Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi fungu la udhamini kwa msanii wa muziki wa Bongo Flava Juma Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa aliyechaguliwa kushindania tuzo za Channel O za Video bora ya Muziki kutoka Afrika Mashariki. Cpwaa alitangazwa kuwa Balozi wa Kili manjaro katika Kampeni ya Jivunie uTanzania.

Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imemtangaza msanii nyota wa muziki wa Bongo Flava, Juma Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa kuwa Balozi wa Bia hiyo hususani katika Kampeni inayoendelea ya Kili Jivunie uTanzania kama sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru.

Hili limebainishwa wakati wa makabidhiano ya tiketi mbili za kusafiri Afrika Kusini kwa hisani ya Kilimanjaro Premium Lager baada ya msanii Cpwaa kuchaguliwa kuwania Tuzo za Video za Channel O. Washindi wa tuzo hizo watatangazwa Ijumaa Novemba 11, 2011 Mjini Sandton, Johannesburg.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema kampuni yake inajivunia kujihusisha na msanii huyo kama njia ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio.

“Akirudi Cpwaa atasaidia katika shughuli mbalimbali za Kili hususan Kampeni inayoendelea ya Jivunie uTanzania,” alisema.

Cpwaa alishinda tuzo mbili wakati wa Tuzo za Muziki Tanzania za mwaka 200/10 na za mwaka huu, 2010/2011 ambapo alishinda katika kundi la video bora ya mwaka. Tuzo hizi zinadhaminiwa na Kilimanjaro premium Lager.

Video ya wimbo wake wa action ambao ulimpa tuzo katika Tanzania Music Awards ndio uliofanya achaguliwe kuwania tuzo ya Chanel O mwaka huu.

Cpwaa ameongozana na Meneja wake Juma Adam Mikidadi, Muongozaji wa video, Luciano Gadie Tsere na maprodyuza wawili wa video. Msanii huyo atatumia safari hii kurekodi video yake mpya.

Kwa upande wake Cpwaa alisema,” Naishukuru sana Kilimanjaro premium Lager kwa msaada huu na hii inadhihirisha wazi nia yake ya kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio.”

Aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Kilimanjaro ili kufanikisha Kampeni yake ya Jivunie uTanzania.

Kampeni hii ilizinduliwa rasmu mwezi Julai mwaka huu kama sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru lengo kuu ikiwa kuwakumbusha Watanzania walikotoka, walipo sasa na wanakokwenda na kikubwa zaidi kuwakumbusha wajivunie mafanikio yakiyopatikana ndani ya miaka 50 ya Uhuru.

Kili inaendelea kufanya tamasha mbalimbali katika mikoa mbalimbali nchini na kilele cha kamppeni hii kitakuwa kupandisha bendera ya Tanzania juu ya Mlima Kilimanjaro siku chache kabla ya sherehe za kitaifa Disemba 9.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. yaani inaniuma sana kuona Kili wasting money and resources katika matamasha. kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mwisho nyinyi ni matamasha tu sasa jamani katika kusheherekea miaka 50 hamuenzi kutofautisha kidogo mkafanya ujenzi wa taifa? vitu kibao mngeweza kufanya ambavyo vingesaidia jamii na wakatihuohuo kutangaza kinywaji chenu. wabongo tunaparty too much instead of kujiletea maendeleo madogo madogo wenyewe, ndugu yangu Kavishe, kama mimi na wewe hatukufanya unategemea nani atafanya? au hiyo miradi ya maji anayotoa mdogo wangu Oriyo ndio mnaona inatosha? with the pulling power you have plus the advertising budget you guys can do a lot more na ni nyinyi vijana wakitanzania wenzetu mnaotakiwa kuwa mstari wa mbele.
    Che

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...