Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwapungia maelfu ya Watanzania waliofurika katika viwanja vya Jwangani jijini Dar es salaam alikoendesha misa maalum ya ziara yake hiyo Oktoba 1990
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimlisha mkate Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwasili Jangwani
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II na ujumbe wake wa Vatican katika mazungumzo rasmi na serikali ya Tanzania chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 Rais  Ali Hassan Mwinyi akimsindikiza Baba Mtakatifu Papa John Paul II baada ya kuhutubia Jangwani
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimpa zawadi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Mhashama Kardinali  Rugambwa
Baba Mtakatifu Papa John Paul II na mwenyeji wake 
Mhashama Kardinali Rugambwa.
--------------
KUTOKANA NA MAOMBI YA WENGI, SIKU ZA JUMAPILI GLOBU YA JAMII ITAKUWA IKIKULETEA MATUKIO MBALIMBALI  YA KIHISTORIA YA NCHI YETU KUTOKA MAKTABA ZETU KAMA HIVI.

MDAU MWENYE AINA YOYOTE YA TASWIRA ZA KUMBUKUMBU 
ANAZOTAKA KUSHEA NA WADAU USISITE KUTUTUMIA KUPITIA
issamichuzi@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. picha hizi zinatukumbusha watanzania tulikotoka. Tulikuwa na uvumilivu wa imani zetu kwa kiwango cha juu sana. Kitu ambacho kimepungua sana siku hizi. Angalia Raisi Mwinyi na imani yake tofauti how he was so happy with this Pope..kwa kweli..ni vema tukauendeleza huu utamaduni wa kupendana na kuvumiliana.Tuache ubinafsi na kudharau imani za wenzetu. We can make our demands and claims without demonizing each other.

    ReplyDelete
  2. Loh...kumbukumbu nzuri sana..inahuzunisha sehemu fulani fulani lakini ndiyo hali halisi..

    David V

    ReplyDelete
  3. Asante sana Michuzi. Niko interested na ubadilikaji wa utamaduni wa mavazi hasa katika tasnia ya siasa. Nilikuwa nikijiuliza bila jibu ni lini suti ya kwa Mama Malkia ilirejea lini kama vazi rasmi la dola. Hii ni data nzuri kabisa kwamba hadi mwaka 1990 katika hafla rasmi kama hii rais alikuwa bado anavaa suti ya kaunda.

    ReplyDelete
  4. Hello Mdau michuzi,
    Asante sana kwa ukumbusho huu mzuri sana, na Pongezi kwa wazo zuri.Keep it up ,We depend on you!

    ReplyDelete
  5. Maelfu walitoka mbali kwenda Jangwani kumwona na kumsika Pope. Hata waislamu walijazana Jangwani kupata baraka ya Pope! Kumbukumbu nzuri sana! Asante Michuzi!

    ReplyDelete
  6. safi sana umetukumbusha mbali endelea na moyo huohuo michuzi juuuuuu

    ReplyDelete
  7. Michuzi Asante sana kwa ukumbusho huu mzuri na muhimu.

    ReplyDelete
  8. mnyenga johnApril 15, 2012

    Babu kubwa kaka issa.nilikuwa sijaona ziara baba mtakatifu john paulo wakati yupo bongo.asante sana

    ReplyDelete
  9. Mdau hongera kwa kutuletea kumbukumbu hizi muhimu

    ReplyDelete
  10. jamani ici yule kwenye picha ya Tano kulia mwanzoni sio spika bunge wetu mama Annie Makinda,naomba jibu wadau wenye data kamili.
    Mdau-Mtafiti wa mambo.

    ReplyDelete
  11. Aliyeleta utamaduni wa suti ya malkia katika ofisi za serikali alikuwa Mkapa baada ya kuchukua nchi 1995. Alianza kuvaa suti ofisini na maafisa wengine wote wakaanza kuvaa suti.

    ReplyDelete
  12. Nguo zote za malkia, muafirka lake lubega, inayobadilika ni mitindindo, hata sasa mtu akitaka kuvaa kaunda hakatazwi, lubega hakatazwi utashi wa mtu binafsi, Nyerere hakufepologr ionsaryd
    mzuia mtu kuvaa anvyotaka, yeye kaenda china kavutiwa na choinlai kavaa, kavutiwa na kaunda suiti kavaa, watu wamemgeza sasa hoja iko wapi? Eeh wanadamu nyie hamna kheri!

    ReplyDelete
  13. Nilikuwepo hapo jangwani enzi hizo tyulikuwa hatuna hata uwezo wa kujenga majukwaa ya maana na matokeo yake tunajenga majukwaa ya mbao na kuezeka kwa makuti
    tumetoka mbali sana na mpaka hapa tulipofikia tumshukuru mungu.

    ReplyDelete
  14. Wengine wameona makuti sio ya maana wakati bado yanatumika kama urembo wa asili
    Sesophy

    ReplyDelete
  15. Nakumbuka hii ziara nilikuwa shule ya msingi darasa la sita. Nilikwenda kumsikiliza pope. Watu walikuwa Nyomi.

    ReplyDelete
  16. Tanzania ya leo sio Tanzania ya enzi hizo maana kipindi hicho bado wazee wetu walikuwa wanasikilizana, vijana wanaheshimiana, dini na dhehebu vinakunywa pamoja. Leo yako wapi? inafurahisha ukikumbuka nyuma, lakini imauma sana ikitafakari leo. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...