Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa kata ya Katandala (Hawako Pichani) katika Ofisi za Kata hiyo katika Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye kikao cha Kamati ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Kilimani Azimio ili kuwezesha wanafunzi waliofaulu na kukosa vyumba vya madarasa waweze kwenda Shule kabla ya mwezi huu wa Aprili kuisha.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari Peti Siyame (Dailynews/ Habari Leo, kushoto) na Mussa Mwangoka (Mwananchi, kulia) jana walipotaka kujua juu ya kampeni iliyoanzishwa na Serikali ya Mkoa wa huo katika kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanakwenda shule kabla ya mwezi huu kuisha. Katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William Shimwela. Tangu kampeni hiyo ianzishwe ni wiki moja sasa na tayari wananchi wengi wamehamasika kuchangia.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wakazi wa Kata ya Majengo katika Manispaa ya Sumbawanga huku akiwasisitiza juu ya usafi wa mazingira katika mtaa wao pamoja na kuwaagiza kuchangia katika sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Kata kama ilivyo sera kuu ya Serikali katika Shule hizo kuwa ni shule za jamii hivyo wanapaswa kuchangia na Serikali kuwaongezea nguvu. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera mama kwa juhudi zako, naomba ukaze buti isije ikawa ni show na nguvu ya soda. Ukweli wa mambo ni kuwa tunahitaji viongozi wanaojitoa kimasomaso kama wewe katika kuwahamasisha wanannchi wetu badala ya kukaa maofisini na kutoa maagizo yasiyo na tija.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...