Msanii Easy Man akikamua stejini. WASANII Dogo Mfaume, Easy Man na kundi la Jaguar jana walifunika vilivyo kwa upande wa Mnanda huku Offside Trick wakisindikizwa na Hammer Q, AT na Shilole wakiangusha bonge la burudani na kuwarusha vilivyo wapenzi wa Mduara waliofurika katika ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem. Bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo nayo haikuwa nyuma kukonga nyoyo za mashabiki wakati washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna wakitikisa na kuwaacha midomo wazi wapenzi wa shangwe mahali hapo. Msanii Izo Business aliyepanda stejini kama ‘surprise’ naye alifanya kweli kwa kuwarusha mashabiki na songi lake kali la Ridhiwan.
AT na Shilole wakiwapagawisha mashabiki.
Msanii aliyepanda stejini kama 'suprise' Izo Business akiwasabahi mashabiki kwa songi lake la Ridhiwan.
Washiriki wa shindano la Vaa, Imba na Cheza kama Rihanna walioingia sita bora wakiwa katika pozi.

Nyomi iliyoitikia shangwe hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ooh wadogo zangu Rihhana alikwenda kujitoa kafara kwa devil worshipper few months ago. Tena hana dini na kila vazi analovaa linamaana kwa hao madevil worshipper i tell you the trueth is not a good person to inspire. Niko Uk kwa muda sasa nawaomba sana msimuige

    ReplyDelete
  2. Ha haha ha ha, mdau hapo juu umeishiwa, who r u to judge?

    ReplyDelete
  3. asante kwa ushauri wako mzuri...watatoa sababu zao kibao lakin angalau we ujumbe umeufikisha kazi kwao...maana wabongo kwa kuiga kiboko

    ReplyDelete
  4. call me old fashion ila hivi ndivo 'unenguaji' huwa kwenye ma-stage??tena public???kaaz kweli kweli....

    ReplyDelete
  5. Mdau wa MaguMarch 13, 2012

    Devil worshiper. Unajuaje unachoamini wewe is non-devil kumbe ni devils pia. kwahiyo suala la imani who is devil, who is not devil ni suala la mtu binafsi. Ukiabudu nini ndio sio devil na kipi ndio GOD? Dini zinawachanganya sana.Fuata dini yako wenzio wewe na dini yako unaonekana unaamunu devils kama wao unavyoawaona wengine. Utakuwa CONFUSED! MY FRIEND believe DIVERSITY uta perish siku hizi watu wa maoni mbalimbali tunaingiliana ktk kazi, buznes,sports utashangaa kukuta kumbe unayoona wewe uko sahihi ni minority.Sijui utajinyonga. POOOOLE.

    ReplyDelete
  6. Kama Rihanna katoa sadaka kwa Mungu wake na mefanikiwa, basi ni changamoto kwako na ww toa sadaka sana kwa huyo Mungu wako ili ufanikiwe. Kama huyo Mungu hakufanikishi basi jiulize km uko njia sawa ndugu.

    ReplyDelete
  7. WEWE DADA MWENYE KAPTULA BLUU,KAPUNGUZE UZITO NA HAYA MANYAMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...