Mshambuliaji wa Twiga Stars, Asha Rashid ‘Mwalala’ akimtoka beki wa Namibia, Lovisa Mulunga.
 Mashabiki ...
 Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omari akiruka daruga la beki wa Namibia, Esther Amukwaya.
 Wachezaji wa Twiga Stars kutoka kushoto ni, Mwanahamisi Omari, Etoe Mlenzi na Pulkaria Charaji  wakishangilia ushindi wa timu yao.
Kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Namibia wa  kufuzu Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake (AWC) uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 5-2. 
Picha zote Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Aisee ni macho yangu au vp?nahisi km timu yetu inawanaume au ndio mambo yakina Semenya?

    ReplyDelete
  2. Congratulations Twiga Stars!! Mbona uwanja mtupu lakini, kwani viingilio kiasi gani?

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Twiga Stars!Taifa Stars ya wanaume ingevunjwa na tungewekeza kwenye mpira wa wanawake zaidi.Wangepewa kipaumbele zaidi au mechi za Taifa Stars wanaume tungewasilishwa na Twiga stars wanawake;)

    Mtoto wa Kabwela,Sweden.

    ReplyDelete
  4. Hongereni Sana Twiga Stars!

    ReplyDelete
  5. HONGERA TIGWA STARS:

    Ni muhimu tuache hulka mbaya ya upendeleo wa Kijinsia!

    Inaweza tokea katika Familia mtu akawa anawajali zaidi watoto wa Kiume kwa huduma za masomo, malezi na kadhalika na akapuuzia wa Kike, Ilihali ikatokea wa Kike akawa na Faida zaidi kuliko wa Kiume!

    Hakuna sababu ya kupoteza muda na Rasilimali UDHAMINI WA SOKA WA MAMILIONI YA KUTOKA MA BENKI,KAMPUNI ZA MITANDAO NA KAMPUNI ZA POMBE NI BORA YAFUTWE ''TAIFA STARS'' NA BADALA YAKE YAELEKEZWE ''TWIGA STAR''!

    ReplyDelete
  6. hebu siku wachezeshwe twiga na yanga tuone kitakachotokea

    ReplyDelete
  7. HONGERA SANA TWIGA STARS, HONGERA MWALIMU WA TWIGA STARS, WAHAMASISHAJI, NA WATANZANIA KWA UJUMLA. MAZOEZI MUHIMU "KEEP IT UP TWIGA STARS".

    ReplyDelete
  8. This proves, Wacheza Mpira Wanawake ni Bora Kuliko Wanaume (TZ) .

    ReplyDelete
  9. jamani wenzangu wa-tanzania hata jezi zetu za taifa za kushangilia na kushabikia shida?, mnaona wageni wetu hapo full jezi ingawasi sio nchi yao hii....jezi za manu unaweza nunua na kizivaa wakati mpira unaonyeshwa kwenye TV, acheni ubahili na ulimbukeni jamanii:-) alex bura, dar

    ReplyDelete
  10. kikosi kazi cha ukweli jembe

    tuachane na taifa stars sasa tutujiunge kusapoti twiga stars timu ya kweli.

    ReplyDelete
  11. Watanzania 2naweza sema huu unyonge wa kuhusudu vya nje ndio unatudumazaga.

    ReplyDelete
  12. Wallahi mumenipa raha nyinyi mabinti, hongereni sana.

    Way to go Twiga stars onyesha wanaume kwamba you are much better than Kilimanjaro. Tunaomba Mungu pamoja na juhudi zenu mutuletee kombe hapa Tz.

    TWIGA OYYEEEEEEEEEEEE! MBELE KWA MBELE MUSILEWE SIFA BALI MULETE KOMBE NA SISI TUNAWAPA FULL SUPPORT.

    ReplyDelete
  13. Hongera sana Twiga stars, wanawake tunaweza hata bila kuwezeshwaaaa.
    safi sana!

    ReplyDelete
  14. Hongera kaza buti forwards ever backwards never!

    ReplyDelete
  15. Bora Mtoto wa Kike(TWIGA STARS) ambaye ni Mama ntilie ana Faida kwetu ktk Familia kuliko Mtoto wa Kiume(TAIFA STARS) ambaye hana mafanikio kimaisha na kazi yake ni PUSHA WA BANGI!

    ReplyDelete
  16. Go Twiga Go, wafute machozi watanzania ambao siku zote wamekuwa kichwa cha mwendawazimu

    ReplyDelete
  17. Michu ingependeza ungetueleza pia kutoka kulia kwenda kushoto tunawaangalia kina nani.
    Watanzania tunakatisha tamaa sana tunaposhindwa kwenda uwanjani kuwaunga mkono Twiga Stars. Tuujaze uwanja huo jamani.
    Nimeipenda sana hiyo picha ya Mwanahamisi Omari akiruka daluga la beki wa Namibia, Esther Amukwaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...