wachezaji wa timu ya bunge mara baada ya kumaliza mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakipata maelezo kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Idd Azan, mwenye miwani ni kocha msaidizi Abdul Mteketa.
Kiungo mchezeshaji wa timu ya Bunge, Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' akijaribu kuzuia mpira kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Timu hiyo ya bunge inajiandaa na michuano ya mabunge ya afrika mashariki michuano itakayoanza Novemba 20 nchini Burundi.
Mchezaji wa kutumaini wa timu ya bunge sports, Mahamoud Mgimwa akichuliwa na daktari wa timu hiyo dkt cesilia sanya baada ya kupata majeruhi kufuatia mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na mashindano ya mabunge ya afrika mashariki yatakayofanyika nchini burundi.
namkumbuka huyo mudi alikuwa beki 3 wa akiba pale JKT mafinga OPERATION NIDHAMU 1986-87 almaarufu kama mudi vitumbua big up mbunge
ReplyDeleteIvi hakuna daktari wa kiume kumchua huyo mbunge; mbona mnaleta mambo zenu za ajabu - uyo kazidisha maumivu baada ya kuona daktari wa kike angekuwa wa kiume angepona bila kuchuliwa
ReplyDeleteKikosi cha Bunge la Tanzania kinaundwa na Wabunge pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Bunge ni kikosi imara na kwa taarifa tu Bunge la Tanzania ndio mabingwa watetezi wa Michuano ya Mabunge ya Afrika Mashariki ambayo kwa mara ya mwisho, ilifanyika Arusha 2009. Kila la heri kwa timu yetu, ituwakilishe vyema na kutetea ubingwa.
ReplyDeleteMdau
hakuna timu hapo uzushi tu wengine hapo ndo nitoke vipi mkiwa bungenihamna kitu hata mpira uzushi mtupu
ReplyDeletesasa mbona mdada anatoa huduma ya 1 hata bila kuvaa gloves?
ReplyDeleteDA, MASSAGE HIYO......
ReplyDeletena hiyo timu profesa mwenyewe maji marefu yumo ndani ikifungwa ndio basi tena!
ReplyDeleteAnkali mbona beki sugu hatujamuona na timu meneja mzee cheyo hayupo?
ReplyDeletembona kamati ya ufundi mzee mrema hayupo?
hapo timu haijakamilika bado
Jamani wingi (plural) ya bunge si mabunge=wabunge
ReplyDeleteSawa "walanchi" sasa hivi mnacheza ili kupunguza mafuta ya mlivyokula, sisi "wananchi" tunatoka jasho la damu kwani mafuta hatuna.
ReplyDelete