Kasaloo Kyanga ndie mtunzi wa kibao hiki maarufu, kilirekodiwa RTD Dar es Salaam katika awamu ya pili ya recording za Tancut Almasi. Recording hii ilitaka kuvunja bendi kwa kuwa wakati bendi ikiwa studio, Said Mabela alipita studio na Katibu wa bendi akamuuliza kwa siri anausikiaje muziki? Sijui kwa sababu gani lakini Mabela alijibu, "Hapa hakuna kitu nasikia solo tupu". 

Katibu wa bendi ambaye pia wakati huo alikuwa Katibu wa tawi la JUWATA la Tancut, akawajia juu wanamuziki wa Tancut kuwa wanapiga solo tupu na hivyo waache kurekodi bendi irudi Iringa kwa mazoezi zaidi. 

Ulikuwa ugomvi mkubwa, wakati huo Mabela amekwisha ondoka hata kumuuliza alikuwa ana maana gani haikuwezekana. Fundi wa RTD James Muhilu ndie aliyemtuliza Katibu huyo kuwa nae haelewi maana ya maneno ya Mabela na recording ikaendelea na dunia ikapata bahati ya kusikia kibao hiki.

Ninakwenda safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
Najua hapa utabaki, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mama watafurahi.

Chorus

Safari sio kifo mama iyeeo
subiri ntarudi mama iyeoo

Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili
Nikirudi mama nitakuletea zawadi
Zawadi nono mama watototo
Iyee mama iyee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kawelee ametisha hapo,huyu jamaa alipiga mpini wa uhakika miaka hiyo, big up kawelee, nyuzi umezikwangua.poa sana.Thanks Kitime kwakutudondeshea hii,umenikumbusha mbali sana.Mdau London.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kawelee hakurekodi huu wimbo bali ni Shaban Yohana Wanted

      Delete
  2. Yes, huu ndo muziki wetu na ndiyo hazina ya tanzania siyo Bongo Fleva. Inasikitisha kuona vijna wa Clouds na redio One wanafanya vita baridi kutaka kuua muziki wetu huku wakiubeza muziki wa kuiga na usio na maana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...