Mratibu wa vipindi wa Radio 5 Prince Baina Kamkulu akimkabidhi mpira wa BBC, Jacob Paulo wa Arusha,huku Mhariri Mkuu wa Michezo wa Radio 5,Willy Protas Cosmas akishuhudia.
Yohane Chance wa Arusha akikabidhiwa mpira wa BBC.
Ibrahim Rashid wa Kaloleni-Arusha akikabidhiwa mpira wa BBC.

kutoka kushoto ni Willy Protas Cosmas,Yohane Chance,Jacob Paulo,Ibrahim Rashid na Prince Baina Kamkulu.Makabidhiano hayo ya mipira yalifanyika katika studio za Radio 5 Arusha Tanzania, huku zoezi kama hilo likitarajiwa kufanyika tena kwa wawakilishi wa Radio hiyo ikiwemo mkoa wa Mbeya, Morogoro na Dodoma.Mhariri wa michezo wa kituo hicho cha Radio Willy Protas Cosmas, amesema kuwa katika mikoa hiyo wamepatikana washindi wa shindano hilo waliokuwa wanatabiri matokeo ya baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya England.Shindano hilo liliendeshwa na Radio 5 kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji la BBC.

Washindi waliokabidhiwa zawadi mkoani Arusha kama 
wanavyoonekana na zawadi zao mikononi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BBC Huwa wabahili sana . Sasa mpira kama mtu hachezi ina maana gani? Mpira ni sh 10,00 tuu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...