TIMU ya Taifa 'Taifa Stars' imewasili jana usiku hapa N'Djamena tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya.

Timu imefikia hoteli ya Santana, na leo saa 10 jioni kwa saa za hapa itafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya. Kesho mechi itaanza saa 10 kamili jioni ambayo kwa nyumbani ni saa 12 jioni.

Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa beki Erasto Nyoni ambaye ameamka leo asubuhi akiwa na malaria. Kocha Jan Poulsen amesema atatangaza kikosi kitakachoanza mechi ya kesho baada ya mazoezi ya leo jioni.

Waamuzi wote wanatoka Nigeria. Mwamuzi wa kati atakuwa Bunmi Ogunkolade wakati wasaidizi ni Tunde Abidoye na Abel Baba. Kamishna wa mechi ni Hamid Haddadj kutoka Algeria.

Stars imekuja hapa na kikosi cha wachezaji 21 ambacho kitarejea nyumbani siku moja baada ya mechi kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Timu itawasili Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana na kwenda moja kwa moja kambini.

Boniface Wambura
Media Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
+23592159563
N'Djamena

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunawatakia kila la heri.Wambura wambie hao wachezaji wacheze kwa kujituma bwana..Yaani tushindwe kufika hata kwenye hatua ya makundi??Kama vipi tafuteni draw mambo mengine yatajulikana Daresalaam.kupoteza mchezo huo ni kujitafutia matatizo mengine.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...