadi siku ya kiama. mambo mengine tuwe tunavumiliana jamani, ndio ustaarabu huo. sio kila siku kulalamika tu vitu visivyo na maana. kama kanisa lingekuwa na nia mbaya na waislamu wa nchi hii, huo mpango ungeshindwa kutekelezeka hadi leo hii? ah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...