Magari mengi yakiwa yamesimama kwenye foleni kubwa katika njia ya mtaa wa azikiwe street katitaki ya Jiji la Dar wakati huu wa jioni.hali hii imekuja kutokana na mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Dar.
hakuna gari inayosogea hata kwa hatua moja mbele.hapa ni kwenye kip left ya makutano ya Azikiwe na Samora.
Makutano ya Makunganya na Indra ghand pamoja na Kaluta pia hali ni kama hivi.
duh hatar kubwa thana
ReplyDeleteKatika maisha ya Dar, kati ya vitu vinavyo sababisha maisha kuwa magumu ni foleni. Foleni ya Dar inarudisha nyuma maendeleo, inawafanya watu wanakosa raha, wanachoka, wanapoteza muda mwingi sana barabarani, wanapoteza hela za ziada kwa sababu ya mafuta ya magari yao, ajali/kupigana pasi, kumkosea muumba wetu maana kuchomekeana kwingi mwishowe kunasababisha hasira na kutoa matusi kwa wingi.
ReplyDeleteHili ni tatizo kubwa ambalo serikali inatakiwa itafute suluhisho la kudumu. Tunapata hasara kubwa sana, ni kwa vile tu hamna utafiti wa kitaalamu ulishafanyika na kuanika ukweli ya hasara zinazopatikana kutokana na foleni hizi. Kuna uwezekano mkubwa wa kutatua hili tatizo ni kiasi cha kutoa kipaumbele hili tatizo. Manuafaa ya kutatua hili tatizo ni mengi sana kulikoni kuendelea kulifumbia macho.
Nafikiri wakati umefika kujengwe "Metro" Dar.
ReplyDeleteufumbuzi upo tena wa haraka ofisi za serikali zote zingehamishiwa makao makuu Dodoma na pia iwekwe sheria m'bunge yeyote asiruhusiwe kukaa nje ya jimbo lake, mi naona kwa kiasi flani foleni ya magari itapungua 7bu viongozi hawa na watu wao wa karibu ndio wanaomili magari mengi pia msafara wa raisi itakua hamna mara kwa mara watu wa dar hebu tupambane kwa kufikisha mawazo yetu maana watabomoa nyumba mpaka lini?
ReplyDeleteHAki Ya nani Tena Bongo Tambarareeee....AhhhAcha Nibebe BOx tu mie...Bongo Nomaaaaaaa!!!
ReplyDeleteYani jr jana ilikua balaa,wa kule Kijichi hakuna cha daraja wala barabara.Ilinibidi nikodi chata.
ReplyDeleteMama Mimah!