Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (wa pili kushoto), akikabidhi moja kati ya mashuka 200 kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Dk. Andrew Lwali, ikiwa ni msaada kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo ilifanyika, Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala wa mfuko huo, Beatus Chiumba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya NHIF, Ali Kiwenge.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi, Dk. Andrew Lwali, akitoa shukrani kwa uongozi wa NHIF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kushoto), akisaidiana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mfuko huo, Ali Kiwenge kutandika kwenye kitanda moja kati ya mashuka 200 yaliyotolewa msaada na NHIF, kwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya NHIF, Ali Kiwenge (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Emmanuel Humba (wa pili kushoto) wakimvalisha vizuri kizibao cha kuakisi mwanga, Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki na Wamiliki Kibaha, Ali Maandiko wakati wa hafla ya kuwahamasisha vijana hao kujiunga na mfuko huo mjini Kibaha, Pwani. Zaidi ya waendesha pikipiki 425 wanatarajia kujiunga na mfuko huo.
Diwani wa Kata ya Maili Moja, Andrew Lugano (kulia), akiwahamasisha waendesha pikipiki kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), mara baada ya viongozi wa mfuko huo kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya tiba kwa njia ya kuchangia kupitia NHIF na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), mjini Kibaha, Pwani.
Waendesha pikipiki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NHIF.

Na Mwandishi Wetu, Kibaha

UONGOZI wa Hospitali ya Tumbi wilayani Kibaha, Pwani umeuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuisaidia vifaa tiba kwa ajili ya upasuaji wa mifupa na macho.

Maombi hayo yalitolewa hospitalini hapo jana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Andrew Lwali wakati akipokea msaada wa mashuka 200 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Emmanuel Humba.

Dk. Lwali alisema kila mwaka hospitali hiyo hupokea wataalam wa mifupa kutoka Cuba ambao wakati mwingine hushindwa kutoa tiba sahihi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa hivyo hulazimika kuwapeleka wagonjwa wao kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI).

Alisema asilimia nane ya majaeruhi wa ajali mbalimbali hapa nchini hutibiwa kwenye hospitali hiyo hivyo upo umuhimu wa kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba hivyo huku akiomba ujenzi wa wodi na eneo kwa ajili ya wanachama wa NHIF.

“Serikali inao utaratibu wa kuleta wataalam wa mifupa kutoka Cuba hao wakija wanafika hapa Tumbi lakini kwa kukosa vifaa vya upasuaji wa mifupa na macho tunashindwa kuwatumia wataalam hao.

“Tuliwaandikia barua kuomba vifaa tiba naamini mtatusaidia hata kwa mkopo… pia tunaomba mtukopeshe ili tuejenge eneo na wodi maalum kwa ajili ya wanachama wa mfuko wa bima ya afya.

“Hii itawasaidia wanachama wa mfuko kufaidi huduma za matibabu na kuona thamani ya pesa wanazochangia,” alisema Dk. Lwali.

Naye Humba aliupongeza uongozi na watumishi wa hospitali hiyo kongwe nchini kwa huduma bora za afya hususan kwa majeruhi wa ajali mbalimbali.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Ally Kiwenge alisema ubora wa huduma za hispitali hiyo umewagusa viongozi wa mfuko na kuamua kusaidia mshuka hayo kama sehemu ya kutambua mchango wao.

Wakati huohuo NHIF ilikabidhi vikoti vya usalama barabarani kwa kikundi cha madereva wa pikipiki 425 wa Kata ya Kibaha Mjini huku ikiwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vikoti hiyo Mwenyekiti wa kikundi hicho Ally Mandiko alisema atawashawishi wamiliki wa pikipiki kuwalipia madereva wa vyombo hivyo vya usafiri kujiunga na CHF.

Madereva wa pikipiki tumetengwa, tunabaguliwa kwenye matibabu hasa linapokua suala la ajili… kule MOI tumetengewa wodi yetu, naamini tukiwa wanachama wa CHF tutapata huduma bora,” alisema Mandiko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...