Katibu wa Baraza la Wazee wa muafaka wa Yanga, Ibrahim Akilimali akizungumza katika mkutano wa wanachama zaidi ya 700 wa Klabu ya Yanga uliofanikisha kumng'oa Mwenyekiti wake,Bw. Lloyd Nchunga.Mkutano huo umefanyika leo Kwenye uwanja wa Kaunda uliopo Klabuni hapo,kwenye Makutano ya Mtaa wa Twiga na Jangwani,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Baraza la Wazee wakiongozwa na mzee, Ibrahim Akilimali (wa tatu kushoto) wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Wanachama wa Klabu ya Yanga wakishangilia baada ya kutangaziwa kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Ameng'olewa katika uongozi huo.
wanachama wa Yanga wakijiorodhesha.
Mwenyekiti wa Yanga alieng'olewa uongozi na wanachama wa Yanga zaidi ya 700,Bw. Lloyd Nchunga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2012

    Wazee wa yanga wakiomba dua! Kuwa mzee wa yanga ni lazima uwe mwislamu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2012

    Hiyo dua sijui inahusiana vipi na mambo yenu ya Mpira jamani. Maana hapo kunawashabiki wasioamini Mungu sasa sijui inakuwaje? Acheni kumuingiza Muumba katika mambo ambayo hayahusiani kabisa na mipangilio ya kidini.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2012

    UONGOZI MTAMU, JAMANI LOH! IWE SIASA, MICHEZO,NGO HANGOKI MTU MPAKA ANG'OLEWE KWA NGUVU? KIPIGO CHA 5-0 NA TIMU KAMA SIMBA BADO UNANG'ANG'ANIA?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2012

    Mmeona dua inavyoombwa hapo? tukiwaambia kwamba hizi klabu zina wenyewe mnajifanya hamtaki kuelewa. Llyod Nchunga huwezi kuwa yanga, fullstop. nenda kaongoze timu ya kwenu huko kama ni tarime au mwakareli utajiju.

    Mdau
    Dar-es-salaam young african. (kijana wa kiafrika wa kidarisalama)

    ReplyDelete
  5. Soka bongo sijui litaendelea lini? Yanga akiwa bingwa basi utasikia Simba viongozi wanatolewa na Simba akiwa bingwa utasikia kesi kibao kwa viongozi Yanga. Nchunga anahusiana nini na Yanga ufanya vibaya msimu huu? N Mungu hatakiwa kuhusishwa ka mmabo ya soka na hapo uliletwa udini kana kwamba fans wote wa Yanga ni waislamu, BADILIKENI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2012

    Yanga siyo chama cha siasa na inaruhusiwa kuwa na dini. Ukweli ni kwamba Yanga ni timu ya kiislamu hali kadhalika Simba, Coastal union na African sports za Tanga.
    Kama ambavyo Boston celtic ni timu ya wakatoliki new york rangers ni timu ya walutheri, hii ndiyo hali halisi dunia nzima. Kama hili limewaudhi dawa yake moja tuu, anzisheni timu yenu.
    Mkiona vinaelea mjue vimeundwa.

    Dunia nzima hakuna "establishment" inayodumu miaka mia moja pasipo kuwa na itikadi ya kidini.

    Ndiyo, Yanga na Simba ni Timu za kiislamu na kama uamini picha hizo hapo juu zinajieleza.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2012

    UCHAWI NA USHIRIKINA HAMNA LOLOTE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2012

    Chuki zenu dhidi ya waislamu hazisaidii. Kama mliangalia TV jana ilimuonyesha mkiristo mmoja akiomba kwenye mkutano huo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2012

    Nimefurahishwa sana !!! lazima Nchunga ajue Yanga INA WENYEWE !~ na wenyewe WANA DARISALAMA! WAISLAMU PURE !!! sio yeye alouja na kudai kaijua yanga enzi la Lunyamila ! what a shame! ila na hao Yanga nao wapate fundisho! wakome kuwapa watu uongozi kwa rushwa wanayotoa baada ya hapo wanaanza kulalama! chagueni kati yenu mwanayanga mwennzenu wa damu! na sio huyo alotoka bara aende akafuge ng'ombe tarime !

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2012

    HAHAHA JAMANI MBONA MNA FITNA NYIE??? WAZEE WA YANGA KUSOMA DUA MNASEMA DINI YA KISLAM.... MBONA WIMBO WETU WA TAIFA UMETOKA KTK KITABU CHA MAOMBI CHA KIKATOLIKI NA WATU HATUSEMI?????

    AU KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARA????

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2012

    Klabu hazina dini ila wanachama wanadini zao. Ingekuwa vema nao walokole wanayanga wakemee pepo la kusababisha kifungwa mkoba. Kila mmoja na aombe dua kwa dini yake sema wengine hamjiamini ktk imani yenu, mngelianzisha tu kunena kwa lugha: Shik, shik, Shika yebo rette raba.........nk.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2012

    Eeeh tuachieni Yanga yetu ebo. Yani nyie mmeona dua tu ndo kisingizio cha kuongea. Mimi mnazi wa yanga na mkristo nimeokoka sioni wala sijaona lolote baya hapa. Kipi kibaya watu wakiomba dua? Au ndo mnafuata ya wazungu kwamba kua na imani siku izi ni nongwa? Acheni mambo yenu hayo sisi waafrika tulikua na imani tokea enzi hizo hata kabla ya kuja ukristo na uislamu tuliamini mababu, miti, matambiko na kadhalika. Acheni kutuletea mambo yenu ya wazungu bana kama hamtaki Yanga iwe inaomba dua, nendeni Azam au Mtibwa Sugar, kha.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2012

    Nchunga, itisha mkutano mkuu na ukabidhi mikoba, hali inavyoelekea itakula kwako kwa aibu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2012

    imewauma kuwaona waislam mbele ? usiseme tu km haujaona kitu vizuri mngefatilia taarifa ya habari ya jana ITV wametoa dua moja tu iloombwa nayo iliombwa na padri na wakaitikia wote ktk mkutano ....

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2012

    Toka lini Tanzania kukawa na mpira? Siku zote watu wanasema kuwa Simba na yanga ndiyo wanaoua mpira wa kibongo ni kweli. Sasa jiulizeni, wazee wa Simba na yanga wanasaidia nini hizi timu zaidi ya kuleta migogoro klabuni. Na je, dua na uchaguzi vina uwiano gani ndani ya klabu? Hii nchi bwana yaani kila kitu kinaendeshwa kipuuzi puuzi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...