Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman, Jumatatu tarehe 9 Aprili alikutana na Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdullah ili kuwasilisha kopi ya Hati za utambulisho, hatua hii ni ya kwanza kumwezesha kuanza kazi zake ya kuiwakilisha Tanzania nchini Oman kabla ya kuwasilisha hati Original kwa Sultan wa Oman Muadham Qaboos bin Said
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman ( kushoto ) akikabidhi kopi ya hati za utambulisho kwa Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdullah, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman ( kushoto ) akipeana mkono na Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdullah, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nje wa Oman.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman akisaini kitabu cha wageni Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman ( wa pili toka kulia ) katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Balozi Hamad Al Kiyumi, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman, wengine katika picha maafisa wa ubalozi waliombatana na mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh ndugu Abdallah Kilima ( wa kwanza kushoto) na ndugu Said Mussa (wa kwanza kulia ).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...