Uongozi wa Ubalozi wa Sweden ukiwasili Makumbusho ya Taifa.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam Dkt Paul Msemwa akimkaribisha Balozi wa Sweden Nchini Lennarth Hjelåker, kulia ni Msaidizi wa Balozi na Mkuu wa Mashirikiano ya Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Bi Maria Van Berlekom.
 Balozi wa Sweden nchini Mh Lennarth Hjelåker akimshauri jambo Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa baada ya kutembelea mradi.
 Balozi wa Sweden Nchini Mh Bw Lennarth Hjelåker akiliangalia gari lililotumika kumpeleka Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere alipokuwa akipelekwa Uingereza kwa Matibabu na ndipo alipofariki dunia.
 Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa akiutembeza kwenye mradi Uongozi wa Ubalozi wa Sweden Nchini kwenye mradi wa Makumbusho hiyo.


Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa

Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth Hjelåker amefurahishwa na maendeleo yaliyo fikiwa na Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam chini ya Dkt Paul Msemwa kwa kuusimamia mradi mkubwa ulio fadhiliwa na Nchi yake ambao umeshaanza kufanya kazi kama ulivyo kusudiwa.

Hatahivyo Balozi Hjelåker alionesha wasiwasi wake juu ya uendelevu wa mradi huo na  kuushauri Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kuhakikisha unapata kiongozi imara mwenye kupenda maendeleo ya Shirika ili aweze kuusimamia vyema mradi huo na pia kuwatafuta wataalam watakaosaidia kuendesha Mradi na kuwa na mtaalamu wa sanaa ambaye ataweka mikakati endelevu ya shughuli zote za sanaa na Utamaduni zitakazoendeshwa na Mradi huo.

Naye Msaidizi wa Balozi na Mkuu wa Mashirikiano ya Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Bi Maria Van Berlekom ameuelezea mradi huo kuwa ni muhimu  kwa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hasa katika tasnia ya Sanaa na  Utamaduni kwani utakapofunguliwa utatoa fursa kwa wasanii wa Sweden kuja na kufanya maonesho yao kwenye Ukumbi wa kisasa wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambao ni sehemu ya mradi huo.

Zaidi ya kuupongeza Uongozi wa Makumbusho na Nyumba Utamaduni kwa kusimamia vyema ujenzi wa Mradi Bi Berlekom aliongeza kuwa wasanii wakitanzania watanufaika na mradi huu kwani wamepata nafasi ya kuonesha kazi zao, kukutana na wenzao wa nchi za nje ambapo watabadilishana ujuzi na uzoefu wa kazi za sanaa.

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt. Paul Msemwa ameushukuru Ubalozi wa Sweden kwa kuzidi kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwani Mahusiano hayo mazuri yatazidi kuwanufaisha wananchi wa nchi hizi mbili Tanzania na Sweden.

Ziara ya Balozi wa Sweden nchini  Bwana Lennarth Hjelåker ilikuwa na madhumuni ya kumtambulisha kwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Msaidizi wa Balozi na Mkuu wa Mashirikiano ya Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Bi Maria Van Berlekom kama mpango wa kuimarisha Mahusiano kati ya Ubalozi huo na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wizara husika inahitaji sana watu kama Dkt Msemwa. Dude has national interest at heart na anajiweka nyuma ya kila mtu ingawa yuko sehemu ambayo angekuwa mlafi kama wale jamaa wa Mfuko wa Utamaduni, angekua kajichotea kila kitu mpaka mkoko wa Mwl Nyerere! Kunahitajika chombo cha kuadabisha wahujumu wa rasilimali za taifa, kibinafsishe mpaka kuku na stiletto za hawa wevi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...