MAMA YETU VICTORIA WILLNESS LYIMO (19/06/1951 - 16/11/2001)

Yapata miaka kumi sasa tangu Mama yetu mpendwa ulipotutoka. Mpendwa Mama, ulikuwa kiungo kikubwa cha familia yetu na kila siku tunakukumbuka kwa wema wako, ujasiri na upendo uliotufundisha wakati wa uhai wako.

Bila wewe Mama sisi watoto wako tusingekuwa hapa tulipo sasa. Malezi uliyotupatia daima tunamrudishia Mungu sifa na utukufu. Kuondoka kwako duniani pamoja na wapendwa wetu Baba na Dada, kumetuacha na majonzi makubwa lakini siku zote tupo pamoja nanyi kiroho.

Unakumbukwa na watoto wako Jackson, Anitha, Linda, Steven na Emmanuel. Pia unakumbukwa na wajukuu zako ambao hukuweza kuwaona Austin, Isaac na Brianna, bila kuwasahau marafiki, majirani zako na familia yote ya Mtui na Lyimo.

Mwenyezi Mungu aendelee kumpumzisha mahali pema Mama yetu mpendwa.

 Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tutaendelea kukumbuka Mama yetu mpendwa. Bwana ameotoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe.

    ReplyDelete
  2. Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi mama yetu mpwendwa, you were a Mum not only to your children but to the friends of your children also!
    Unakumbukwa sana na Watoto wako wa familia ya Msuya, Sia, Neech, Dayana na Norah

    ReplyDelete
  3. oooh my neighbor ... tunakumiss sana!

    ReplyDelete
  4. R.I.P mama Lyimo. U have the most owesome-est kids and we know u r looking down upon them and u r proud. May God continue blessing ur family forever and ever.
    With love and prayers
    The Mbatta's

    ReplyDelete
  5. R I P Mama, poleni tena wapendwa.

    - Friend from Columbus, OH.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...