Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete



Ndugu Watanzania Wenzangu;
Kwa mara nyingine tena naomba tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima, na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi. Mwezi huu tunaoumaliza leo ulijawa na mchanganyiko wa mambo, yalikuwepo mambo ya furaha na ya majonzi.


Tuliuanza mwezi kwa sherehe za Eid El-Fitr, kuadhimisha kumalizika kwa swaumu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Nafurahi kwamba sherehe hizo zilifana na kuisha salama.


Lakini, usiku wa tarehe 10 Septemba, 2011 katika mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar kulitokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyokuwa na watu wengi na shehena kubwa ya mizigo. Mara baada ya taarifa ya ajali kutufikia hatua zilichukuliwa za kuokoa watu, meli na mali iliyokuwamo. 


Bahati nzuri ndugu zetu 619 waliweza kuokolewa wakiwa hai na sasa wanaendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa na kujiletea maendeleo yao. Maiti 203 waliweza kupatikana na kuzikwa kwa heshima. Maiti 197 walipatikana eneo la tukio, tano walipatikana Kenya na mmoja Tanga. Maiti waliopatikana eneo la tukio walizikwa Unguja na wale waliopatikana Kenya na Tanga walizikwa huko huko. Meli iliyozama haikuweza kuopolewa. 


Wataalamu wa uzamiaji wanasema ipo kwenye kina kirefu cha mita 300 ambacho hawakuweza kuifikia. Wao walifikia mita 58 tu. Wametushauri kuwa haitakuwa rahisi kuifikia meli hiyo, hivyo tukubali kuwa ndiyo makazi yake ya kudumu na vyote vilivyokuwamo ndani yake. Kwa kweli hatujui kwa uhakika kama wapo watu waliozama pamoja na meli hiyo au hapana. 


Bahati mbaya idadi kamili ya watu waliokuwamo katika meli hiyo haijulikani kwa uhakika. Orodha rasmi ya wenye meli inaonesha idadi ya watu waliokuwemo kwenye meli wakati inaondoka bandari ya Malindi, Zanzibar kuwa pungufu kuliko idadi ya watu waliookolewa na maiti waliopatikana. Kwa sababu hiyo, huenda wapo watu waliozama na meli na kushindwa kutoka.


Kupata hotuba kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mweshimiwa rais hongera kwa hutuba yako nzuri na nimefurahi sana hasa kwa wale wanaosema kila kukicha hapatawaliki kwani kunanchi isiyotawalika duniani?mibinafsi nashindwa kumshangaa sana mtumzima na akili yake kwa uchuwao wa madaraka eti hakutawaliki wenyewe ni kina nani nchi hii?wakumbuke kuwa sio vijana wote tunao wapenda la hasha tupo wengi tu na ni wasomi tena sio wa udsm kwenye vyo vyenye ubora kidunia tunaipenda nchi yetu na rais wetu mwenzao zambia kaona ndani ya chama chake hakuna watu wa kuweza kumsaidia kuongoza nchi matokeo karudi kulekule ccm hoyeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. mheshimiwa wa kwanza kutoa maoni,
    Si vema kutoa lugha ya kejeli na kujiita wewe ni msomi wa vyuo vyenye ubora kuliko udsm. Ni vema kuzungumzia hotuba ya mh. Rais kama hotuba siyo kuanza ku-attack group fulani ya watu.

    ReplyDelete
  3. kijana katoa mawazo yake sababu kaangalia mkumbo unawakuta vijana wengi wa udsm ndio wanatumiwa kuchafua hali ya hewa nadhani kilichomuuma ni kauli zisizo za kiungwana kusema nchi haitatawalika au hapatakalika hii ni nchi yenu pekee yenu nyie?hiyo ni kerokubwa iliyomfanya kijana huyo mtoamaaoni wa kwanza anayo haki ya kutoa hongera zake kwa kiongozi wake wa nchi na hiyo ndio inatakiwa ukali lazima uwepo tu nadhani ndugu yangu hapo juu umeumia baada ya kauli nzito kutolewa na mweshimiwa raisi wetu sote mpendwa uliona wapi mtu mzima akatishiwa nyao?haiwezekani kabisa kukaakimya kwa ajili yenu no

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...